Arusha: Ongezeko kubwa la omba omba mjini, je ni mradi wa watu?

Arusha: Ongezeko kubwa la omba omba mjini, je ni mradi wa watu?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Siku za hivi karibuni kumekuwa na Ongezeko kubwa la omba omba katikati ya jiji la Arusha, kulinganisha na miaka miwili iliyopita.

Miongoni mwa omba omba hao ni wazee, vipofu, viziwi walemvu wa miguu na mikono Watoto, na baadhi yao wanaojifanyisha ni walemavu.

Hali hiyo imekuwa kero sehemu zenye mikusanayiko ya watu kama vile stand, saluni Bar. nk

Peter anasema kuwa omba omba hawa wamekuwa kero haswa wanapokuwa kwenye Bar wakinywa maana kila baada ya dakika kumi lazima apite omba omba huku akinyooshewa mkono kuomba.

Nae Muuzaji wa duka la nguo za watoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Fabiola anasema kuwa ni kweli kuwa kuna ongezeko kubwa la omba omba wa kila aina na hajui wametokea wapi maana ambao hupitia dukani kwake kuomba ni zaidi ya nane kwa siku.

Hadija ni mtoto anaemuongoza babu yake ambae ni kipofu hutembea kutwa nzima katikati ya jiji kuomba anasema kuwa hali duni ya nyumbani ndo inawafanya waje kuomba na babu yake na hivyo jioni hurudi nyumbani na hela kidogo inayotosheleza matumizi ya siku moja na hivyo hulazimika tena kila siku kufanya hivyo bila kupumzika.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wakidai kuwa ongezeko hilo la omba omba mjini ni miradi ya watu ambao huwakusanya omba omba hao kutoka sehemu mbalimbali na kuwaleta mjini kama aina mojawapo ya biashara

Hata hivyo baadhi ya omba omba walioulizwa kama yupo mfadhili anaewafadhili kwa kuwapa hifadhi na ambae jioni huwapelekea mahesabu wamekanusha kwa madai kuwa ni wao wenyewe tu hujitaftia riziki.

16925d394142626e7da38d14dc98deaa.jpg
 
Unakuta mlemavu amewekwa kwenye jua kali siku nzima..analetwa na nani na kuchukuliwa na nani jioni??..huyo anayemleta hawezi kumpambania atleast apate kula bila kuanikwa juani?

Huwa najiuliza tu haya maswali..
 
Ombaomba siku hizi wanamilikiwa na watu. Mwaka jana jijini Nairobi walifanya operation ya ombaomba, na waliokamatwa wengi walitokea Tanzania.

Walipelekwa huko na ''matajiri'' wanaowatumia kuomba. Bila shaka watakuwa wamepelekwa Arusha. Hata wengi wa wanaoonekana Dar wanakuwa na ''matajiri'' wanaowamiliki.
 
Back
Top Bottom