Asante Rais Samia kwa kuruhusu usawa kwenye elimu

Asante Rais Samia kwa kuruhusu usawa kwenye elimu

Unahisi ni kwanini,

Kuna uniform za jeshi, polisi, daktari, rubani n.k. na nilazima mtu husika katika vipengere tajwa avae?
Ni kwa sababu weweze kutambulika kirahisi hasa kwa mtu anayehitaji huduma yao. Wewe unahisi ni kwanini baadhi ya wanafunzi wanaruhusiwa kuvaa hijabu, kofia na vilemba huku wengine wakinyimwa kuvaa kanzu na vibaragashia? Kuna shida gani?
 
Watakuwa sawa na wenzao waliovaa hijabu, vilemba na kofia.
Mkuu huko sasa umefika mbali tofautisha kati ya mavazi yanayofunika kichwa na yanayofunika mwili mzima

Hizo kofia vilemba sijui hijabu hizo zinafunika kichwa tu na si mwili mzima kwa maana kwamba lengo ni kutozuia uniform ya shule kuonekana

Ungesema vibaragashia tu ningekuelewa ila si kanzu inayofunika mwili mzima maana uniform itakuwa haionekani na huo wala si usawa
 
Mkuu wakivaa kanzu fupi nyeupe zinazofanana na mashati ya shule kuna shida gani hapo?
 
Ni kwa sababu weweze kutambulika kirahisi hasa kwa mtu anayehitaji huduma yao. Wewe unahisi ni kwanini baadhi ya wanafunzi wanaruhusiwa kuvaa hijabu, kofia na vilemba huku wengine wakinyimwa kuvaa kanzu na vibaragashia? Kuna shida gani?
Wote wakinyimwa iyo haki ya kuvaa vilemba na hijabu bado haina madhara yoyote.

Huku mtaani ambako mko huru kuvaa hijabu na Kanzu hakuna impact yoyote ya haya mavazi, hayapunguzi wala kuongeza chochote zaidi ya watu kuvaa tu kama sehemu ya matakwa ya dini tena walio wengi huvaa kwa event maalumu.
 
Mkuu wakivaa kanzu fupi nyeupe zinazofanana na mashati ya shule kuna shida gani hapo?
Bado watakuwa tofauti sababu kanzu ni tofauti na mashati ya shule

Wakiruhusu wanaume wavae kanzu na wanawake nao watataka wavae majuba yanayofunika mwili mzima

Kama lengo ni kuwa sawa na wenzao wanaovaa kofia vilemba na hijab ambavo vinafunika kichwa tu na si mwili mzima basi vibaragashia vinawatosha
 
Wote wakinyimwa iyo haki ya kuvaa vilemba na hijabu bado haina madhara yoyote.

Huku mtaani ambako mko huru kuvaa hijabu na Kanzu hakuna impact yoyote ya haya mavazi, hayapunguzi wala kuongeza chochote zaidi ya watu kuvaa tu kama sehemu ya matakwa ya dini tena walio wengi huvaa kwa event maalumu.
Lakini wakiruhusiwa kuvaa shuleni na vyuoni italeta USAWA na kuwafanya wanafunzi kujisikia vizuri hata kufaulu kwenye masomo yao, na hili ni jambo zuri halina madhara yoyote.
 
Bado watakuwa tofauti sababu kanzu ni tofauti na mashati ya shule

Wakiruhusu wanaume wavae kanzu na wanawake nao watataka wavae majuba yanayofunika mwili mzima

Kama lengo ni kuwa sawa na wenzao wanaovaa kofia vilemba na hijab ambavo vinafunika kichwa tu na si mwili mzima basi vibaragashia vinawatosha
Waki design kanzu fupi na kuvaa suruali kama vile shule za kiislamu wanavyovaa sidhani kama kutakuwa na shida yoyote mkuu.
 
