Asiyesikia la mkuu! IMF walituonya, sasa uchumi umeshuka kwa 2% kwenye robo ya kwanza

Umeambiwa kuwa hiyo taarifa ya sasa ni taarifa ya Tanzania Bureau of Statistics. Au na huko wapo IMF na WB?

Hata kama tunaipenda nchi na Rais wetu namna gani, ni upuuzi na kuvia kwa akili zetu kuukataa ukweli. Kwa sababu hata ukikataa kama ukuaji wa uchumi umeshuka, utabakia kama ulivyo. Hautapanda kwa sababu umekataa.

Wenzetu taarifa kama hizi huzitumia sana positively. Hata Marekani kuna wakati uchumi ukuaji wake huwa unashuka. Wanaukubali ukweli na kisha wanabadilisha baadhi ya sera ili kuokoa uchumi. Sisi tunaokoa kwa kukataa kwa mdomo. Hopeless!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wataalam wa uchumi tuambieni viashiria vya kukua kiuchumi wa nchi

Ova
 

hilo nalo neno.....
 

 

Baba wa Taifa alishatuonya sana kuwasikiliza hao IMF na alituambia IMF sio wajomba zetu and is not an "International Ministry of Finance"
Hivi walishawahi kutuonya hata siku moja kuwa uchumi wetu unashuka kwa asilimia ngapi kwa kusafirisha makinikia na akina Barrick kurusha dhahabu zetu directly nje kutoka machimboni?
Walishawahi kutushauri kujenga smelters kwetu ili kudhibiti wizi na kutengeneza ajira nchini kusaidia uchumi wetu kupanda?
Unapowasikiliza kuwa makini kuchanganya na za kwako.
 
Mbona hata vitu unavyojadili huvifahamu? Au lugha is not reachable? Hujachelewa Ras SSimba yupo, kajifunze ngeli
 
...safari ya kuelekea Zimbabwe imeshika kasi....Na dereva aliyeshika usukani anakaza mwendo ili tufike upesi....huko njiani mabenki hayana liquidity (pesa)kisa dereva ameona bora mapesa yarundikane garini(BoT)....raia wanalia njàa...dereva anawaambia kuleni majani...lakini yeye na inner circle yake wanakula asali na maziwa na nyama...tena kwa mbwembwe....hii safari hata tukifika zimbwabwe...wengi watakuwa wamefia njiani....maana dereva anatuswaga kama magunia...God forbid....
 
hii sijui ina ukweli au ndio figisu tu za kutuharibia nchi yetu

 
Hiyo retardation ya 1.1% haikufanyi uchekelee,haswa ukitilia maanani hiyo ni first quater

Kumbe wewe ndio furaha yako! Tulia tushuke tena uchekeleee! Ndio nyie wa "tutanyolewa bila maji" puuu (hapo nimetema mate chini)
 

Unapswa kujibu hoja kwa hoja sio kusema kwa sababu ni IMF ndio waliosema basi sio la kweli. Je unahizi uchumi unakua? Nyerere alitu-fail kwenye uchumi ndio maana akaachia ngazi. Yeye sio wa kumsikiliza kabisa. Tulikula ugali wa njano enzi zake. Swala la Barrick kurusha makinikia (if its true) na IMF vina connection gani? Kinachofuata sasa utasema watukumbushe luku ikielekea kuisha nyumbani. Swala la smelter lina issue ya viability. Ni nchi ngapi zina madini lakini hazina smelter? Jiulize kwanini. Tunayo volume ya ku-justify?
 
Kwani Serikali imefanya nini kilichoshusha uchumi zaidi ya kuwabana wakwepa kodi na kudhibiti madili ya kifisadi? Maana kama UFISADI na ukwepaji kodi ndio ulikuwa unapaisha uchumi wetu basi tuiingize CHADEMA madarakani.
 
Kwani Serikali imefanya nini kilichoshusha uchumi zaidi ya kuwabana wakwepa kodi na kudhibiti madili ya kifisadi? Maana kama UFISADI na ukwepaji kodi ndio ulikuwa unapaisha uchumi wetu basi tuiingize CHADEMA madarakani.
Hata kuwabana wakwepa kodi kunaweza kufanyika kwa namna ambayo inabomoa uchumi zaidi ya kuujenga.

They say "the road to hell is paved with good intentions". The law of unintended consequences applies most charitably in the most inopportune occasions.

Rais kubwatuka ovyo, hata kama anasimamia jambo la kweli kimsingi, kunaweza kuangusha uchumi.

Na hili si jambo la Magufuli na Tanzania tu. Juzi Donald Trump kabwatuka kwamba anaweza kumpiga Mkorea Kaskazini kivita.

Dow Jones Industrial Average imeanguka points 205 kwa siku moja watu wamepoteza mabilioni ya dollars.

Kwa hivyo, hata kama uongozi wa juu wa nchi unasimamia kupinga ufisadi na ukwepaji wa kodi, habari hizi inabidi zifanywe kwa weledi wa hali ya juu na kuepuka kuropoka kwa kauli ambazo zinabomoa zaidi ya kujenga.

