Arusha: Wananchi walia na kituo cha mabasi makubwa ya abiria ya kwenda mikoani

Kiufupi Arusha hakuna stendi, kale ka uwanja hakana Hadhi ya kuitwa Stendi kwa Jiji kubwa kama Arusha
 
Acha uongo, hakuna basi la mikoani linaloshusha abiria stendi ndogo! Mbona Dar mabasi mengine yanashusha abiria ktk ofisi zao? Umbea umekuzidi sana utadhani msemaji wa Simba.
 
Ukishuka Ubungo au mbagala kule unakosa usafiri wa kwenda kokote unakotoka? Ukishuka Usagara au Nyegezi pale au Buzuruga kule unakosa magari ya kuunganisha unakotaka?
Wenzetu wamefanikiwa kutanua miji yao kwa kuyeyusha akili zao. Sie tunazigandisha kwa kulazimisha mepesi yanayowezekana yasiwezekane!
Hivi Arusha tunakwama wapi mji wenye jina kubwa duniani kwamba huduma muhimu zote zimejikusanya sehemu moja??
Madini yanaisha na utalii utaisha. Tutumie hizo rasilimali kutanua miji yetu!
 
Maendeleo ya watu na makazi yanahitaji akili tu wala si siasa za majitaka!
Yaani Arusha ni mji lakini ugumu wa kusafiri unasababisha mji kulazimika kulala mapema na kuchelewa kuamka!
Niliwahi kumsikia mwenyeji akilalamika kwanini AUWASA, NIDA na Safari City wamepeleka huduma/miradi yao maporini kuleee Mateves/Kisongo!!
Kwa uzoefu wangu wa Dar na Mwanza nilipata taabu sana kumuelewa!
#Shame
 
Kwa ramani ya mji wa Arusha ulivyo kituo kimoja tu cha mabasi hakitoshi bila kujali kitawekwa wapi!
 
Stendi iimarishwe iwe na ghorofa juu kwa ajili ya abiria na chini ndio parking ya mabasi.Hii iwe kwa mabasi yanayoenda mbali kama dar, nairobi, mwanza, tabora, mbeya nk. Yale ya maeneo ya karibu yatumie stendi ndogo. Hata hivyo kampuni zingine zina ofisi karibu na stendi na hupaki gari zao huko. Kuhamisha stendi ni jambo si jema maana miaka mingi imekuwepo na hivyo mahoteli na maeneo yenye mahitaji ya jamij yanaizunguka. Kuna stendi inaitwa VICTORIA STATION LONDON UINGERZA. ipo katikati ya jiji hilo ina makarne ipo hapo hapo. Kuna siku ile stendi ya Magufuli iliyohamishwa kwanz toka kisutu , halafu ubungo ITAKUJA KUJoNGEA MLANDIZI AU MBELE ZAIDI HUKO DAR.
 
stendi ya sasa haina eneo, pia ujue Arusha haina barabara, yaani Ni finyu sana.
 
Kuna miji inastahili kuwa na stand zaidi ya moja ila Halmashauri hawajaliona hilo, ile ya Arusha ((kama ndio ile ile nayoijua mie ukitokea Sheikh Amri Abeid kwenda Jogoo House maana nilitoka Arusha kitambo) inatakiwa ibaki pale pale na ikajengwa nyingine na ile ikawa ni ya kupita tu hasa magari yanapoingia usiku yaani yanashusha stand hizo za mbali alafu yanamalizia hapo yanaenda ku-park na kujaza mafuta vivyo hivyo asubuhi wakati yanaenda stand kuu yanapita pale yanakula vichwa alafu linaenda stand kuu ila hasara yake abiria wa pale ni kama hisani maana kama gari linaondoka saa 12 alfajiri basi pale linapita mapema zaidi maana safari inahesabiwa kuanzia stand kuu.

Mwanza waliliona hili kitambo sana zaidi ya miaka 15 kwa kuwa na stand ya Nyegezi na Buzuruga yaani hapo gari zinazotokea Nairobi au Musoma zinaishia Buzuruga ila kama zipo zinazounganisha Dar zinashusha hapo na kula vichwa kisha zinakwenda Nyegezi na zinaendelea na safari na gari zikiingia usiku hata jioni zinashusha Nyegezi alafu zinawasogeza abiria Natta (mjini kati) na zingine mpaka Buzuruga. Na katika utaratibu huu wa kujenga stand mpya na zote zinajengwa ila hii ya Buzuruga wametafuta eneo lingine na imeshakamilika bado kuizindua ambapo hii ya zamani inaweza ikatafutiwa matumizi mengine hata kuwa ya daladala au magari ya kwenda vijijini / wilayani.

Mikoa ya Dar, Mwanza, Arusha na Dodoma zinahitaji stand kuu zaidi ya moja, wenzao Mwanza walishaonyesha mfano tangu kitambo na sasa wanakamilisha stand kubwa 2
 
Arusha mipango miji bado sana too much ufisadi
Hata hivyo Arusha ni mji mkubwa wenye eneo finyu angalau sasa hivi watakuwa wameongeza mipaka ya jiji na mbaya zaidi kule maeneo mengi yanamilikiwa na watu tangu enzi hizo na wanajua thamani ya ardhi hivyo hata serikali inapata wakati mgumu wa kupata maeneo ya shughuli za maendeleo zaidi ya kwenda pembezoni nako lazima walipe fidia ndefu
 
Hapoa Arusha wanaweza wakafanya mpango wakahamisha hayo makaburi nyuma ya stendi Ndogo kisha eneo lote mpaka huku stendi ndogo likiwa stendi kubwa ya mabasi.Yaani kuanzia hapo stadium kote kunakuwa ni STAND.Inawezekana kabisa
 
Hata wakiamisha bado pata kuwa padogo kwa jinsi miji inavyopanuka na wingi wa mabasi
Hapoa Arusha wanaweza wakafanya mpango wakahamisha hayo makaburi nyuma ya stendi Ndogo kisha eneo lote mpaka huku stendi ndogo likiwa stendi kubwa ya mabasi.Yaani kuanzia hapo stadium kote kunakuwa ni STAND.Inawezekana kabisa
 
Kweli kabisa
 
Arusha hakuna kituo kikuu chenye hadhi kwakweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…