Asante Rais Samia kwa kuruhusu usawa kwenye elimu

Asante Rais Samia kwa kuruhusu usawa kwenye elimu

Bado shule za msingi na vyuo vya kati hawajaruhusiwa kuvaa mkuu. Hawa ndio nawapigania waruhusiwe kuvaa haya mavazi ili kuleta usawa na kuwaondolea unyonge na kujihisi kutengwa.
Katika uislamu, mwanamme akijifinika magoti na kitovu, tayari ameshavyaa nguo kisawa sawa, wanafunzi wa shule za msingi, wazazi wawashonee watoto wa kiume, suruali inayofinika magoti, hata kama ni fupi, na shati linalofinika juu.
 
Wakishakuwa sawa hii inatusaidia nini kwenye elimu?
Italeta usawa wa kiraia na kuondoa dhana na mawazo ya kutengwa, jambo ambalo huwaathiri watoto kisaikolojia na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo.
 
Katika uislamu, mwanamme akijifinika magoti na kitovu, tayari ameshavyaa nguo kisawa sawa, wanafunzi wa shule za msingi, wazazi wawashonee watoto wa kiume, suruali inayofinika magoti, hata kama ni fupi, na shati linalofinika juu.
Walau hapo itakuwa sawa mkuu. Unajua hawa watoto wa shule za msingi wanapoona wenzao wamepewa haki na wao kunyimwa hujisikia wanyonge sana kisaikolojia na hili hupelekea wao kufanya vibaya kimasomo.
 
ni kweli, na hiyo shule ichunguzwe, watoto wa primary wa kike na wa kiume analelewa na Matron si Patron sababu anakuwa bado ni wadogo.

Sasa hilo baba la kiume lilikuwa linawaleaje watoto under 13, na inawezekana hata mke halikuwa naye.
Sule gani hii mkuu? Haya ndiyo mambo ambayo hayapendezi kabisa kufanywa kwa watoto wetu wadogo wasiokuwa na hatia na wasioweza kujitetea. Inauma sana.
 
bado sijaona hoja hapo, yaani mwanafunzi wa primary ama secondary aende na Kanzu lake shuleni ? kisa tu usawa wa ki-imani ...hili jambo unaliona lina tija kweli.?
Mkuu hapa hatuongelei usawa wa kiimani bali tunaongelea usawa wa kielimu. Ndio maana hata baadhi wameruhusiwa kuvaa kofia, hijabu na kofia. Hoja nzima iko based on equality, not spirituality. Nadhani utakuwa umenielewa mkuu.
 
Italeta usawa wa kiraia na kuondoa dhana na mawazo ya kutengwa, jambo ambalo huwaathiri watoto kisaikolojia na kushindwa kufanya vizuri kwenye masomo.
Kuna tafiti yoyote imewahi fanyika ikaonesha watoto wanashindwa kufanya vizuri kwenye masomo kwa sababu hawavai kanzu???

Tukirudi kwenye jamii haswa upande wa dini ya kiisalamu, nimefanikiwa kuishi nao kwa wingi kiasi chake na hili vazi mara nyingi watoto wamekuwa wakilivaa wanapoenda madrasa pekeake. Wakirejea wanavaa mavazi ya kawaida.

Sasa huko nyumbani wanakovaa mavazi ya kawaida bila kushurtishwa na mtu hakuna madhara sindio? Huko hawawezi kuwa na dhana ya kutengwa sindio??

Sasa kama nyumbani hawavai kanzu na hawahisi kutengwa na shule iwe hivyohivyo.
 
anzisha shule yako uruhusu kila denti anende na guo lake - ila kwa Tanzania Shule zetu za umma sahau.
Mbona wanavaa hijabu, vilemba na kofia mkuu? Au hujasoma vizuri uzi wangu?
 
Vilevile na misamiati hii kutoka kwenye matumizi ya lugha Serikalini....Kistaha-arabu na Ki-Ngwana.

Pole Raisi kwa kufungulia masikio kwa watakao kumaliza kisiasa. Watakao kudhoofisha. Tunaona mbinu zao.

...kwenye mada, hizi haki za usawa ziwe haki za kweli na za Utamaduni wa Mwafrika.

