Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Asante 2022, nilipata mil. 4.5 kimasihara

Jana imeshapita, furahia leo yako ya kesho muachie MUNGU kila kitu kipo kwenye mpangilio wake
 
Bank simu huwezi iba hela utailipa tu, fanya kama umekopeshwa usiitumie vibaya izalishe na ukipata hela yako mtafute alokutumia mrudishie.
 
Hiyo pesa utakuja kuilipa ,either wewe mwenyewe ,au watoto wako ....

Every action there is equal and opposite to the reaction ...
Kumbe newton's third law inaapply na kwenye hz ishu.. noma sana..
 
Kipindi nipo chuoo niliwahi kutumiwa pesa kimakosa laki 8 nikajifanya mjanja nikaitoa nikakusanya marafiki nikaenda nao kunywa pombe ile laini niliswitch off kwa wiki 3.ikapita miezi 8 kimya..baadae bibi alipata shida ya figo ilitakiwa afanyiwe dialysis kila mwezi so michango ya kifamilia ikatembea, bila kujua ili wala lile shangazi akanitumia mchango pesa ya matibabu laki 9.5 niitoe ili nimpatie mzee kumbe alituma katika ile line niliyotumiwa pesa kwa bahati mbaya..tigo hawajuchelewesha sms ikaingia hapo hapo
Ndugu mteja umekatwa sh laki 8 salio lako jipya ni laki na nusu niliishiwa pozi aisee.

Ili kuuawa soo nikaingia hasara nikatoa pesa yangu ya mkopo nikampatia mzee uku moyoni nina maumivu.
Juzi kati kuna mtu alikosea tena akanitumia pesa kimakosa mwenyewe nikamtafuta nikampigia cm nikamwambia umenitumia pesa kimakosa nakurudishia pesa yako..yaanini mie
 
Kama laini yako ya tigo na ya voda umesajilia kitambulisho kimoja na hiyo ya airtel usishangae wakikupigia hodi muda wowote.

By the way hii ni chai la sivyo usingekuwa na ujasiri wa kuileta hii mada jf, kwa zama hii za technolojia ya mawasiliano ila kama ni kweli basi ushajikamatisha
Hapana hiyo iliyotumiwa hela imesajiliwa kwa kitambulisho cha mtu mwingine na hata sijui yuko wapi kwa sasa
 
Mimi kuna mtu alikosea akatuma hela kwangu kwa roho nzuri tu nikampigia nimuulize katuma ya nini au kakosea akawa anakata simu mwishoe naona txt ikisema "uliniona maskini chukua kihela chako usinisumbue unaonekana una njaa sana hela ndogo inakutoa povu" aloo ilikua 240k nilifurahi sana nikamjibu nashukuru nikaitoa nikaendelea na harakati siku kama mbili akanipigia sikusave namba ndipo ananiambia samahani nilituma hela kimakosa na mm nikamwambia nishaitumia samahani sana. Nahisi alijiskia kufa huko alipo.

Fundisho ni kwamba alikua na dharau huenda alisaidiwa na mtu alafu kwenye kudaiwa akawa mgumu katoa na maneno ya dharau wakati aliponitafuta ili nirudishe muamala alikua anaomba kwa upole😂😂😂😂
 
Kuna siku utailipa...."what goes around comes around". Apandacho mtu..huvuna!...., utailipa kwa njia nyingine..kama sio utatapeliwa basi utatiwa hasara ambayo jumla yake itakaribiana na au itazidi hiyo yako...

