Arusha: Ukikutwa umevaa Suruali ya kubana, Sketi fupi Faini Tsh. 50,000

Arusha: Ukikutwa umevaa Suruali ya kubana, Sketi fupi Faini Tsh. 50,000

Hawataweza.

Hawataweza ng'oo

Huo muda Kwanza wametoa wapi wa kujadili mavazi ya mtu hizi ni dalili za kukosa Kazi za kufanya.

Maisha yakikaza hata muda wa kuvaa hovyo hawawez kuwaza
Ukienda kwa wameru hizi sheria zipo mda sana na unachapwa viboko kweli kweli hawana masihara
 
Ukianza kuingia kwenye mipaka ya Meru kuwa makin ukileta uduanzi unachapwa 70 chap wadada wa kimeru wanajua likizo hawaendi na vimini meru

Hiyo elf 50 ni kiini macho tu hapo lazima uchezee fimbo hawana shida na hiyo 50
Tumefanana mawazo hiyo faini au kupelekwa mahakamani ni geresha ili wapitishe ila ukikutwa hzo fimbo utakazochezea hutakaa uamini kama upo Tz🤣🤣, kipindi flan wadada walikua wakiwa town wanavaaa vbya kinyama ila mda wa kurudi wakifika maeneo ya jiran wanafunga vitenge siku Moja akijichanganya aisee alitandikwa mpaka akajikojolea
 
Nimesikia Aibu mimi kwa niaba ya Waziri Dorothy Gwajima, Yani Waziri Mzima ana endorse hii taka taka kweli? Sheria za ovyo sana izo tunarudi nyuma aisee
Kwaio kuvua nguo hadharan ndio kwenda mbele
 
Nimesikia Aibu mimi kwa niaba ya Waziri Dorothy Gwajima, Yani Waziri Mzima ana endorse hii taka taka kweli? Sheria za ovyo sana izo tunarudi nyuma aisee
Ukivaa katakundu huko meru umeusha!! Ni taarifa nimekupa
 
Tatizo lako huna akili, we na mbuzi hamna utofauti.... nguruwe pori
Hamna tatizo Mimi kuwa mbuzi au nguruwe pori,maana kama kukosa akili alianza bibi na babu Yako walioshindwa kugundua nguo walikaa uchiiiii mpaka mzungu alipoleta nguo,Sasa hivi usijifanye unazijua sana nguo....
 
Tena nyie wakutokea "daslama" habari iwafikie vizuri msije kusema hamkuambiwa, nyie ndio mnaongoza kwa kutembea uchi hadharani, ole wenu sasa sheeeenzi kabisa 😡
 
Mnakubaliana wachache ili muwakamate na muwaadhibu walio wengi
 
Lazima mdhibitiwe tu hakuna namna. Mmezidi kuvaa na kunyoa minyoo ya kihuni. Dawa yenu ishachemka; kaa tayari kuinywa!
😂😂Hii dunia imebadilika Mzee Acha mawazo ya kizee kudeal na watu ni saikolojia sio nguvu
 
Kutokana na kuporomoka kwa maadili hasa kwa vijana katika maeneo mengi nchini, uongozi wa Kijiji cha Olevolosi, Kata ya Kimnyaki wilayani Arumeru, Mkoa wa Arusha umeweka sheria ndogo mbalimbali na kupitishwa na mkutano mkuu wa kijiji.

Miongoni mwa yaliyopitishwa ni pamoja na kupiga marufuku wasichana au wanawake kuvaa suruali za kubana au sketi fupi 'vimini', kijana wa kiume kusuka nywele au kunyoa pembezoni mwa kichwa na kuacha nywele katikati 'kiduku', kuvaa hereni au kuvaa suruali inayoonyesha makalio na adhabu za makosa hayo ni faini Sh50,000.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa kijiji hicho, Mtendaji wa Kata hiyo ya Kimnyak, Joshua Mollel, aliwasilisha sheria hizo kwa niaba ya mtendaji wa kijiji hicho, ambazo zilipitishwa na mkutano huo.

"Marufuku kwa msichana au mwanamke yoyote kuvaa suruali ya kubana na kuonyesha maungo yake au kimini ukibainika faini yake ni Sh50,000 na kama hauna hapo kuna akina mama walioandaliwa tumeambiwa tuwaletee," amesema.

"Marufuku kwa kijana yoyote wa kiume kusuka nywele au kunyoa pembezoni mwa kichwa,na kuacha katikati ‘kiduku' au kuvaa suruali mlegezo inayoonyesha makalio au kuvaa suruali iliyotobolewa, faini yake ni Sh50,000 na kama huyo kijana hana kuna adhabu nyingine wazee wamependekeza," amesema mtendaji huyo.

Sheria nyingine ni kupiga marufuku kijana wa kiume kuvalia hereni, marufuku kijana mwenye nguvu kutokufanya kazi na atakayeonekana kijiweni asubuhi bila kufanya kazi atatozwa faini Sh50,000, ni kosa kupika au kuuza pombe haramu ya gongo na adhabu yake ni kupelekwa mahakamani na atakayekutwa na anauza pombe muda wa kazi atatoza faini Sh50,000.

