Asee Wazee wenzangu tunaofikisha umri wa miaka 40+ mwaka huu na hatuna any direction njooni hapa tu jadiliane

Ila hili taifa, kizazi cha kuanzai miaka ya 1979 hadi maika ya 2000 mwanzoni ni kizazi ambacho kinaongoza kwa kupotezewa direction na Serikali ya CCM.

Maana asilimia kubwa hawana kazi au ajira rasmi wanaishi kwa madili ya mjini,michongo ya kupeana na misaada so hii ina maanisha ni kizazi ambacho hakitakuwa na mafao ya uzeeni ya kiinua mgongo.

Asilimia kubwa hawajaoa na kuolewa wanaishi mahusiano ya kusindikizana na kuachiana njiani na kila wakitoka uhusiano m'moja kwenda mwingine partner mpya anakuwa hasara kuliko aliyetangulia so no future in relationships ni kupoteza muda kama kujifurahisha na kuwa katika risks ya kuambukizana magonjwa na kutoa mimba hovyo.

Asilimia kubwa wamezaa bila ndoa na wamezaa na watu ambao hawapo nao tena kifamilia so hii inamaanisha no proper family bali ni kuishi tu king'ombe ng'ombe. [emoji23][emoji23][emoji23]

Ni kizazi ambacho hakijielewi kililetwa duniani kufanya nini kwa asilimia kubwa wapo wapo tu kwenye siasa hawawajibiki, kwenye jamii hawapo, kwenye imani sifuri yaani basi tu wapo wapo bora twende.

So dah..... MUNGU atusaidie sana hiki kizazi maana tuyaishi maisha yetu kama watoto wa kafara.
 
Busara hizi ntalifanyia kazi
 
Mahali sikutoa nilihaidi tuuu ila baadae akaniomba nimlimie mashamba yake kama mkwe wake, kwakuwa sikua na pesa ya kuweka vibarua ikabidi niingie mwenyew shamban ili baba mkwe aridhike na heshima iwepo
Hapana hiyo sio heshima kwako. Moja ya kipino Cha ndoa Bora ni uwepo wa heshima Kwa wakwe wote wawili..

Kukulimisha ni upuuzi. Sio heshima.
 
Mahali sikutoa nilihaidi tuuu ila baadae akaniomba nimlimie mashamba yake kama mkwe wake, kwakuwa sikua na pesa ya kuweka vibarua ikabidi niingie mwenyew shamban ili baba mkwe aridhike na heshima iwepo
Ulilima pamoja na mkeo au peke yako? Mimi siwezi kulima hata robo heka ndo udhaifu nilio nao, na sijawahi kwahiyo mke kwa sitailo hiyo atakua amenishinda
 
Ulilima pamoja na mkeo au peke yako? Mimi siwezi kulima hata robo heka ndo udhaifu nilio nao, na sijawahi kwahiyo mke kwa sitailo hiyo atakua amenishinda
Peke yangu mke alibaki mjini
angekuwepo angenichelewesha kaz kabisa
 
Shida Ni wewe ulioa bila kutoa mahari shida ndo iko hapo.
 
Hiyo mbona ipo tuu kila sehemu kuoa bila kutoa mahali, mimi sio wa kwanza sema bahat ya mtu tuu
Mkuu inatakiwa utoe mahari hata Kama ng'ombe mmoja au laki moja maana hakunaga mahari ndogo Wala kubwa.

Mahari zote Zina same VALUE hata kama hata Kama ni different MAGNITUDE.
 
ni kweli kizazi chetu asilimia kubwa hakina dira.
 
Mkuu inatakiwa utoe mahari hata Kama ng'ombe mmoja au laki moja maana hakunaga mahari ndogo Wala kubwa.

Mahari zote Zina same VALUE hata kama hata Kama ni different MAGNITUDE.
Hiyo Laki sasa mtaji kabisa huo
 
Umeongea ukweli mchungu.Jamaa hawajui kuwa tupo hapa duniani for temporary.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…