Asante Rais Samia kwa Kumtumbua Maharage wa TANESCO. Naomba apelekwe Mahakamani

umepatia sana mkuu,
huyo ndie.
ndio tunakamilisha vetting hapa japo kuna mabishano kidogo kuhusu sifa stahiki
Anajua mfumo wa serikali unavyofanya kazi?Ana uelewa wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii?Ana Background ya kuelewa mambo ya Uchumi na Biashara na Diplomasia.
Hatutafuti Ofisa habari wa serikali ila tunatafuta Msemaji Mkuu wa serikali!
 
Figganigga kila mara nakwambia humu... CCM hawana utaratib huo wa kupelekana mahakamani!! Na ikitokea ujue issue imekua nzito inabid mtu atolewe kafara, utaratib wa CCM ni huu... Ukifurunda au kuitia hasara serikali ni unatenguliwa na kuhamishiwa kwingine kweny ulaji!! Huu ndio utaratib wa CCM ✔️
 
Why not Kelvin Twisa!
Twisa ni mzuri sana kwenye marketing, nafasi ya marketing ingemfaa hapo ila kwa bahati mbaya huwezi market kitu ambacho hakipo. TTCL ipo kwenye phase ya kuweka/kuimarisha miundombinu, inahitaji kiongozi mwenye ujuzi eneo hilo
 
Hajamtumbuwa kambadilishia kitengo.kimtumbuwa ni kutenguwa uteuzi jumla.
 
Ametumbuliwa au amebadilishiwa kituo cha kazi?
 
Usikubali kupumbazwa mkuu. Maharage ni kama Blandina Nyoni tu. Hao wapo kazini muda wote, kazi zao si kufanya chochote bali kuandi reports na kushauri wakuu wao.
Blandina Nyoni anaandika ripoti gani na anampelekea nani? Wacha kutukumbusha mboga iliyochacha hapa?
 
Kumtoa Ulanga TTCL ni kosa la kiufundi...
 
Hapa ndipo ninapowapenda wabongo. Ukitaka kuwafurahisha wabongo basi wewe badilisha tu watendaji, yaani tumbua, halafu tunakuja na kauli mpya ya kurekebisha makosa kama miezi 6 hivi, baada ya hapo tunakuja na mkakati mpya wa maboresho ya miundombinu na mitambo ya umeme itakayochukuwa mwaka mmoja na nusu, then kipindi cha majaribio kama miezi 6 hivi, hapa kwakuwa wananchi watakuwa wameshaanza kulalamika tena kitakachofanyika NI KUBADILI UONGOZI WA SHIRIKA NA WATENDAJI (KUTUMBUA), KISHA TUNAKUJA NA TAMKO JIPYA NA MKAKATI WA UBORESHAJI.

NISEME TU KUWA TABU IPO PALEPALE
 
Hizo ni dua za mwewe mkuu. Ametumbuliwa TANESCO amepelekwa TTCL akale bata zaidi. Nchi ngumu sana hii asisee!
 
Anajua mfumo wa serikali unavyofanya kazi?Ana uelewa wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii?Ana Background ya kuelewa mambo ya Uchumi na Biashara na Diplomasia.
Hatutafuti Ofisa habari wa serikali ila tunatafuta Msemaji Mkuu wa serikali!
uto tuvitu tudogotudogo sana, kwahiyo ww ulivyoajiriwa apo tanesco ulianza kazi tu bila orientation right?

au unadhani pia hao wanaoteuliwa kuwa mabalozi sehemu mbalimbali duniani wanaenda tu?

Hakuna kitu mtu anaweza shindwa, mwanzoni ataona ngumu, chungu na inauma, akizoea inakua kawaida na tamu.
 
Watanzania tunakuwa wajinga miaka yote kwa nini? Kabla ya maharage Umeme ulikuwa haukati? Umeme umekuwa shida tangu uhuru.Hata baada ya kuondoka maharage Umeme wa mgao utaendelea kama kawaida.Kikubwa vitafutwe chanzo vingine vya Umeme kama vile sola na Umeme wa upepo.
 
Mambo yameharibika ndio akili zinawarudia. Tulishasahau mgao wa umeme alafu mnaturudisha huko kihuni tu. Nimefurahi mama kupeleka Meja Jenerali kuwa mwenyekiti bodi ya Tanesco.
Ulisahau mgao wa Umeme my foot au umezaliwa mwaka huu dogo
 
Unamtoa Eng. Peter Ulanga TTCL unampeleka maharage???!!! What a joke??
Sasa Perer Ulanga ana miaka 2 pale sijui kwani umeona TTCL hata ikibdilika? Ni kama mgonjwa aliye kwenye coma
 
Hii nchii shida ni kujuana,pale angempa Kelvin Twisa!
Huyu jamaa amefanya mambo makubwa kwenye Telecommunications sector upande wa Private sector!
Kama wewe ndiye Kevin Twissa nakuhakikishia kuwa huna kitu unachojua. Hata vyeti vya chuo chochote huko Marekani huna zaidi ya ujanja ujanja wa kupozi kwenye TV.
 
Sasa Perer Ulanga ana miaka 2 pale sijui kwani umeona TTCL hata ikibdilika? Ni kama mgonjwa aliye kwenye coma
Alijipanga upande wa fixed network, katizame mafanikio yake kwenye mradi wa FTTH, muda ni jaji mzuri tutampima maharage pia. Ki uhalisia project ya FTTH ndio mkombozi wa TTCL ila kama maharage atakuja na habari za mobile atafeli vibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…