Lakini wakiruhusiwa kuvaa shuleni na vyuoni italeta USAWA na kuwafanya wanafunzi kujisikia vizuri hata kufaulu kwenye masomo yao, na hili ni jambo zuri halina madhara yoyote.
Hakuna usawa wowote unaoenda kuleta unafuu wowote kwenye elimu kwa kuvaa kanzu shuleni zaidi ya kuleta matabaka ya kidini.
 
Hakuna usawa wowote unaoenda kuleta unafuu wowote kwenye elimu kwa kuvaa kanzu shuleni zaidi ya kuleta matabaka ya kidini.
Mbona wanavaa vilemba, kofia na vilemba lakini hakujawahi kutokea matabaka yoyote mkuu? Hayo matabaka yatatoka wapi sasa?
 
Uliyeandika sio muislam. Kanzu na balaghashia sio dini ya kiislam.
Mkuu mimi hapa siongelei IMANI bali naongelea USAWA, hasa katika elimu. Umenipata?
 
Mbona wanavaa vilemba, kofia na vilemba lakini hakujawahi kutokea matabaka yoyote mkuu? Hayo matabaka yatatoka wapi sasa?
Matabaka yapo tayari, pata tu muda wa kufatilia huko mashuleni na vyuoni utajifunza kitu.

Kila tabaka linataka kujitofautisha na lingine kwa misingi ya imani.
 
Matabaka yapo tayari, pata tu muda wa kufatilia huko mashuleni na vyuoni utajifunza kitu.

Kila tabaka linataka kujitofautisha na lingine kwa misingi ya imani.
Hayo huenda kweli yapo lakini uzuri ni kwamba Rais Samia ameonesha njia ya kuleta USAWA ili kujaribu kuyaondoa hayo matabaka na kuujenga taifa lililo sawa na lenye misingi ya kupendana na kuheshimiana tofauti na Mendazake ambaye alikuwa analigawanya taifa hili kila kukicha.
 
Sahihi...lakini udini usizidi sana kwenye suala LA elimu

Pamoja na jitihada nyingi, ikiwa ni pamoja na Kutumia Kiswahili ili kupunguza makali ya Ukimbari asilia, na kudumisha Muungano wa mataifa mbalimbali hapa Tanzania, kuna wachache wanatumia Ukarimu na Utu wa Mwafrika /Mtanzania kuona tunasambaratika kwa makundi-Kidini, Kikabila, Kitamaduni n.k na hata kwa rangi ya Ngozi, ni karaha sana.

Naona jitihada zinawekwa kwa makusudi.
Tutakosa heshima tukiyaachia....

Katika nchi zinazoheshimiwa na zenye maendeleo ni zile Nchi ambazo zilikataa katu katu kutokuingiliwa kwenye Jadi, Tamaduni, na Maadili yao.

Hakuna mtu au Nchi anaeweza kukuheshimu pale unapokuwa una sua sua , yaani unakosa uadilifu. Hakuna. Awe Babu Bibi Baba Mama mtoto au hata Mbwa. Huwezi pata heshima.

Tusiwe chaka la majaribio ya utafiti wa jamii. Tuwakatae wanaotaka tutengane kwa sababu za kishetani.
 
Mkuu mimi hapa siongelei IMANI bali naongelea USAWA, hasa katika elimu. Umenipata?
Mtumishi!?
Acha kuongelea kitu usichokijua na kukiamini.

Turudi kule kwenye betting na machimbo ya kina dada poa. Huku hapakufai.😂😂
 
Habari wakuu! Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwapotezea muda. Leo nimeona waraka mzuri sana kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (MoEVT) unaoruhusu wanafunzi wenye imani ya Rastafali kuruhusiwa kuvaa kofia kufunika nywele zao kwani hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu tangu serikali zilizotangulia. Hili limewezekana tu katika awamu hii ya sita inayoongozwa na Jemedali, Chifu Hangaya, Rais Samia Suluhu Hassan. Nakupongeza sana kwa kujali imani za watu unaowaongoza. Mama anaupiga mwingi jamani! Wenye roho mbaya mkajinyonge au msage sumu mnywe, tutakuatana mbinguni.

