DOKEZO Arusha: Pombe iitwayo "Nyingii Nyingii" inavyotesa vijana na kuvimbisha nyuso zao

DOKEZO Arusha: Pombe iitwayo "Nyingii Nyingii" inavyotesa vijana na kuvimbisha nyuso zao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mbongo sahv we mpe pombe, muweke mziki kwisha kazi
Anasahau kila kitu,yaani kamaliza

Ova
 
Gongo hiyo, huku kwetu Songea Inaitwa SAWANI.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
TBS hawafanyi kazi yao ipasavyo, Arusha kila mtaa utakaopita kuna toleo lake la pombe ya vibobo na ukisoma label unakutana na mhuri wa TBS kuwa inafaa kwa matumizi. HIGHLIFE, SAUWA, DIAMOND ROCK, JAMBO REE, RIVELA, DON NYATI, ZED, MASTA, POWER, TIGER n.k ni pombe ambazo hazikuaswa kuuzwa wala kupewa leseni a kuzalishwa kwa sababu ni hatari kwa afya ya mnywaji na vichupa vyake vinaongozo kuchafua mazingira.
 
Wapi hiy
Hii ni aina mpya ya pombe ambayo kwa sasa inapatikana jijini hapa, katika baadhi ya maeneo haswa yenye mkusanyiko wa watu wengi.

Aina hii ya pombe haijulikani mchanganyiko wake unatokana na nini na wala haina nembo yoyote yenye kuonyesha asilimia za kilevi ni ngapi.

Pombe hii husafirishwa na madumu ya lita 20 wakati wa kupeleka sokoni (madukani) na ikiwa huko hujazwa kwenye chupa ndogo zilizokwisha tumiwa pombe kwa bei ya shilingi elfu moja na elf mbili kulingana na kiasi cha ujazo.
Idadi kubwa ya watu haswa vijana wanaotumia pombe hii wananenepa sana usoni pamoja na kukosa hamu ya kula. Huku wengi wao wakiwa wakiwa hawataki kusikia habari za kuwa na familia. (kuoa au kuolewa).

Dereva bajaji mmoja aitwae Joseph anasema kwa Mara ya kwanza kunywa Pombe hiyo itwayo "Nyingii Nyingii." alikunywa ya shilingi elfu mbili na alilala siku mbili bila kuamka wala kujua Bajaji yake aliipaki wapi na tangu siku hiyo ameacha kunywa pombe hiyo.
Nae mama mmoja mkazi wa eneo la ungalimited ambapo Nyingi Nyingi hupatikana kwa wingi alisema kuwa Alikunywa pombe hiyo mara mbili na wala hana hamu nayo tena kutokana na kiwango kikubwa cha ulevi kilichopo Kwenye pombe hiyo.

Wateja wakubwa wa hii pombe ni madereva bodaboda, waokota Machupa,waokota vyuma chakavu, vijana wasiokuwa na ajira rasmi na wale wasiokuwa na ajira yoyote. na baadhi ya wanawake wanaoshinda majumbani na wafanyao shughuli ndogo ndogo,mafundi ujenzi.
Wapi tupicha picha twa hiyo nyingiii nyingiii
 
Back
Top Bottom