DOKEZO Arusha: Pombe iitwayo "Nyingii Nyingii" inavyotesa vijana na kuvimbisha nyuso zao

DOKEZO Arusha: Pombe iitwayo "Nyingii Nyingii" inavyotesa vijana na kuvimbisha nyuso zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Hii ni aina mpya ya pombe ambayo kwa sasa inapatikana jijini hapa, katika baadhi ya maeneo haswa yenye mkusanyiko wa watu wengi wa hali ya chini

Aina hii ya pombe inatengenezwa hapa hapa Arusha haijulikani mchanganyiko wake unatokana na nini na wala haina nembo yoyote yenye kuonyesha asilimia za kilevi ni ngapi.

Pombe hii husafirishwa na madumu ya lita 20 wakati wa kupeleka sokoni (madukani) na ikiwa huko hujazwa kwenye chupa ndogo zilizokwisha tumiwa kulingana na kiasi cha ujazo utakao hata kwenye glass au kikombe unapimiwa pia .
7fe97b5d-16ce-40dd-a6de-8646b119d30a.jpg
Idadi kubwa ya watu haswa vijana wanaotumia pombe hii wananenepa sana usoni pamoja na kukosa hamu ya kula. Huku wengi wao wakiwa wakiwa hawataki kusikia habari za kuwa na familia. (kuoa au kuolewa).

Dereva bajaji mmoja aitwae Joseph anasema kwa Mara ya kwanza kunywa Pombe hiyo itwayo "Nyingii Nyingii." alikunywa ya shilingi elfu mbili na alilala siku mbili bila kuamka wala kujua Bajaji yake aliipaki wapi na tangu siku hiyo ameacha kunywa pombe hiyo.
ab07ec34-da51-4f11-a819-0a96e729fdad.jpg
Nae mama mmoja mkazi wa eneo la ungalimited ambapo Nyingi Nyingi hupatikana kwa wingi alisema kuwa Alikunywa pombe hiyo mara mbili na wala hana hamu nayo tena kutokana na kiwango kikubwa cha ulevi kilichopo Kwenye pombe hiyo.

Wateja wakubwa wa hii pombe ni madereva bodaboda, waokota Machupa,waokota vyuma chakavu, vijana wasiokuwa na ajira rasmi na wale wasiokuwa na ajira yoyote. na baadhi ya wanawake wanaoshinda majumbani na wafanyao shughuli ndogo ndogo,mafundi ujenzi,ikiwa ni pamoja na vijana wa mtaani.
Baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakilalamika vijana wengi kapoteza mwelekeo wa maisha kutokana na upatikanaji wa kila Aina ya pombe kali katika mitaa.
 
Back
Top Bottom