DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es Salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Maji ya kopo au ya chupa au kandoro? Binafsi sijawahi kuona maji ya kopo hapa Dar.
 

Dew drops Maji yao matamu sana lakini naona hawajajipanga kiuzalishaji na usambazaji.

Wabongo wengine kwenye operations ni shida.

Huenda kuna tatizo la management na marketing kwa ujumla.

Wameshindwa ku meet demand kwa wakati .

Kila ukienda shoppers super markets hakuna Maji yao,

Shoppers wanasema wanakuwa wameagizia lakini hataki kwa wakati.

Mungu awape nini?

Kukubalika sokoni ni Neema lakini mnaochezea?

Watu wata Shift in demand wa kusubiri na kuchoka.

Mna matatizo gani?

Si muongeze mitambo ya uzalishaji?

Ongezeni capacity of production muweze ku meet demand kwa wakati.

Bila ku compromise na quality.
 
Maji ya kopo au ya chupa au kandoro? Binafsi sijawahi kuona maji ya kopo hapa Dar.
Chupa na kopo ni tofauti ,chupa ni ile ya glasi kama vile Serengeti ,coca au Pepsi ile ni chupa ! Plastic ndio kopo ,
 
Dew drops Maji yao matamu sana lakini naona hawajajipanga kiuzalishaji na usambazaji.

Wabongo wengine kwenye operations ni shida...
Dew drop nimefika hata mahali ya napotoka ni meji ya chini ,wamechimmba chini ,sio mto ,yanatoka sumbawanga mjini sehemu unaitwa kiziwite ni kampuni ya tawaqal yako poa sanaa
 
Ujanja ujanja kuhusu biashara hususan ya vyakula Dar ni mwingi.

Sio tu maji hata kwa hawa mama ntilie au wauza chipsi waweza uziwa kuku vibudu na sekela moja safi sana we hujui ama wali wa juzi umechanganywa na mchele wa leo.

Hadi mboga za majani mtihani vile vile umwagiliaji wake ni uchafu mtupu.

Ila viwanda vizuri vya maji vipo mathalan AFYA ya watercom limited Kigamboni,maji yao ni Kisima cha mwamba kimetobolewa yako poa fresh kabisa .
 
Dar unaweza kujikuta umenyweshwa Kinyesi, hilo ni Jiji la Kuogofya sana hilo.
 
Mwaka 2008 hapo K/koo ,kuna sehemu niliwakuta jamaa wanayaweka kwenye makopo hayo maji .Aisee nilishtuka sana.
Viwanda vingi vipo uswazi ,yaani Tandale ndani ndani ,keko Mwanga, Mbagala na Manzese.

Michezo hiyo ndio walianzisha wale wanaouza kwa toroli ,wale sio wa kuamini ni wachache wanauza Maji original.

Wale unakuta ana mkokoteni wa kusukuma ,amebeba maji safi ni hatar sana ogopa.

Wengin wale unakuta wapo stendi za Hiace kama pale Mbagala ,vituo vya Hiace wana friji fulani zipo hovyo , aina deep freezer
 
Hawa mtambo wao uko jikoni ni mdogo sana unatumia phezi moja ya umeme.
 
Zamani ilikuwepo security seal ambayo ilizuia mambo ya fodgery....wizara ys mazingira wakapiga marufuku....kisa ati ni kuchafua mazingira...!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Ni Dalili za maisha magumu ya wananchi. Serikali na Afya njooni huku.
 
Aliekosea ni yule aliesema, zile karatasi za kwenye vifuniko visiwekwe ndio kakosea sana.
Zile karatasi za kwenye vifuniko zifungwe.
 
Ni hatari mnoo kwa sababu hata hayachemshwi
 
Yanatoka mbali sana sumbawanga
 
Mbona huji na Chakula chako na Choo chako?
Wivu tu
 
Dar uhuni mwingi sana, tena nyie wanywa nyagi, kvanga na pombe kali ndio mna hatari zaidi. Zinazalishwa pombe bandia nyingi zilizo chini ya viwango.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…