Asili ya jina Tanzania na mwasisi wake: Mohammed Iqbal Dar

evaluate its present value you'll find out!

vipi thamani yake kipindi kile? Mbona wavaa trauza kabla ya kufuli?
Kipindi kile ilikuwa na thamani kubwa.jaribu kuendana na wakati. Kama ingekuwa leo ni dhahir asingepewa hicho kiasi bali mamilioni.
 
wewe mbona subjective sana. Me historia naifahamu sana. Me sioni uhusiano kati ya koran na neno dar es salaa. Hili ni neno la kiarabu na kwa kuwa koran imeandikwa kwa kiarabu ni waz litakuwepo ndani. Jaribu kutofautisha imani na utamaduni. Mfano neno good hope au tumaini jema lipo ktk biblia. Je tunaweza kuihusianisha rasi ya tumaini jema nchin afrika kusini na biblia?
Hiv upo uhusiano gani kt ya jina lako na ww? Hakuna sema mazoea na utamaduni ndo umekuathir ndo mana kama waitwa hamis utakuta wapo hamis wengi. Au waweza kutueleza wana jf nini lengo lako kupost haya makamburu[machicha]?
 
wewe kuwa objective. Mpaka umo htmu najua wewe ni mwanataaluma flani na mising ya kila taaluma ni kuwa wa mrengo wa kati na kutazama mambo ktk mtazamo chanya. Mi ninajua hst kuwa jina dar ni la kiarabu. Swala la kuwa kwe koran ni rahs kuwa imeandikwa kwa kiarabu. Au unamaana gan kupost hii coment?
 
Hiyo si comment hilo ni darsa kwa wale wasioelewa kuwa maana ya Dar Es Salaam si "Bandari salama" kama wengi wanavyotaka iwe. Maana halisi ni hiyo hapo na huo ni ushahidi wa hiyo maana?

Una swali jingine?
 
kama kawa waliomwambia mwl kuwa watagomea uhuru, asipokubali mashari yao bado wana propaganda kuwa waligombania uhuru na si mwalimu.uhuru wenyewe ulikuwepo mezani ni mwalimu tuu kuthibitisha kuwa alikuwa na uwezo wa kuongoza na umoja wa kitaifa ambao alithibitisha.
 
Tutumie picha yake na ya nyumba yake na watoto wake, separately, ili tuzihifadhi. Huenda mmoja wetu akapenda kuandika kitabu juu ya historia ya Tanzania tangu Uhuru! Waache hawa Mawaziri wa Habari wakae tu wale rushwa zao badala ya kujali mambo muhimu kwa vizazi vijavyo!
 
Acha mambo ya kihuni, si kila mtu hapa ni mvutaji. Umemeza dawa zako leo?
 
Huyu Iqbal ana bahati sana! Wajua wangejitokeza wote washindi 15 angeambulia Shs.13 na senti 30 tu? Kweli 'early bird catches the worm'!
 
Jina Tanzania limetokana na Takanyika na Nzanzibar. Majina yeto haya yametoka kwa Wasambaa na si mtu yeyote ambaye anataka kudanganya kupata credit.

Yalijiunda yenyewe?..uctumie pua kufikiria na sitaki utokwe na povu ukirudi rudi taratibu
 
Habari wanajf.
Baada ya kusoma habari hii nimeona ni vyema ku share nanyi pia kupata michango yenu juu ya habari hii.

Mwandishi wa habari hizi anaanza kwa kusema:

Historia ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kutaja jina la mtu maarufu aliyebuni jina la Tanzania ambaye kwa bahati mbaya au makusudi hakumbukwi tena.
Wengi tunaambiwa kuwa jina la Tanzania lilipendekezwa na Watanganyika na Wazanzibari, na raia wengine wa nje lakini hawatajwi waziwazi na picha zao tukaziona.
Inaaminika kuwa mtu aliyebuni jina la Tanzania ni MOHAMED IQBAL DAR, raia wa India ambaye alikuwa miongoni mwa watu walioshindana katika shindano la kubuni jina la nchi mpya baada ya Tanganyika na Zanzibari kuungana.
Mohamed alizaliwa Mkoani Tanga miaka ya 1944; baba wa Mohamed alikuwa daktari huko mkoani Morogoro akiitwa Dk. T. A DAR aliyefika Tanganyika kuanzia mwaka 1930.

Mohamed Iqbal Dar alipata elimu yake ya msingi mkoani Morogoro katika shule ya H. H D Agakhan ambayo kwa sasa ni mali ya serikali. Alijiunga na Shule ya Sekondari Mzumbe alikosoma kidato cha kwanza na cha sita.

Aliingiaje kwenye shindano la kupendekeza jina la Muungano kati ya Tanganika na Zanzibar?

