DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es Salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

DOKEZO Asilimia 80 ya maji ya kopo Dar es Salaam ni feki na machafu, hayafai. Kwa hali hii usalama wetu uko wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Miili yetu ishakuwa sugu, huko vijijini tulikuwa tunakunywa na ng'ombe, punda, mbwa nk
Bora kunywa maji pamoja na ng'ombe au punda hautapata maradhi yoyote, kuliko kunyweshwa kinyesi na wahuni wa DAR.

Punda anà shida gani mnyama msafi yule, kinywa chake kina majani tu!

Usiombe unywe maji ya vidimbwi vya DAR, TEGETA, BOKO BUNJU 😕😕 Ni mavi matupu!

Maji yana minofu ya mizoga kwa ndani
 
Hapo mkuu wa mkoa yuko busy . Kichwa kama senene badala ya kuhangaika wanaoandamana.
 
Kujali afya ya binadamu mwenzio hata kama unafanya biashara na unatafuta hela ni muhimu sana.

Wafanyabiashara mnatuua bila huruma sisi waja wema. Nimefika Mbezi mwisho barabara inayokwenda Kinyerezi kuna ofisi maalumu ambayo wanakusanya makopo na kupakia maji machafu yasiyofaa hata kidogo.

Wanaweka package na vifuniko wanayatia kwenye friji na kuwauzia wateja kama maji orijino. kwa kuwa yanakuwa baridi sana huwezi kugundua chochote. Hao wamana wanaofanya kazi hapo na mazingira ya eneo ni machafu kupindukia, makopo hayaoshwi na wanayaokota majalalani na kwenye mitaro michafu.

Makopo mengine yanakuwa na mikojo wao hawajali hilo wanachojali ni kupata pesa. Hii ni hatari sana!

Maji haya tunawanywesha watoto na wagonjwa. Ndiyo sababu magonjwa ya kuhara haishi hapa mjini. Jeshi la polisi na wenye viwanda jaribuni kubuni namna nyingine na kufanya misako kwa wenye hizi biashara. Wanatuua bila huruma.
Achana na maji ya kopo. Nunua ya chupa.
 
Back
Top Bottom