Naona...
Kuna nguvu kubwa zinatumika kuona kuna utengano Tanzania.

Jambo hili linatengeneza Uhasama. Ndio tunavyo valiwa hivi?
 
Kuna tafiti yoyote imewahi fanyika ikaonesha watoto wanashindwa kufanya vizuri kwenye masomo kwa sababu hawavai kanzu???

Tukirudi kwenye jamii haswa upande wa dini ya kiisalamu, nimefanikiwa kuishi nao kwa wingi kiasi chake na hili vazi mara nyingi watoto wamekuwa wakilivaa wanapoenda madrasa pekeake. Wakirejea wanavaa mavazi ya kawaida.

Sasa huko nyumbani wanakovaa mavazi ya kawaida bila kushurtishwa na mtu hakuna madhara sindio? Huko hawawezi kuwa na dhana ya kutengwa sindio??

Sasa kama nyumbani hawavai kanzu na hawahisi kutengwa na shule iwe hivyohivyo.
Mkuu, hata kama utafiti haujafanyika kuna viashiria vya wazi kwenye matokeo ya mitihani yanayoonyesha wasichana kuwa na ufaulu mzuri ukilinganisha na wavulana.

Shuleni na vyuoni wanafunzi wanaruhusiwa kuvaa kofia, hijabu na vilemba (kwa masista wa kanisa katoliki). Kwanini vijana wa kiume wa kiislamu wao watengwe?

Nyumnani hakuhitaji unifomu; kila mtu anavaa ajisikiavyo pasipo kushurutishwa na mtu yeyote. Shuleni kuna shuruti pale unapokuwa hujavaa uniform iliyoruhusiwa kwa mujibu wa sera ya elimu. Ndio maana napigania baragashia, kanzu na lubega zivaliwe shuleni bila kuwabagua wanafunzi kwa namna yoyote ile.
 
Mleta mada nina kuunga mkononkwa kutoa pongezi kwa mh.Rais kuruhusu kofia kwa wanafunzi wa imani ya Ras Tafar.
Lakini sikubaliani na wewe kwa ombi lako la Kanzu na kofta kwa wanafunzi wa kiislam wakiume kwasababu sio WAJIBU(lazima) kuvaa kanzu na kofia.
Inamaana anaweza asivae kanzu na kofia na bado hata ondokewa na UISLAM WAKE.
 
Unahisi ni kwanini,

Kuna uniform za jeshi, polisi, daktari, rubani n.k. na nilazima mtu husika katika vipengere tajwa avae?

Sababu inayopelekea mtoto wa kiume kutofanya vizuri ni huangalizi hafifu na sio kanzu.

Jamii inamuona mtoto wa kiume kama mtu anayeweza kujiongoza mwenyewe na nguvu kubwa ya uangalizi imewekwa kwa mtoto wa kike na hapo ndipo tatizo lilipoanzia.

Hizi kanzu hazina maajabu ya kuleta utofauti kwenye elimu.

Tuzipime basi hizi kanzu kwa ngazi ya dini,
Waislamu waliowengi hawavai kanzu ila tu kukiwa na event maalamu, kama hiki kitu ni muhimu kiasi hiki mbona utekelezaji wake ngazi ya jamii uko chini na sasa mnataka zivaliwe shuleni?
 
Mleta mada nina kuunga mkononkwa kutoa pongezi kwa mh.Rais kuruhusu kofia kwa wanafunzi wa imani ya Ras Tafar.
Lakini sikubaliani na wewe kwa ombi lako la Kanzu na kofta kwa wanafunzi wa kiislam wakiume kwasababu sio WAJIBU(lazima) kuvaa kanzu na kofia.
Inamaana anaweza asivae kanzu na kofia na bado hata ondokewa na UISLAM WAKE.
Mkuu wangu hii hoja msingi wake ni USAWA sio IMANI. Ndio maana baadhi yao wanaruhusiwa kuvaa hijabu, kofia na vilemba na haijawahi kuleta shida yoyote katika imani. Ninachojaribu kusema ni kuhakikisha kuna USAWA kwa watu wote bila wengine kujihisi wanyonge au kupendelewa. Nadhani utakuwa umenielewa sasa.
 
Back
Top Bottom