Mimi nakumbuka nilikuwa na laini ya uwakala yenye jina tofauti na langu naifanyia kazi mwaka 2018, nikapita zangu pale BOA Bank tawi la Moro mjini...nikawaambia waniwekee laki na nusu wao wakaweka 1.5mil...na bahati mbaya laini niliiacha kihonda narudi nakuta muamala umezidi 😛 ...nikafanya muamala wangu wa laki na 50...hizo zingine nikaziacha....nikaiacha laini hewani ili wakidai waitoe, wakapiga simu usiku eti kuna hela wamenizidishia nikawaambia ndio nimeiona ila nipo mbali siwezi kuja....nikapita siku ya pili nikawapa laini wakaitoa..ila hawakunipa hata hela ya nauli jamani😎😎😎😎..kadada kalikokosea mwamala kakawa kananishukuru sana mimi nakaangalia tu..najisemea moyoni kwamba hunijui mimi ndio tabia yangu...sina amani ninapokuwa natumia mali ya mtu bila idhini yake😀😀😀

Ila wewemleta mada huna roho nzuri, unataka tukae mbali nawe sasa😀😀
 
Pole mkuu, ulijifunza kupitia njia ngumu...
Kipindi nipo chuoo niliwahi kutumiwa pesa kimakosa laki 8 nikajifanya mjanja nikaitoa nikakusanya marafiki nikaenda nao kunywa pombe ile laini niliswitch off kwa wiki 3.ikapita miezi 8 kimya..baadae bibi alipata shida ya figo ilitakiwa afanyiwe dialysis kila mwezi so michango ya kifamilia ikatembea, bila kujua ili wala lile shangazi akanitumia mchango pesa ya matibabu laki 9.5 niitoe ili nimpatie mzee kumbe alituma katika ile line niliyotumiwa pesa kwa bahati mbaya..tigo hawajuchelewesha sms ikaingia hapo hapo
Ndugu mteja umekatwa sh laki 8 salio lako jipya ni laki na nusu niliishiwa pozi aisee.
Ili kuuawa soo nikaingia hasara nikatoa pesa yangu ya mkopo nikampatia mzee uku moyoni nina maumivu.
Juzi kati kuna mtu alikosea tena akanitumia pesa kimakosa mwenyew..yaanini mie
 
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala ..... hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Haki ya mtu haipotei Kwa sababu mlipaji halali itafika kipindi utakua unajiuliza au labda Kwa sababu nilichukua pesa si yangu
 
H
Screenshot_20221229-154103.jpg
 
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala ..... hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Nikuulize kitu. Hiyo laini yako si imesajiliwa kwa jina lako. Kama imesajiliwa wafwa.
 
Newton's Third Law Of Motion
Hayo mafomula wakati mwengine huwa hayana maana yoyote, ninachoogopa ni kudhulumu nafsi, au mtu mnayefahamiana, the spirit or her work well on attacking others endapo kama kuna uovu.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Nikiwa nimepitia misukosuko mingi tangu Januari ya mwaka 2022 Nitaikumbuka zaidi siku ya Alhamis tar 29 majira ya saa saba za mchana, nikiwa nimekaa kijiweni na jamaa zangu huku nikiwa sina ramani ya kazi na sikuwa hata na uhakika wa mlo wa mchana kwa siku hiyo iliingia sms ya muamala kwenye simu yangu kuwa nimepokea kiasi cha ml 4.5 kutoka kwa wakala.

Hakika sikuamini nilichokiona, kwa haraka hiyo pesa nikaihamishia kwenye lain yangu ya tigo pesa ml 2 na laini ya voda nikahamishia ml 2, mbio hadi kwa wakala nikaitoa pesa kwenye lain zote na ile iliyokuwa imebaki kwenye namba niliyotumiwa ya airtel nayo nikaitoa.

Na laini iliyopokea muamala sijaiweka hewani hadi sasa na kabla sijaitoa hewani sikupigiwa na mtu kwamba ametuma hela kwangu kimakosa na wala mimi sikuwa na ahadi na mtu eti anitumie hela.

Kwahiyo ninashukuru sana aliyenitumia hiyo hela, kiukweli hata kama angenipigia na kuniambia eti kakosea muamala asingeambulia kitu. Mungu amlinde sana nilikuwa nina Magumu sana asante Mungu, na nitakukumbuka 2022.
Magumu umeshayamaliza? Na pesa imeshaisha na magumu bado yapo. Uaminifu hufungua Baraka zaidi.
Tusiendekeze sana njaa.
 
Sijui nikupongeze au nikulaumu but anyway maisha lazima yasonge
 
Back
Top Bottom