Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

Asili na Maana ya Jina/majina ya sehemu mbalimbali Tanzania

ILALA = Ni kutokana na sauti za misikitini wakati huo -- Lai la la aila (sijui ni hivyo?)
SHAURIMOYO = Ilitokana na ujambazi uliokuwepo maeneo ya mitaa hiyo wakati huo. Watu wakawa wanasema inabidi uushauri moyo wako kabla ya kukatiza eneo hilo.

Mzee Punch umenimaliza sana ha ha ha aha
 
Kilimanjaro - Kilima kyaro kwa kichaga yaani Mlima mrefu
 
Mchamba Wima
Mferejimaringo
Kibanda Maiti
Mwembe Tayari
Mwembe Togwa
Mwembe Chai(ulikuwapo na nilwahi kunywa chai hapo)
Keko MACHUNGWA
Keko TOROLI
Keko MAGURUMBASI
 
TABATA😛alikua na mwarabu eneo hilo alikua anadaiwa wenye hela yao wakimfata anawajibu UTAPATA ,Kwakua lafdhi yaki arabu iana mushkel kwenya U na P akawa anatamka TABATA
 
Magomeni-miaka ya zamani meli na treni zilkuwa zikitumia kuni kuendeshea injini.Wafanya bisahara wa kuni walitakiwa kupeleka kuni bila magome(magamba) na pale Magomeni ndio shughuli yenyewe ikifanyika...walala hoi walikuwa wakija kuchukua hayo Magome na ndio maana wakaishia kusema twenda MAGOMENI...hii ipo Tanga na Zanzibar pia

Kinondoni-kulikuwa na imani hapo zamani kuwa kuna jini liitwalo NONDO lakini likiwa dogo(Kinondo) na eneo hilo likaitwa kwenye Kinondo yaani KINONDONI...pale penye miembe miwili mikubwa baada ya makaburi...miembe ile mapaka leo inaitwa miembe jini
 
ZIMBABWE - ZIMBA ZYA MABWE au kwa Kiswahili JUMBA LA MAWE. Kishona kweli ni Kibantu.

Wao huandika Dzimba Dza Mabwe.Ila wanasoma kama hapo juu.
 
Kistaarabu wakuu hatusemi Umesema uwongo tunasema sio kweli,ambayo haimuzi sana.

Upanga -lilikuwa pori na majambazi yenye mapanga yalikuwa yanajificha huko.

yani hapa tunaongea tulivyosikia, hivyo mtu aachwe huru kuongea alichokisikia na siyo kupewa majina ya ajabu kwa mambo haya
 
Jamani nainjoi ndani ya jamii forum,haya bwana nangojea kwa hamu kusikia asili ya tanganyika-haya wadau ...
 
haha haa mbavu zangu dah.. sijui ni ukweli, sijui ni uingo.. mi sijui, lol
iringa pia kuna MKIMBIZI, jina lilitokana na mama aliyekuwa anauza gongo akafukuzwa , ndio akahamia hiko mkimbizi so watu walikuwa wanasema twende kwa mkimbizi , kwa mkimbizi, mpk leo panaitwa mkimbizi
 
IRINGA:
gangilonga- ni kihehe meanz jiwe linaloongea, kuna jiwe kubwa sn mpk leo lipo , ukipaza sauti inatoa mwangwi so wahehe wakaiita gangilonga(jiwe linaloongea)

tosamaganga- meanz tupa mawe, kijiji kiko kilimani, enzi hizo wkt vita ya wajerumani na wahehe , walikuwa wanajificha kilimani then wanasema tosa mawe yaan tupa mawe ili yawapate wajerumani waliopo chini
 
Hapana ni CAREER CALL makuli waikuwa wanakutana hapo kusubiri ujira wa kutwa ambapo waliitwa kwa majina

No ni CARRIER COPS kama alivyosema Blobu, wakati wa ukoloni pale kilikuwa ni kambi ya askari wa kubeba mizigo!
 
Tanga- Ntanga ni kizigua, maana yake ni shamba. kuna mgeni alikwenda kutembea kule na akafika sehemu akakuta watoto akauliza wazazi wako wapi wakajibu " waita ntanga" yaani wameenda shamba
Dodoma- Idodomya- yaani imezama- inasemeka ilikuwa ni marshland/wetland na tembo alizama na wenyeji wakwa wanasema idodomia
Serengeti-siring'eti- Kimaasai maana yake nyika aumbuga
 
Yani we nziri sijui ulitumwa! Umeiba idea yangu live! Nilipanga kuja na topic kama hii nikianzia na jina Tabata. Pale enzi hizo palikuwa hapana jina ila eneo hilo aliishi mwarabu akifuga ng'ombe wa maziwa. Sasa wateja walipoenda pale kufuata maziwa waliuliza, mzee maziwa nitapata. Mwarabu alijibu, maziwa TABATA! Ikazoeleka na watu wakawa wakisema naenda Tabata!
 
Yani we nziri sijui ulitumwa! Umeiba idea yangu live! Nilipanga kuja na topic kama hii nikianzia na jina Tabata. Pale enzi hizo palikuwa hapana jina ila eneo hilo aliishi mwarabu akifuga ng'ombe wa maziwa. Sasa wateja walipoenda pale kufuata maziwa waliuliza, mzee maziwa nitapata. Mwarabu alijibu, maziwa TABATA! Ikazoeleka na watu wakawa wakisema naenda Tabata!

Teh teh teh ,jamani nimecopy na ku-paste idea yako duh nsamehe !!
 
Mchamba Wima
Mferejimaringo
Kibanda Maiti
Mwembe Tayari
Mwembe Togwa
Mwembe Chai(ulikuwapo na nilwahi kunywa chai hapo)
Keko MACHUNGWA
Keko TOROLI
Keko MAGURUMBASI
KEKO MAGURUMBASI mzee wa kingoni aliyeitwa Magurumbasi aliishi eneo hilo na mabaki ya familia yake wapo hadi leo.Alikuwa akifuga mbuzi ambao walikuwa hawana mchungaji wala zizi(walizurura toka keko,chang'ombe hadi kariakoo)lakini hakuna aliyewaiba ama kuwadhuru.
 
Back
Top Bottom