Asafirisha wahamiaji 20 kwa V8 yenye bendera ya CCM

Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”

Chanzo: Ayo TV
Alikuwa anawarudishwa kwao baada CDF kuonya juu ya Wageni
 
Hili ni jema sana, ni vizuri sana ili viongozi wa vyombo vyote vya ulinzi wajitafakari ni wapi wanakosea!

Utekelezaji wa sheria kwa vyombo vyetu umekuwa sio mzuri, tunaangalia huyu ni nani. Sasa watu waovu mara nyingi hutumia udhaifu huo wa vyombo vyetu kufunya maovu.
Tatizo Uchawa.....yaani Chawa anafanya maovu makubwa na anaachwa sasa na wengine wanafata.

Ndio maana kila anayekuwa Chawa anatoboa. Unajiuliza anatoboaje?

Hii ni moja ya mbinu zao. Huenda ziko nyingi na mbaya zaidi ya hii.
 
Itakuwa amechomewa. Halafu kuwapeleka uhamiaji nako ni kuwapelekea tu ulaji.

Kwasababu hao kwanza hawana nia ya kuishi Tanzania.
Kweli mkuu ajali kazini
Hao vijana nawaona sana 🇬🇧 tena unaona kabisa ni fresh wanavyozubaa zubaa
Wakifanikiwa wao mwisho wa safari ni Ulaya

Ila wakishikwa wanarudishwa halafu wanaanza upya tena
Ni majaaliwa kufika ila wapo wanaofika huku na kuwasaidia wenzao waje pia
Jamaa sio kachomwa ila kabeba wengi sana lakini pia kwa waswahili linawezekana
 
Mtanzania Edward Erihard (31) Mkazi wa Dodoma anashikiliwa na Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kusafirisha kinyume na sheria Wahamiaji 20 Raia wa Ethiopia.

Akiongea Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara ACP Lucas Mwakatundu amesema tukio hilo limetokea March 23 2024 ambapo gari hilo limekamatwa katika kizuizi barabara ya Arusha Babati eneo la Minjingu likiwa na Wahamiaji ishirini Raia wa Ethiopia kwenye gari namba T.774 BDL Land Cruiser likiwa na bendera ya Chama cha Mapinduzi CCM.

“Gari hili V8 lilikuwa na Bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kwenye upekuzi tulipoona sura tofauti na Watanzania ilibidi tuweke gari pembeni na baadae kuwashusha tukakuta wapo Wahamiaji 20 kwenye gari V8 na wote uelekeo wao ni kusini mwa Afrika wakitokea usawa wa Arusha, Dereva wa gari hili ni Mkazi wa Dodoma tunamshikilia mpaka sasa na kesho tunatarajia kuwakabidhi Uhamiaji”

Chanzo: Ayo TV
Ukute na kadi za CCM wanazo hapo CCM ni janga la Taifa
 
Back
Top Bottom