DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es Salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es Salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Daresalama mimi huwa sili Ovyo ovyo nimeshawahi kula Pweza na Supu yake halafu kidogo nife kwa kuhara karibia utumbo unitoke.
Mkuu, hapo ndio unakomaza mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ...ukipata na kitu kama hii mara mbili kwa mwezi mambo yanakuwa🔥🔥🔥

IMG_20240302_211754.jpg
 
Matokeo ya Rushwa, TBS hapo wana bahasha zao, Dar watu wanalishwa sio tu maji hata vyakula kama kuku au nyama ya Ng'ombe ni vibudu tupu.

Dar watu wanalishwa uchafu sana.

Nikijaga Dar huwa ni wali maharagwe tu nakula, make kuchakachua mchele au magaragwe sio rahisi.

na matunda ndizi pekee,
 
Napendelea kula Wali maharagwe tu, silagi nyama Dar, wala kuku, wala mboga za majani.
 
Ila ninachokijua huku mtaani kuna wajasiriamali wadogo huwa wanaokota chupa, wanaosha, wanaweka maji kisha wanaweka kwenye friji na kuwauzia watu kwa uwazi kabisa.
Yaani badala ya kutia kwa mfuko maarufu kama kandoro, wao wanatia kwenye chupa.

Bei zao ni 100 kwa chupa ndogo na 200 kwa chupa ya lita 1 na lita 1.5.
Kwa hiyo mteja anaponunua anakuwa anajua kabisa kuwa hii ni kandoro iliyopakiwa kwenye chupa.

Sasa hao wa Mbezi kama wanauza kandoro kwa udanganyifu kuwa ni maji safi huo ni utapeli na wanahatarisha afya za watu.
 
Hili taifa ni majangaa unakuta wafanyabiashara wengine ni wasomi wameweka maji na juisi kwenye jua badala ya kuwekwa stoo na wanauziwa wananchiii na mamlaka wapo wizara ya afya,maafisa afya wa halimashauri na TBS wapo bize na posho na semina wakati tunalishwa uchafu.
 
Napendelea kula Wali maharagwe tu, silagi nyama Dar, wala kuku, wala mboga za majani.
Mboga za majani dar siku hizi zinatoka mkuranga,rufiji,dododma mpaka mwanza,tofauti na zamani zinalimwa bonde la msimbazi,Ila ukitaka uhakika wa mboga kula kipindi Cha mvua nyingi sababu mabonde hayalimiki
 
Mboga za majani dar siku hizi zinatoka mkuranga,rufiji,dododma mpaka mwanza,tofauti na zamani zinalimwa bonde la msimbazi,Ila ukitaka uhakika wa mboga kula kipindi Cha mvua nyingi sababu mabonde hayalimiki
Kuna mtu alifia kwenye bwawa jirani na kambangwa secondari mwezi ulopita na pembeni yake kuna mboga inayomwagilia kwa kutumia hayo maji na yametuama tu.
Mtu mwenyewe kwa mwonekano alikaa kwa siku 2 au 3.

DSM utakwepa uchafu huku utanaswa kule.
 
Miili yenu ikichunguzwa ina wadudu wa ajabu duniani hawapatikani
Poleni sana maana hata wachina ndio zao wao wanapewa na permit kama wawekezaji kabisa 😄
 
Nishawai nunua maji ya hilli kakoo yale maji nilipata poison ya atar nilitapika san mbaka nikawa naogop maji ya hilli ila nilikuja fatilia yale maji nilipigwa ayakuwa maji safi
 
Dew drops Maji yao matamu sana lakini naona hawajajipanga kiuzalishaji na usambazaji.

Wabongo wengine kwenye operations ni shida.

Huenda kuna tatizo la management na marketing kwa ujumla.

Wameshindwa ku meet demand kwa wakati .

Kila ukienda shoppers super markets hakuna Maji yao,

Shoppers wanasema wanakuwa wameagizia lakini hataki kwa wakati.

Mungu awape nini?

Kukubalika sokoni ni Neema lakini mnaochezea?

Watu wata Shift in demand wa kusubiri na kuchoka.

Mna matatizo gani?

Si muongeze mitambo ya uzalishaji?

Ongezeni capacity of production muweze ku meet demand kwa wakati.

Bila ku compromise na quality.
🤝
 
Nisha wahi leta Uzi humu kukemea tabia ya watu kukojolea kwenye makopo nikiunga doti na huu uzi, nachelea kusema tuna hali mbaya sana kiafya.
 
Back
Top Bottom