Arusha: Ukikutwa umevaa Suruali ya kubana, Sketi fupi Faini Tsh. 50,000


My sincere apologies kama nimetumia lugha ya kukera accidentally.

Nakuombea kwa Mwenyezi Mungu uwe PhD holder in near future. Naiona hekima kubwa ya kiuongozi na busara nyingi ndani mwako.

Much blessings ndugu Waziri Daktari Gwajima. 🤝🤝🤝

-Kaveli-
 
Uwe na amani tele Kaveli, hakika don't count, kwa umri wangu mm najiona mama kabisa ninayepaswa kuchukulia jambo lolote humu duniani kwa jicho la wema na kutafuta kile chema kilichomo ndani ya mtu yeyote Ili kitumike kwa maendeleo na ustawi wa jamii. Karibu Sana kwenye wizara yako ya jamii. Huku tunahitaji mawazo ya jamii kutoka saiti kabisa, na wewe kipo kitu, tafadhali tupatie tujenge pamoja [emoji1431][emoji1431][emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Hizi sheria sio mbaya sema kuna baadhi huzitumia vibaya. Mwaka huu huko Sanawari kuna mama kampoteza kijana wake baada ya kumkabidhi kwa wanakijiji wamchape hizo fimbo 70 aache tabia mbaya. Dogo alifariki kwa kipigo na mama akatelekezewa maiti.

Pia kusema kuwatoza faini vijana wasio na kazi ni kuzidi kuongeza matatizo yasiyo ya lazima kwenye jamii. Kijana kasoma zake Engineering pale COET karudi kijijini hana kazi mara ghafla kuna watu hawakumaliza hata shule ya msingi wanamkamata na kumchapa fimbo 70 kwamba kakutwa kijiweni. Wazee wa kimeru waache upumbavu. Hizo sheria wajiwekee wao wenyewe ili waache kuuza hovyo maeneo yao.
 
Hujambo? Ahsante kwa kuingia kwenye mjadala wetu. Ila tu ingia tu vzr tutaenda sawa. Unajua nini, mm naona Hawa Wazee wametu challenge sisi hapa ambao wengi wetu tunaona mambo yanaenda mrama lakini wengi tunalalamika tu naku komenti online hatuchukui hatua saiti.

Sasa, faida hapa ni moja tu: Hawa wameanzisha mwendo, hili shukrani kwamba Nia njema wanayo..sasa sisi twendeni tuka regulate mwendo huo usije ukarudi kinyume nyume zikatokea ajali fulani. Sisi tu tutengeneze bond chanya nao..watatuelewa halafu hata hao target group nayo itaelewa tu. Ujenzi wa saikolojia ya jamii unahitaji mazungumzo na kuthamini Kila mmoja anachowaza ilimradi Nia yake njema, basi na wewe ukishathamini mnasikilizana nawe unatia lako mnaenda.

Sijui kama ni mm tu ndiyo nawaza upside down au kuna mtu ananielewa[emoji26]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Kwann wasingeanza vitu vya kidini dini kama mavazi, mikufu na salamu za kidini...
Kwann mtu akutazame Tu ajue dini yako hiyo inaweza leta upendeleo, kuondoa usawa au kunyimwa haki
 
Sijambo shkmoo Mama. Kwanza nikutake radhi kama lugha yoyote mbaya imekukera kwenye comment yangu. Binafsi nimekulia huko Arusha na ninafahamu sana kuhusu hiki ambacho kimekuja kwenye media. Hizo sheria zilizofika kwenye vyombo vya habari sio ngeni kabisa na huwa zinatumika kwa miaka mingi. Kuna kaka yetu alikuwa akinyanyasa sana mke wake kwa vipigo na kutomjali. Alichukuliwa akatandikwa viboko sabini na wazee wa kiarusha. Tatizo linakuja kuna baadhi ya watu wanaotumia vibaya hizo taratibu kufanya unyanyasaji hadi kusababisha vifo na ulemavu. NAUNGA MKONO hoja yako ya ku-regulate hizo taratibu. Serikali iweke mkono wake ili watu wasivuke mipaka na kufanya ukatili. Viboko 70 ni kawaida sana Arusha.
 
Ahsante Sana kwa mchango wako. Hasa uliposema kuwa hizi taratibu zipo kumbe kwenye jamii za huko tangu zamani. Ila sasa ndiyo wanaanza kutoka na kuzisema bayana.

Hii sasa ni hatua nzuri wamefanya kwa kuwa, kisaikolojia sasa wame open up maana yake wako tayari kufikika kwa mazungumzo na maboresho.

Tukiwaendea tukiwa positive hakika watafanya mabadiliko chanya. Tukiwasema sema vibaya wakajua, watajificha tena tutakuwa tunakutana na Matukio tu na aliyefanya tusimjue.

Ahsanteni sana kwa michango yenu. Mm pia nimejifunza mengi, na hii ndiyo njia sahihi ya kushiriki mijadala migumu ya jamii, Hadi wote twende sawa.

Mbarikiwe, usiku mwema. Kama kuna maoni mengine, kesho nitayaona pia.

Kila la heri kwenu wote [emoji1431]

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Tuje na wanaume wasuka nywele,wavaa Heleni puani,vikuku mguuni wanyooshwe

Ova
 
Nimesikia akisema ikioneka kijana hafanyi kazi atapigwa faini Elfu 50.Swali kijana Hana kazi unampiga faini Elfu 50 hio Elfu 50 ataitoa wapi
 
Ila mwamba nimecheka balaaa toa kiduku hicho
 
Kwahiyo bangi na ulevi wa kupindukia Arusha ruksa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…