Asasi za Kiraia kuishtaki Tanzania kwa kutaka kujitoa kwenye itifaki ya Mahakama ya haki za binadamu Afrika

Hivi hawa watu wanaelewa maana ya sovereign state? Wanaelewa maana ya nchi kuwa huru? Nchi kujiunga na hiyo Mahakama ni hiari na kujitoa ni hiari pia na ndo maana kuna hiyo option ya kujitoa, sasa nchi imeamua kujitoa unasema unakwenda kushitaki, hivi mna akili timamu kweli?

Mimi ni Mwanachama wa Club, nimejiunga kwa hiari na naweza kujitoa kwa hiari sasa iweje unishitak kwa kujitoa? Kama una deni na mimi nitalipa lkn huwezi kunizuia kujitoa, ...
 
You have gotten personal!
 
Acha uongo Afrika ina nchi 54 kwa hiyo unataka kuwadanganya watanzania kuwa zimebaki nchi 14 tu? Watanzania sio wajinga kuwa unaweza kuwadanganya.
nchi 9 tu ambazo zimethibitisha. Anachokisema ni kweli


Members

Members of the African Court on Human and Peoples' Rights.
Burgundy - fully recognize the competence of the court
Pink - other states that have ratified the protocol
As of January 2019, nine state parties to the protocol have made a declaration recognizing the competence of the Court to receive cases from non-government organizations (NGOs) and individuals. The nine states are Benin, Burkina Faso, Côte d'Ivoire, Ghana, Mali, Malawi, Rwanda, Tanzania, the Gambia and Tunisia.[2] Altogether, 30 states have ratified the protocol: Algeria, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Chad, Côte d'Ivoire, Comoros, Republic of the Congo, Gabon, Gambia, Ghana, Kenya, Libya, Lesotho, Mali, Malawi, Mozambique, Mauritania, Mauritius, Nigeria, Niger, Rwanda, Sahrawi Arab Democratic Republic, South Africa, Senega
 
Hahaha ni hiyari ya watawala au wananchi?
Hoja hiyo imepelekwa bungeni kwa wawakilishi wetu, wakaafiki tujitoe Tanzania au ni mtawala mmoja kaamua kujitoa kwa Tanzania?!
Hii ni kulinda maslahi ya wananchi au ya watawala?!
 
Hahaha ni hiyari ya watawala au wananchi?
Hoja hiyo imepelekwa bungeni kwa wawakilishi wetu, wakaafiki tujitoe Tanzania au ni mtawala mmoja kaamua kujitoa kwa Tanzania?!
Hii ni kulinda maslahi ya wananchi au ya watawala?!


Siyo lazima kila maamuzi ya Serikali yapelekwe Bungeni, na ndio maana tunafanya Uchaguzi na tunayemchagua tunamuamini atuwakilishe.
 
Siyo lazima kila maamuzi ya Serikali yapelekwe Bungeni, na ndio maana tunafanya Uchaguzi na tunayemchagua tunamuamini atuwakilishe.
Nilidhani unaongelea taifa kumbe kikundi cha watu?!
Kabudi hajachaguliwa bali aliteuliwa kumsaidia mtu mmoja kazi, alipaswa amshauri aliyechaguliwa kisha yeye ndiye aamue.
Ukimuajiri personal secretary, sidhani kama anaweza kukufanyia maamuzi kwenye kampuni yako. Anaweza kuchapa barua lakini signatory ni wewe uliye muajiri, siyo yeye.
 
Hahaha una pinduka piduka, ulikuwa hutaki alaumiwe Kabudi sasa umeanza ligi nyingine.
 
Kuna nchi zaidi ya 40 Afrika zimejitoa katika hiyo mahakama sio Tanzania pekee!

Zitaje usilete uongo wako hapa. Mahakama yenyewe haijawahi kuwa rectified na nchi 40 hizo zilizojitoa zilijitoaje?
 


Kabudi anaingiaje hapa?
 
Acha uongo Afrika ina nchi 54 kwa hiyo unataka kuwadanganya watanzania kuwa zimebaki nchi 14 tu? Watanzania sio wajinga kuwa unaweza kuwadanganya.

Ni kweli, si Watanzania wote ni wajinga. Jamaa hajui kuwa msingi wa African Charter ni uanachama wa African Union. Na hapa ndipo Tanzania itashindwa katika ombi lake, haiwezi kujitoa katika msingi mkuu wa kuanzishwa kwa African Charter on Human and People's Rights huku akiwa mwanachama wa AU. Moja ya haki zenyewe ni kutoa kwa haki za kisheria bila kuangalia rangi, utaifa, dini, kabila, jinsia nk. Ninadhani ombi lao hili litawafungua akili kujua hawawezi tu wakata wao wawe washitaki, hakimu, na watoa adhabu. Moja ya sababu kubwa ya vita Afrika ni kuwepo kwa vyombo visivyoheshimu haki za binadamu. Kutokuwepo na access kwa mahakama hii kutaikosesha jumuia ya kimataifa kujishughulisha na mambo ya ndani ya Tanzania na wakati huo huo haki hazitolewi ndani ya Tanzania. Lawlessness huanza hivi na kisha kufikia spillover.
 
Mfano ni faida zipi unapata ukijitoa kwenye mahakama hiyo??? Acheni kutaka kuwaburuza wtz kama mbuzi!!! Ni bunge lipi ambalo limekaa na kuridhia??? Wananchi tumewatuma huduma bora na sio kujitoa taasisi za kimataifa ili mtunyonge gizani na hivi mnatuitaga wanyonge
 
Sasa Nchi inakuwaje Nchi bila ya Wananchi? Hao unaotaka kuwaona ni Nchi ni watumishi wetu hivyo hawana mamlaka yoyote ya kuamua mustakabal wetu bila ya ridhaa yetu.
 
Sasa Nchi inakuwaje Nchi bila ya Wananchi? Hao unaotaka kuwaona ni Nchi ni watumishi wetu hivyo hawana mamlaka yoyote ya kuamua mustakabal wetu bila ya ridhaa yetu.


Unaelewa maana ya Uchaguzi wa Viongozi? Isitoshe kama ni hivyo kwa nini nchi nzima hamuhudhurii Mkutano wa UN New York badala yake wanakwenda wachache?
 
Hata ninyi (THRDC) na (LHRC) wenywe kaeni chonjo mtakuja kufutwa mbele ya safari. Na ndicho kilichoua EAC ya zamani na hii mpya haifiki mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…