Baada ya kusoma mapendekezo hayo ya sheria ndogo hizo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Olevolosi, Emanuel Ngauliva aliuliza wananchi hao walioshiriki kikao hicho endapo wanapitisha sheria hizo, ambapo wananchi hao waliridhia na kuzipitisha kama sheria ndogo.

"Imepita kwa kishindo kuanzia leo ukikamatwa na makosa hayo utapewa akaunti namba utaenda kuweka fedha hizo na kuna kamati husika itafanya hiyo kazi. Kama kuna aliyevaa suruali hapa tuanze kufanya naye kazi hapa kama kuna kijana amenyoa kiduku au amevaa hereni tufanyie kazi hapa na tutakuwa na sungusungu wanapita katika vitongoji kukagua," amesema.

Mmoja wa wananchi hao, Olariv Robert amesema yeye ni miongoni mwa walioshirikiana na viongozi kuunda sheria hizo ndogo kufuatilia matukio yaliyotokea kijijini hapo ya vijana waliouawa kwa kudaiwa kuiba na kuwa waliona hilo limesababishwa na maadili kuporomoka.

"Uongozi wa kijiji na wazee wa ukoo wakakubalia sheria ndogondogo zitumike na sisi kama wananchi tumekutana kupitisha jamii irudi katika mstari wa mbele," amesema.

Naye Lily Lazaro amesema wanaamini sheria hizo zinasaidia kubadili maadili kwa jamii hasa watoto.

Aidha kupitia taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima imepongeza jitihada za kijiji hicho kutunga sheria ndogo hizo zitakazowaongoza kukabiliana na mmomonyoko wa maadili.

Amesema kuwa changamoto ya mmomonyoko wa maadili imezidi kuchukua sura mpya kila siko katika jamii, huku Serikali kwa kushirikiana na wadau ikifanya jitihada mbalimbali kukabiliana na hali hiyo ikiwemo programu zinaziratibiwa na wizara hiyo za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa lengo la kuhakikisha wanakuwa katika misingi bora ya maadili mema.

"Hatua hiyo ni kubwa kwa jamii yetu kuamua yenyewe kutunga sheria zao kuhusu maadili, kwani kila wakati mmekua mkitoa wito kwa viongozi hasa wa mamlaka za serikali za mitaa kubeba ajenda ya kusaidia jamii kwenda mbele hasa katika maadili, fursa za kiuchumi na kupinga ukatili," imesema taarifa hiyo.

MWANANCHI
Punguani hao wa huko Longido Vijijini wanamtishia nani?

Serikali ingilia kati ujinga huu kabla ya kuleta Madhara.
 
Sombetin tu watu wanachezea 70
Sombetini ipi wewe, kuanzia soko mjinga, kwa mjapan, sawmill, kwa mama nairo, kanisani, duka la cement, madukani , kwa shemeji yake mkapa, imani, kwa diwani, shuleni, shuka mpaka ngusero huko hakuna huo upumbavu

Au ulijua unaishi sombetini pekeyako
 
Nimesikia Aibu mimi kwa niaba ya Waziri Dorothy Gwajima, Yani Waziri Mzima ana endorse hii taka taka kweli? Sheria za ovyo sana izo tunarudi nyuma aisee
Hbr za jioni ndugu.

Awali kabisa naomba niwapongeze wote kwa ufuatiliaji wa mijadala ya jamii.

Aidha, niseme kuwa, mimi binafsi sitaona aibu kusema kuwa nimewapongeza jamii hiyo kwanza kwa uthubutu tu wa kubaini kuna changamoto na kuketi pamoja kama jamii ya rika zote kujadili na kukubaliana wao.

Hii kwangu ni ishara kwamba, sasa kumbe jamii yetu imeanza kubaini changamoto na kuzimiliki na kuzijadili na Sasa kinachofuata ni msaada wa kitaalamu Ili mijadala yao isikinzane na sheria mama za nchi na uhuru wa haki za binadamu. Mm nimelitazama hivyo.

Sasa kwa kuwa nyie mmelitazama tofauti, haki yenu kujadili katika jicho lenu. Ila sisi huu ni mwanzo mwema wa jamii Sasa kuanza safari ya mabadiliko ya fikra kwamba wao ndiyo injini ya kujadili changamoto zao na sisi ni wa kupeleka msaada wa kitaalamu Ili wafike salama safari yao pasipo kuathiri sheria kuu zote.

Ruksa kuniona mm siko sawa ila niwaombe tu pia kuwa, ziko Mila au sheria za kijamii huko kwenye maeneo yetu ambazo zina athari kiafya, zinaua na kuleta ulemavu, ningependa pia zianzishiwe mjadala kwani ni dharura.

Ahsanteni sana, tupo pamoja na mawazo tunapokea. Mbarikiwe.

Sent from my CPH2207 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom