Arusha: Yaliyojiri mapokezi ya Godbless Lema, Adai VICOBA ni umasikini, Mama lishe ni utumwa, Samia asitukanwe, Mbowe ampa kazi ya Katiba Mpya

Lema ameendeleza dharau Kwa watu maskini akisema vikoba ni umaskini.

Ikumbukwe Vicoba ni ubunifu wa wamama katika kujikwamua ila kama kawaida kwa kuwa amefanywa kipofu Ili aumbuke amewatukana tena wamama.

Watu maskini eleweni kwamba huyo sio mtu wenu na kama hamuamini endeleeni kimshabikia.

 

Watu Kufa au Kupata ulemavu Kwa sababu ya bodaboda ni Kutokana na ukosefu WA Elimu katika kazi hiyo na kutofuata sheria za udereva na usalama Barabarani, Na sio kuwa kazi hiyo ni Laana.

Ni jukumu la serikali kuandaa Mpango na utaratibu na kuupa nguvu kuhakikisha ili uwe bodaboda na uendeshe MTU lazima upate mafunzo na upewe Leseni,
Kisha iundwe sheria kuwa endapo utakuwa hauna Leseni na hauna cheti cha mafunzo utapewa adhabu ya kifungo cha muda Fulani.
Pia endapo utasababisha ajali na hauna Leseni wala mafunzo itahesabika kama umefanya mauaji ya kukusudia

Ni Sawa na MTU ajenge nyumba alafu Hana gani ya uhandisi majengo, nyumba ikianguka anapaswa kupewa adhabu Kali. Lakini huwezi sema ujenzi wa nyumba au ufundi Washi ni Laana.

Ndio maana Elimu ni muhimu.
Lakini sio Elimu ya kupotosha Watu kuwa kuna kazi ni Laana ilhali sio Laana.
Ndivyo wasomi wengi WA siku hizi mlivyo,
 
Umekosa uelewa. Suala siyo kiwango cha mapato ndicho kinachoifanya kazi fulani kuwa ya baraka au ya laana.

Kama kipato kikubwa ndiyo kipimo cha ubora wa kazi, basi ujambazi ungekuwa ni kazi bora sana kwa sababu jambazi, kwa mara moja anaweza kuiba milioni 50.

Panua mawazo yako ufanye argument sensibly.
 
Akili ndogo haiwezi kuelewa positively ilichoongea akili kubwa. Lema analenga kuwamsha msiridhike na maisha hayo bali mdai Serikali iwajengee mazingira ya kupata maisha bora zaidi.
 
Huyu jamaa hajui kuongea, ni wa kumpa taifa aongoze kweli? Ina maana aliokuwa anawatetea JPM wenye kipato cha jinsi hiyo wana laana? Hao hoa kwa kuwa ni wengi kidemokrasia ndio wanaokupa uongozi.
 
Sikudhani nawe unaweza kuwa na akili ndogo! Na kwa hakika akili ndogo haiwezi kuelewa positively ilichoongea akili kubwa. Lema analenga kuwamsha msiridhike na maisha hayo bali mdai Serikali iwajengee mazingira ya kupata maisha bora zaidi.
 
HAo hightablers wengi vi vikoba
 
Ajira ya bodaboda ni laana ya nchi yetu. Laana hutokea pale mtu au nchi in this case inapotawaliwa na viongozi wavivu, wezi na wazembe.
 

Oooh!
Wenzako tumesomea mambo ya Lugha. Tunapomsikiliza MTU akiongea au akiandika tunachujua ujumbe na dhamira juu ya alichokiongea. Wewe ambaye hujaelewa ujumbe wa Lema basi itakupasa urudi shule ufundishwe namna ya Kupata ujumbe pale MTU anapozungumza au mtu anapoandika.

Kwa kukurahisishia,
Lema kajikita zaidi kuuzungumzia umaskini na watu wenye kipato duni, katika mifano yake akachomekea Ubodaboda, Kwa hiyo bodaboda haikuwa Hoja kuu isipokuwa ni ndani wa kile alichokuwa anakieleza kwenye hoja Ya Hali duni ya watanzania,
Akatoa mfano mwingine wa Serikali kugawa Gesi, bado hujapata ujumbe wa kile anachokizungumza?
Akatoa mfano WA Vikoba, akichomekea mfano mdogo wa Mke wake aliyecheza kikoba Mwaka mzima lakini kwenye kuvunja kikoba akashangaa kuna laki na busy.
Bado huelewi mantiki ya hotuba ya Lema?

Ili mtu awe na Hali duni bila Shaka lazima awe anafanya kazi yenye kipato DUNI. Hata hivyo sio Kwa wote.
Bado hujaelewa?
Hujui ni Kwa nini wanasiasa wanapenda Kutumia mifano ya machinga, bodaboda, na waalimu?
Bado hujaelewa mantiki ya Lema.

Nilichoandika ndicho ambacho kulikuwa ujumbe Katika hotuba ya Lema

Kama hukusoma Lugha omba usaidiwe
 
Labda kama unafikiri ulisikia na kuona mwenyewe lakini tulimsikia na kumuona akisema hivyo, kuwa bodaboda ni kazi ya Laana.
Mimi naweza kuiita ni kazi ya laana kwa context moja tu, siyo kazi salama. Inaua vijana wetu wengi wakiwa kwenye umri mdogo sana, na kuwaacha wengi wakiwa na ulemavu.

Kuna wakati, kwenye kampuni yetu, tuliamua kuwapa mikopo isiyo na riba wafanyakazi wetu. Vijana wengi kwa kutumia pesa hiyo wakaamua kununua pikipiki. Ndani ya wiki 3 tukawapoteza vijana 4 na mzee 1 mwenda kwa miguu kwa ajali za pikipiki (aliyegongwa na kijana wetu). Iliumiza sana. Tukasimamisha mikopo. Mwanzoni tukafikiria tutoe conditions za mkopo, kuwa hakuna atakayeruhusiwa kutumia hela ya mkopo kununulia pikipiki. Lakini tukaona kuna shida, maana mkopaji akinunua pikipiki, bado inakuwa ni vigumu kutambua kama ametumia hela ya mkopo au hela yake ya mshahara au mapato mengine. Tukaamua tuzidishe mafunzo, yaliyohusisha wataalam mbalimbali. Tukafanikiwa, mpaka leo hatujashuhudia kifo chochote cha ajali ya pikipiki kwa wafanyakazi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…