Arusha: Mtoto anyongwa na Mfanyakazi wa ndani

Arusha: Mtoto anyongwa na Mfanyakazi wa ndani

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mtoto wa mwaka mmoja, Tifan Osward wa Olasiti Arusha amenyongwa na msaidizi wa kazi za ndani aliyeajiriwa miezi miwili iliyopita.

Msaidizi huyo ambaye ametokea Mkoa wa Mara aliajiriwa na wazazi wa mtoto huyo miezi miwili iliyopita. ACP Justine Masejo, Kamanda wa Polisi Arusha amesema tukio limetokea Juni 19, na wameshamtia mbaroni mtuhumiwa.


1624277302566.png
 
Uzoefu wangu: Baadhi ya watu wa maeneo hayo hawapendi kulazimishwa kufanya kitu ambacho hajaridhia. In hatari sana.

Nakumbuka kulikuwa na issue ya msichana wa miaka 18 ambaye alilazimishwa kuolewa na kijana mmoja ambae inaonekana hakuwemo kabisa katika fikira zake kiasi kwamba hata kujamiiana alikuwa anaona kama kubakwa vile!

Siku ya siku, kasubiri jamaa kapitiwa na usingizi. Alichukua panga tatu za uhakika shingoni.
 
Mtoto wa mwaka mmoja, Tifan Osward wa Olasiti Arusha amenyongwa na msaidizi wa kazi za ndani aliyeajiriwa miezi miwili iliyopita

Msaidizi huyo ambaye ametokea Mkoa wa Mara aliajiriwa na wazazi wa mtoto huyo miezi miwili iliyopita. ACP Justine Masejo, Kamanda wa Polisi Arusha amesema tukio limetokea Juni 19, na wameshamtia mbaroni mtuhumiwa

1624279588112.png
 
Alaa balaa gani hili unaleta mtu awasaidie kulea mtoto nayeye ndio anajeuka ndoto yako mbaya kuwahi kushuhudia live
 
Jeshi la polisi Mkoani Arusha linamshikilia mfanyakazi wa ndani,(jina linahifadhiwa )akituhumiwa kumnyonga hadi kufa Mtoto wa mwajiri wake.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya Sasa 12.00 jioni katika mtaa wa olekerian kata ya Olasiti jijini Arusha.


Kamanda Masejo alisema kuwa Mtoto aliyeuawa ana umri wa mwaka mmoja na nusu na kwamba binti hiyo aliajiriwa kufanya kazi katika nyumba ya Oswald, miezi miwili iliyopita akitokea Mkoani Mara.


Alisema chanzo Cha tukio bado hakijafahamika na mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi na upelelezi utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.


Akiongelea tukio hilo mwenyekiti wa mtaa wa Olekerian ,Aminiel Mollel ameeleza kuwa alipigiwa simu na majirani na baada ya kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa alidai kuwa hilo ni tukio lake la tatu kulifanya kwa kunyonga watoto wa waajiri wake na amekuwa akifanya hivyo kutokana na nguvu za Giza.


"Tulifika na kumkuta mtuhumiwa aliendelea kuosha vyombo bila kujali kuwa ametenda tukio la mauaji ,tulipo mhoji alisema kuwa hilo ni tukio lake la tatu kufanya mauji ya kunyonga watoto akifanya kazi za ndani maeneo tofauti"alisema Mollel.


Aliongeza kuwa mtuhumia huyo amedai kuhusika na matukio mengine mawili ya kunyonga watoto akiwa mfanyakazi wa ndani maeneo tofauti na amekuwa hakamatwi na polisi kwa sababu anatumia nguvu za Giza .
 
Aisee kwa hiyo safari hii nguvu za giza zimeshindwa bila yeye kujua akawa anaosha vyombo akidhani all is well, kumbe is not.
 
Back
Top Bottom