Asante Mbowe, umeongea hoja ambayo nilii-post hapa JF siku kadhaa zilizopita. Wewe umeiweka vizuri zaidi kuliko mimi

Hili fungu lote la maneno hapa ndiyo ulikusudia kuandika hiki nilichosoma hapa? Si mlikuwa hapa mnapinga JPM asiondoe ukomo wa miaka 10?

Au hayo hayamhusu Mbowe? Kila siku tunakejeli na kulaumu vitendo vya Museven na Kagame kwa kukalia kiti muda mrefu, leo nakuta umebariki.

Hebu tuwe serious na vipaumbele, vinginevyo tutaonekana hayawani.

Ova
 
Huyo J alikuwa kichaa huwezi ongozwa na kichaa.
 
Kwani mama yetu na jiwe walipochaguliwa uenyekiti wa ccm mnaloliita chama kubwa walikua na uzoefu gani?? Hoja ya uzoefu ni 🤮🤮🤮🤮
 
Museven ana experience ya Miaka mingapi, na kaifanyia nini Uganda ?
Kagame ana experience ya Miaka mingapi na Kiafanyia nini Rwanda ?
Kama CHADEMA wangekuwa wanaangalia experience wasingemleta Lisu kugombea nafasi ya Uraisi kwa sababu hakuwa na experience ya huo uraisi wenyewe.
Halafu bado CHADEMA wanasema waliibiwa kura 2020,kumbe walileta watu wasio na experience
 
Mbowe Hakuzaliwa Na Uongozi Waliomtangulia Wangepima Kwa Kipimo Hicho Leo Hasingefika Hiyo Miaka Anayojisifu Nayo Kama Ana Mawazo Hayo Basi Hana Tofauti Na Madikteta Wenzake Wote Waliopo Na Walio Pita Mi Namuona Mbowe Kwenye La Museveni.
 
Kwa hoja yako hii unakubaliana na sisi waCCM tunaoamini vyama vya upinzani havipaswi kuongoza nchi yetu kwasababu havina uzoefu au sio.

Kwa uelewa wako unadhan Mbowe alizaliwa tu akawa mwenyekiti wa chama Taifa au aliaminiwa na ndio akawa hapa alipo leo.

Umeleta hoja ya hovyo sana ila umeiandika kwa kujichekesha ili uonekane umeandika jambo la maana.Mbowe na wote mnaomuunga mkono ni maadui wa demokrasia.

Sijawahi kumuona Mbowe kama mpinzani tangu nimeanza kuzijua siasa za Taifa hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…