Mohamed anasema alikuwa maktaba akisoma gazeti la Tanganyika Standard (siku hizi Daily News) akaona tangazo lililowataka wananchi washiriki shindano la kupendekeza jina moja ambalo lingezitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar.
Mohamed anasema alichukua kipande cha karatasi akaanza kwa kuandika jina la Tanganyika ikafuatia Zanzibar, alafu aliandika jina lake Iqbal kisha akaandika jina la jumuia yake Ahmadiya.
Aqbal Dar alichukua helufi tatu kutoka Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar akachukua herufi tatu za mwanzo ZAN na kuziunganisha akapata neno TANZAN. Anadai alianza kutafakari na kuona nchi nyingi za Afrika ziliishia na herufi za IA, kama vile Zambia, Tunisia, Namibia, Gambia, Nigeria n.k, hivyo akaamua kuchukua herufi ya kwanza ya jina lake Iqbal yaani I pia akachukua herufi ya kwanza kutoka jila l;a dhehebu lake Ahmadiya yaani A na kuziunganisha akapata jina kamili la TANZANIA, ikiwa limezakiwa kutoka majina ya Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiya.

Mohamed Aqbal Dar alituma jina hilo kwenye kamati ya kuratibu shindano, ambapo baada ya muda alipokea barua nzito kutoka serikalini na kusainiwa na Idrisa Abdul Wakil ambaye alikuwa Waziri wa Habari na Utalii wa wakati huo akimjulisha kuwa alikuwa miongoni mwa washindi katika shindano hilo.
Jumla ya washindi 16 walipatikana, ambapo iltakiwa kila mmoja ilibidi apate kiasi cha shilingi 12.50 kwa maana ilikuwa imetengwa shilingi 200 kwa ajili yao.

Mohamed aliibuka kuwa mshindi kwa kuwa wenzake 14 hawakutokea ile siku ya kutolewa zawadi hizo ila alikuwepo mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Yusufal Pir Mohamed ambaye hata hivyo alikosa sifa baada ya kushindwa kutoa barua ya pongezi ya kushinda kwa madai kuwa amepoteza (barua hizo za pongezi walitumiwa kabla ya tukio lenyewe).
Hivyo Wizara ya Habari na Utalii ikaamua kumtangaza Aqbal Dar kuwa mshindi na kumpatia zawadi yote ya sh. 200 pamoja na ngao.

Aqbal Dar anayo masikitiko ya mchango wake kutotambuliwa ingawa anaipenda Tanzania na kujivunia kuwa Mtanzania japo ana asili ya India.

Mohamed Iqbal Dar kwa sasa anaishi Uingereza kwa kuwa huko ndiko alikopata kazi eneo la Birmigham b35 6ps UK, Dar -es-salaam House, 18 TURNHOUSE ROAD, PHONE 44 21-7479822.

Source: Tanzania Daima 16 Februari, 2013.
 
Habari wanajf.

Baada ya kusoma habari hii nimeona ni vyema ku share nanyi hasa wale wanaoujua ukweli huu waweze kunijuza kwa undani.

hii habari ilishawahi kuelezewa hapahapa jf kipindi ha nyuma BTW nice remembrance..
 
Ni kweli ila inawezekana wengine hatukubahatika kuisoma, si unajua jf kila siku inapata watu wapya.
 
Kwa kumbukumbu zangu Mwl Nyerere aliwahi kusema hajui asili ya jina hilo Tanzania; sasa tumwamini nani, Nyerere au Aqbal? Hivyo, anayosema Aqbal ni kweli, au ni usanii. Achapishe hiyo barua ya pongezi iliyosainiwa na Abdulwakil. Na bado tuna MIULIZO, Abdulwakil alikuwa Waziri wa Muungano au wa Zanziba?
 
Mkuu Kyenju, mbona huu uzi upo humu jf! jamani wanajf wenzangu muwe mnatembelea majukwaa tofauti tofouti, nenda kwenye jukwaa la historia utaukuta uzi huu!!!
 
Nikweli mkuu pia nimegundua kitu kimoja, habari nyingine waandishi wanazichota kutoka jf hivyo ni vyema mtu kabla uleta habari yako kwenye jamvi ukatembelea majukwaa yote.
 
Mkuu Kyenju, mbona huu uzi upo humu jf! jamani wanajf wenzangu muwe mnatembelea majukwaa tofauti tofouti, nenda kwenye jukwaa la historia utaukuta uzi huu!!!
Kweli kabisa, mie nilimsikia mdosi huyu akihojiwa na BBC.
 
Wana Jamiiforums,,binafsi naamini jambo lolote kubwa lina sababu.Na kama lina sababu basi nyuma yake kuna mwazilishi wa wazo hilo.

Napenda kujua,,Baada ya Mwl Nyerere kutangaza nia ya kuunganisha visiwa vya Zanzibar na Tanganyika,,je nani alikuja na jina la "TANZANIA"? Je,ni Nyerere mwenyewe? Kama si yeye,ni nani? Aliishi mkoa gani? Kama ni wengi, Nani walikuwa kwenye kamati ya mchujo? JE, wako wapi hadi sasa?

Nikiwa mwananchi wa nchi hii nitafuraji kujua,mengi kuhusu Taifa langu kutoka kwa yeyote mwenye uelewa.
ASANTENI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…