Asilimia 88 ya vijana (umri 30 - 35) hutegemea wazazi na mashemeji

Ulifanyaje mkuu
Simple tu nilimnyima ugali,nilimpa kama wiki mbili kuwa atafute pa kwenda kula hapa kwangu awe anakuja kupiga story tu na kusalimia.
Dogo akafikiria masihara,zilivyopita wiki mbili nikaongeza siku kama tatu nne hivi.Siku ya siku ilivyofika nikachukua tu mabegi yake nikayatoa nje,tena ilikuwa jioni.Nikaenda zangu kulala.Shemu akaenda Kwa sister yake (Wife) kuwa anibembeleze nimhifadhi Kwa muda.Nikakubali kuwa kesho aondoke.Dogo kesho yake akaenda kujihifadhi Kwa Shangazi yangu mimi,kule Kwa Shangazi akaona aibu alikaa wiki moja tu akatafuta kazi nyingine na akasimama mwenyewe na mpaka Leo Huwa ananambia Bila Mie kumkomalia angekuwa kapotea.
Mnyime tu ugali
 
Ila nilifanya hivo baada ya kuona dogo hataki kufanya kazi na kaanza kuwa msumbufu
Hongera Mkuu. Mm 2016/17 nilianzisha mahusiano na Divorced woman flan baada ya kunieleza matatizo yake pia nilivutiwa na umbo lake (wezere kama lote japo alikua na smell ya ajabu sana ila nilivumilia) basi akaomba nimlipie kodi nikaona why nilipe kodi wakati nina kwangu akahamia kwangu mwanae wa kiume alikuwa SAUT-Mwanza final year basi alipomaliza mqsomo Julai 2016 nikamtafuta kazi ofisini akawa analipwa 35,000 per day. Na hapo ofisi inatoa chakula na usafiri na home anakaa bure halipii chochote. Kafanya week 2 tu kaacha. Aisee kumuambia Mama yake anadai namnyanyasa mwanae kwa sababu mm si baba yake nilicholifanya nilienda kukodi kirikuu wakabeba vilivyo vyao hasa nguo na mapazia mm nikabaki huru nikihitaji nanunua tu
 
Umetisha mkuu
 
Mashemeji mnajilegeza mno ipo siku mtaombwa "O" position ndo muanze kuhamaki
 
Hii uwa inaanzia kwa mtoa mada
 
Mm baada ya kuhitimu chuo nilienda kwa kaka dar kuishi, nilifanyiwa vitimbi mara kuitwa mchawi, nikaondoka kwenda kupanga , nashukuru Mungu sasa nimeajiliwa serikalini ,nimeoa, nina watoto, nimejenga .

Vijana kwa ndugu sio pakuishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna shemeji yangu kazaliwa 1985 anaishi kwa shemeji yake aliyemuoa dada yake na hana dalili za kuondoka hivi karibuni. Najua hayanihusu ila nashangaaaga saana

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkuu ukamfukuza na mama yake kabisa [emoji3][emoji3]
 
Ni kweli mkuu vijana wengi wamekuwa legelege wanategemea kuwezeshwa at the age of 35 someone must be very responsible for your own life and the family at large.
Siamini huo umri ni mkubwa sana kubaki nyumbani labda kwa wadada lakini nao lazima waolewe 30-35 duu parefu
 
Nilijifunza from my own experience,nilikaa Dar kwa msamalia sio ndugu karibu mwaka nalala nakula na nilikuwa na kibarua kwa mwezi 270k take home lakini hadi naachishwa kazi sikuwa hata na kijiko nikawa omba omba ghafla kwa washkaji
Nakumbuka hadi nauli jamaa alininipa msaada nikarudi home kwa dingi mdogo nae kwa tukazinguana akanitolea mabegi nje kuanzia hapo ndo ikawa safari ya kujitegemea nilimuona hafai lakini nimekumbuka bila yeye huenda nisingefika hapa,nadiriki kusema nitamtafuta nimshukuru maana nilimchukia kwa kitendo kile japo kesi ilikuwa haihusiani
So kukaa kwa mtu utalemaa yaani hata leo akija dogo namtimua sembuse mashemeji lazima mtu awe na mpango mkakati wa kujitegemea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…