Mungu ni upendo, Mungu ni mwenye huruma nyingi, Mungu ni bwana wa Haki, Amani na Mwenye Nguvu Nyingi.
Haya maovu yanatoka wapi, au unataka tuamini kuna nguvu nyingine inayomzidi nguvu? Inayoleta hayo huku yeye akiwa hana cha kufanya?
Hili ni swali zuri. Ni swali zuri mno kwa mtu ambaye kwa kweli ni mjinga mno ila ana nia ya dhati ya kujifunza.
Hata hivyo, ni swali la kipumbavu mno kwa mtu ambaye tayari anataka kutumia swali hilo kukana uwepo wa Mungu.
Ndio maana SITALIJIBU.
Mtu anayetaka kutumia hoja au maswali ya namna hii kutetea ukana-Mungu (atheism), huyo anazidi kuthibitisha kile Biblia inasema kwenye suala la uwepo wa Mungu hakuna mjinga, kuna wapumbavu tu. (Zaburi 14:1 na 53:1)
Fikiri, Biblia HAIJAWAHI KUJARIBU HATA SEHEMU MOJA KUTHIBITISHA KUWA MUNGU YUPO!! WEWE NDIO UNAJARIBU KUTHIBITISHA TENA KWA HOJA NAMNA HII!!
KWA NINI BIBLIA HAIJAWAHI KUTHIBITISHA KUHUSU UWEPO WA MUNGU?
KWA SABABU UWEPO WAKE NI TOO OBVIOUS KIASI AMBACHO HAKUNA MWANADAMU MJIGA KIASI HICHO, BALI KUNA WAPUMBAVU KATIKA HILO, NDIO MAANA BIBLIA HAIHITAJI
KUTHIBITISHA UWEPO WA MUNGU.
SIJUI SANA KUHUSU QURAN AU VITABU VYA DINI ZINGINE, ILA UKIONA KITABU CHA KIDINI KINACHOJARIBU KUTHIBITISHA UWEPO WA MUNGU UJUE HIYO NI DINI YA USANII.
Nimeona mnamtaja ndugu mmoja anaitwa Kiranga, naye natamani kujua hoja zake kuhusu Ukanamungu. Huenda akawa na hoja za msingi. Huenda.