Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akitoa taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema awali mtoto huyu alikuwa ametumwa dukani toka asubuhi lakini hakurejea na ilipofika mchana wazazi wake walianza kumtafuata maeneo mbalimbali baada ya kuingiwa na wasiwasi.
SACP Masejo amesema hadi sasa tunawashikilia watu watatu akiwepo Jaina Mchomvu Mama mwenye nyumba ambaye amekamatwa na askari Polisi huko Mabogini Moshi, Mkoani Kilimanjaro alikokimbilia kujificha baada ya tukio hili kubaainika, mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
SACP Masejo amesema kuwa Baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa Jaina Mchomvu alihojiwa na kukiri kutenda tukio hilo la mauaji ya mtoto huyo.
Amefafanua kuwa Uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali za kiuchunguzi ili kubaini chanzo cha tukio hilo.
Jeshi la Polisi Mkoani humo limewaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu huku Jeshi hilo likiwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kuhusiana na tukio hilo.