Lakini pamoja na pongezi hizi, nakuomba mama yangu Rais Samia uwaruhusu vijana wa kiislamu nao waweze kuvaa kanzu na baragashia ili kuondoa dhana ya upendeleo. Sio kwamba waislamu hatuna shukrani, la hasha! Tunakupongeza sana kwa kuruhusu mabinti wa kiislamu kuvaa hijabu wawapo mashuleni na vyuoni lakini tunasikitika watoto wa kiume hawaruhusiwi kuvaa kanzu na baragashia kwanini? Tatizo liko wapi?

Najua huenda wasaidizi wako wa chini ndio wanakushika miguu lakini nafahamu una uwezo wa kutoa amri leo na kesho Waziri wa Elimu akaandika waraka wa kuruhusu jambo hili kutekelezwa. Tunajua hushindwi kitu mama yetu kwani huwa unahakikisha watu wa imani zote wanatimiziwa matakwa yao bila kuathiri maslahi ya watanzania wengine. Kwa kuanzia nawaomba BAKWATA wapigie chapuo jambo ili liweze kufanikiwa haraka kuliko wanavyokaa kimya kana kwamba hawaoni tatizo.

Nina hakika baada ya waislamu kutimiziwa matakwa yao pia utatazama makundi mengine ya kijamii kama vile wamasai ili nao waruhusiwe kuvaa lubega na katambuga shuleni na vyuoni. Pamoja na kuwa utakuwa umewatendea haki wapiga kura wakao bila ubaguzi wowote, nina imani uvaaji wa vazi hili la kitamaduni utachangia kwa kiasi kikubwa kutangaza utalii wa kiutamadani (cultural tourism) kwani sekta ya utalii huliingizia taifa hili fedha nyingi za kigeni ambazo hutumika kujenga miundombinu ya umma kama vile SGR, Bwawa la Umeme la Nyerere, barabara na miradi mingi yenye manufaa kwa wananchi wote.

Nawasilisha.
Hijabu ni kwa ajili ya stara ya mwanamke wa kiislamu dhidi ya nywele zake.

Kanzu ni stara?
 
Mtumishi!?
Acha kuongelea kitu usichokijua na kukiamini.

Turudi kule kwenye betting na machimbo ya kina dada poa. Huku hapakufai.
Sawa twenzetu mkuu 😀 😀 😀 😀
 
Hayo huenda kweli yapo lakini uzuri ni kwamba Rais Samia ameonesha njia ya kuleta USAWA ili kujaribu kuyaondoa hayo matabaka na kuujenga taifa lililo sawa na lenye misingi ya kupendana na kuheshimiana tofauti na Mendazake ambaye alikuwa analigawanya taifa hili kila kukicha.
Hakuna usawa alioweka Hapo zaidi ya kufungua mianya kwa matabaka mengine.

Na Bahati mbaya au Nzuri haya matabaka matokeo yake tunayaona kila siku huko mashuleni na vyuoni kwa baadhi ya matabaka kujiwekea utaratibu wa kutoshirikiana na wengine kwa sababu si watu wa tabaka Lao.

Kaongeza tatizo,
 
Hijabu ni kwa ajili ya stara ya mwanamke wa kiislamu dhidi ya nywele zake.

Kanzu ni stara?
Kanzu hufunika hadi magoti ya mwanaume (stara) au kama itakuwa designed kanzu fupi na itakayovalliwa na suruali fupi inayofunika magoti bado ni sawa tu hakuna shida mkuu.
 
Hakuna usawa alioweka Hapo zaidi ya kufungua mianya kwa matabaka mengine.

Na Bahati mbaya au Nzuri haya matabaka matokeo yake tunayaona kila siku huko mashuleni na vyuoni kwa baadhi ya matabaka kujiwekea utaratibu wa kutoshirikiana na wengine kwa sababu si watu wa tabaka Lao.

Kaongeza tatizo,
Mbona uvaaji wa hijabu, vilemba na kofia (kwa rastafali) hakujawahi kuleta matabaka? Hayo matabaka atayaleta nani sasa?
 
Back
Top Bottom