Wao wanasema kumuhudumia siyo kosa inaruhusiwa kumpa huduma za kibinadamu, lakini wao wanamuona huyo mtoto tofauti na watoto wengine mfano uwezi kusikia mtoto wa nje ya ndoa kupewa kipaumbele kipindi cha sikukuu aende kula na kufurahi kwa Bibi na Babu wala huwezi kusikia akipewa zawadi kutoka kwa Bibi na Babu au Shangazi, Baba wadogo, kwa Zanzibar mwanaume ukizaa nje ya ndoa mtoto anakuwa siyo wako umuesabu kama una mtoto ata ukimuoa huyo mwanamke mtoto mliye mpata nje ya ndoa awezi kukurithi, kwenye mgawanyo wa urithi yeye apati ataachia wadogo zake Mali zote labda hao ndugu zake waingiwe na huruma wamgaiye nje ya urithi.