Sasa hivi wawekezaji wanaogopa kuja kuwekeza Tanzania kwa sababu Magufuli kwa kauli zake zisizo simile amejenga image ya kwamba hayupo business friendly.

Kuendesha nchi kunaweza kulinganishwa na kuendesha lori kubwa, hata kama ukiona umepotea njia na unakoelekea si sahihi, hutakiwi kufunga breki kwa kasi usimame mara moja ubadili muelekeo katika sekunde chache, utasababisha ajali kubwa.Unatakiwa usimamishe gari polepole kwa usalama mpaka upate nafasi ya kugeuza.

Magufuli kwa kutaka kuleta vita ya kiuchumi kwa pupa, badala ya kusaidia kukuza uchumi atauharibu zaidi.
 

Kwa hiyo solution ni kumshauri RAIS asiwabwatukie wakwepa kodi na MAFISADI awe anasema nao kama Kikwete alivyokuwa akisema na MAFISADI na wapiga dili ili uchumi upande.
Tumshauri RAIS aache vita ya kiuchumi ili waendelee kutuibia IMF watusifie halafu uchumi wetu upande.
 
Wenye utaalam wa uchumi tusaidieni, ni nini maana ya uchumi kukua kwa asilimi 1, na nini maana ya uchumi kupungua kwa asilimia 1, je impact yake ni ipi?. Naomba elimu tafadhali
niliwah kuuliza swali hill muhim non maana ya kukua kwa uchumi
 
Rais wako hashauriki, ukishaanza na "kumshauri rais" tu ushapotea. Your sarcasm is conceptually lacking.

Na ukishamchagua mtu anayehitaji kushauriwa mambo basic kama kauli tu ushaboogie step.

Huu uchumi ukianguka sitashangaa na sioni haja ya kusikitika.

Ni funzo la Darwirian evolution tu.

Nyerere alikuwa anasema "ukigusa moto utaungua tu".

Ndiyo haya sasa.Mmegusa moto, mkiungua sishangai sana.

Wewe rais anawaita mawaziri aliowateua yeye mwenyewe "wapumbavu" openly, bila kujua kwa kufanya hivyo anajiita yeye mwenyewe mpumbavu.

Uchumi ukianguka utashangaa vipi?
 
Huna tofauti na yule alokuwa msemaji wa Saddam Hussein kipindi kile cha vita. Labda kwa kuwa uko kwenye wanaoneemeka

Sent by Tukunyemamzee
 
Kwani Serikali imefanya nini kilichoshusha uchumi zaidi ya kuwabana wakwepa kodi na kudhibiti madili ya kifisadi? Maana kama UFISADI na ukwepaji kodi ndio ulikuwa unapaisha uchumi wetu basi tuiingize CHADEMA madarakani.

Nimekukusanyia vichache kama hauvijui

1. Kubwatuka ovyo (unpredictability and uncertainty) - hata watendaji wanashindwa hata kutoa usharui sasa. Ukitoa ushauri tofauti unatumbuliwa.

2. Maamuzi ya ghafla (unpredictability) k.m viroba, makinikia (hata kama wanihisi wizi kuna namna ya kushughulikia. Kama wamekosea je?), Bombarider

3. Kutolipa suppliers (kuna makumpuni mengi yana filisika yanaidai Serikali. Tunajua Serikali huwa sio mlipaji mzuri sana lakini safari hii ni balaa. Trillions zinadaiwa zimeshikiliwa na bwana mkubwa)

4. Reduced Governement spending imeupunguza mzunguko wa hela ambao kimsingi ndio uchumi. Sisemi hela itumike vibaya, naongelea kulipa suppliers, kuweka hela commercial banks, serikali kufanya biashara na private sector (mfano uko number 5)

5. Serikali kutaka kufanya kila kitu kwa mtazamo mbovu kwamba akitajirika mtu binafsini vibaya. k.m Sasa hivi kila taasisi ya Serikali inambiwa watumie huduma ya TTCL wakati TTCL ina huduma mbovu, reponse ni slow na inaathiri efficiency ya watumiaji. Anataka kuua privte competition wakati anashusha quality of servie hapo hapo na kuathiri shughuli za wateja

6. Aggressive taxation - mara kodi kwa bank services, alafu unawazui wasipeleke hio cost kwa wateja, tax on auxillary services (port) ikaamisha biashara kwenda kenya/mombasa na South Africa. Hiyo tax ni ndogo sana ukiangalia pesa serikali na wananchi wangepata kwa malorry kununua mafuta, kipato na matumizi ya madera, familia zao (kodi kwenye mafuta ya malorry, mishahara, VAT kwenye goods and services sold to the logistis industry. Hiyo tax on auxillary services kenya hawana na tunapaswa kushindana nao kuvutia mizigo port. Hata kodi inaweza kuua uchumi

na kadhalika.....

Production and consumption of goods and services = Uchumi = Mzunguko wa hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…