Arusha: Wanne wadaiwa kufariki dunia baada ya Noah kusombwa na maji ikijaribu kuvuka barabara iliyofunikwa na maji

Arusha: Wanne wadaiwa kufariki dunia baada ya Noah kusombwa na maji ikijaribu kuvuka barabara iliyofunikwa na maji

Wapumzike kwa amani, majeruhi wapone haraka. Ila hizi ajali za magari kusombwa na maji huwa zinatokea lakini hatujifunzi. sijui kwa nini.
 
Sio Noah, si tulikua na land rover 110 mkuu hiyo gari ni nzito na ilipigwa kikumbo na maji mpk pembeni huko porini.
Itakua Noah
Ni kweli ndugu yangu Kwani ukifunga vioo tayari unakuwa umetengeneza meli (air balloon) na flooting balloon ni matairi ya Gari, hivyo lazima ubebwe na maji
 
Usalama wowote unaanzia na wewe mwenyewe

Ova
Leo nimekukubali kwenye argument zako, watu wanafikiri Serikali inaweza kulinda ujinga wa kila mtu. Haimaanishi kwamba hatari isipoweza kumkumba mmoja wengine watakuwa salama pia. Mungu awapumzishe kwa amani, roho za watu wasio na hatia zimedhulumiwa na dereva
 
Uzembe wa dereva. Hayo ndo madhara ya kujifunzia udereva mtaani kisha unahonga pesa kupata leseni.
 
Tuliwai kukutwa na same scenario kipindi cha el- ninyo.
Safarini Shinyanga.
Dom bahi daraja limevunjika mto maji km yale tukaona huko hatutoboi,ikabidi kukunja kwamtoro,
Dereva mbishi anawai kupeleka zawadi za sikukuu kwa wanae.
Tukakunja huko
Ilikua 110 londo, tumesota sana njiani mpk tukafika hapo kati kwa wasandawe.
Hapo tukakuta daraja nalo limesombwa ikabidi tutafanyaje.
Jamaa kadai tukae ndani gari iwe nzito tutapita.
Nikamwambia tujaze mawe iwe nzito upite nayo mi sikai humo ndani wala ndugu yangu.
Akagima.
Bahati nzuri wakatokea wanajeshi toka Singida na roli lao.
Walivyokuta pale hapapitiki.
Wakaingia shamba jaza miti pale mtoni mpk pakajaa wakasema nyie piteni kwanza si tutapita tu baada yenu.
Sijui ilikua mtego[emoji16],
Tukapita fresh na wao wakavuka wakapunga mkono haoo.
Tumefika mbele kidogo gari ikateleza ndani ya maji tena.
Hapo katikati ya pori ni milio ya simba na chui tu.
Ikabidi kujifungia tulale humo ndani.
Kesho kukakucha wakaja hao wasandawi(hadzabe)
Sukuma gari wapi wanadai hela tunawapa sukuma tena wapi wanadai hela iongezwa tunawapa.
Mpk usiku hola.
Hapo njaa balaa.
Katokea mwl mmoja ndio kasema twende home nikatengeneze ugali japo mle.
Tukaongozana toka pale porini mpk kwake.
Buku 5 kachinja jogoo na dona la kutosha.
Tulikua tumeenda na muhaya mmoja bonge kufika kule kashiba kagoma kurudi pale tumekwama[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
Ikabidi nigeuze mwenyewe maana nikifkiria wenzangu hawajala siku 2 na hasa bwa mdogo.
Aisee ningeliwa na wanyama siku hiyo.
Nilikutana nao wawili wakaniangalia tu.
Nikapita mwenyewe nikafika salama na ugali kuku.
Wale wengine wakafurahi sana kupata chochote.
Tulikua sita pia.
Kesho wasandawi wakaja rundo tukakomaa gari ikatoka.
Tukampitia yule mpuuzi pale kwa mwalimu amelala, tukaendelea na safari.
Tulifika salama.
Bonge akajisahau kabisa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Sasa huyu nae ki gari cha kilo 1500 ana kupitisha kwenye maji yanayo enda kwa speed ..afu kwenye iyo video ina onesha Ali enda kwenye kingo kabsa
Na hapo ndipo alipofeli, alifata kingo ya daraja kabisa. Kiufupi uzembe ndio chanzo cha ajali, hayo maji hayakuwa na kasi sana.
 
KILA siku hawasikii hawajifunzi kwamba usivuke bila kuona barabara hawasikii
 

Hii ni ile noah iliyozama ilikuwa na watu sita wawili wamepona, watatu wamepatikana wamefariki, mtoto mmoja hajaonekana sijui kapelekwa na maji hadi wapi

=======

Watu wanne wamepoteza Maisha na wengine wawili kunusurika kufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya NOAH T 499 DMY kusombwa na waji katika eneo la Malalula Kata ya King'ori wilayani Arumeru wakitokea Arusha kuelekea Kilimanjaro.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Emmanuela Kaganda amewaambia waandishi wa habari waliofika katika eneo hilo kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili na dakika arobaini asubuhi wakati dereva wa gari hilo Naimani Metili ambae ndio baba akiwa na abiria watano wakielekea katika mahafali ya mtoto wao Moshi.
Kama ndo dereva alikuwa baba hiyo ajali nliiona ni mshenzi flani tu hata hakuna haja ya kumpa pole mpumbavu kabisa. Ninapokuwa nimebeba familia yangu huwa sikubali kufanya uzembe wowote wa kijinga.
Kamwe nisingetumbukiza noah kwenye yale maji ni utahira wa sgr. Inamaana katekekteza familia yake
 
Kama ndo dereva alikuwa baba hiyo ajali nliiona ni mshenzi flani tu hata hakuna haja ya kumpa pole mpumbavu kabisa. Ninapokuwa nimebeba familia yangu huwa sikubali kufanya uzembe wowote wa kijinga.
Kamwe nisingetumbukiza noah kwenye yale maji ni utahira wa sgr. Inamaana katekekteza familia yake
Usiombe Sir Izrael akiwa anaitaka roho yako! ... anything can happen
 
Back
Top Bottom