Asiyesikia la mkuu! IMF walituonya, sasa uchumi umeshuka kwa 2% kwenye robo ya kwanza

Endeleeni na propaganda uchwara zenu,kila mnalolianzisha baya linafeli na bado mtaendelea kukosa hoja hivohivo by 2020 mnakufa kifo cha mende kwa sababu ya ujuha wenu,CCM itaendelea kuwaongoza tu kama hamtoacha ujinga na kuanza kutumia akili.
Unapigania na kulilia huo wa taifa kushuka kishabiki tu.. Wakwako na familia yako umeupandisha mpaka ngapi??! Pambana na hali yko, ya Ngoswe muachie Ngoswe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
.
Duh, kwa hiyo ni mwendo wa kushuka tu?
Kufa hatufi ila cha moto tutakiona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna dhana zinajirudia rudia hapa.

Ukiangalia habari ya kutaka taasisi za serikali zote ziweke fedha benki kuu, ingawa nia inaweza kuwa nzuri kubana ufisadi, lakini hili nalo limechangia kupunguza mzunguko wa fedha na kuzidisha muanguko wa uchumi.

Hili lina elements za uliyoyataja hapo juu.

Kutoka 1 serikali imekurupuka bila uchunguzi wa kina.Kulitakiwa kuwe na quantitative analysis ya kujua tubane mpaka point of diminishing returns tu, tukizidi kubana zaidi ya hiyo point tutaharibu.

Serikali yetu haijui nuance ya ku determine "point of diminishing returns".

Ni kama mtu anayeambiwa "aisee, biashara ya dhahabu kwa sasa inalipa sana, nunua dhahabu" akaenda kununua dhahabu tu, mradi ananunua dhahabu, bila kujua kwamba hata ukinunua dhahabu, ukinunu kwa bei inayozidi bei unayoweza kuiuza, ingawa kununua dhahabu ni kitu kizuri, utakuwa unafanya baishara kichaa.Unatakiwa ununue dhahabu kwa bei itakayokuja kukupa faida tu.

Sasa hapa nalinganisha juhudi za serikali kubana ubadhirifu kwa kutaka fedha zote za taasisi za serikali ziwekwe benki kuu kuwa sawa na kununua dhahabu.Hili ni jambo zuri kimsingi. Lakini, lifanywe kwa weledi na kiasi.Tujue, tubane kwa kiasi gani ili tuepushe ubadhirifu to the maximum possible without afecting the economy by choking money circulation.

Hapo ndipo kuna tatizo. Serikali ikishasema tu "taasisi za serikali zina ubadhirifu mkubwa sana, tuzuie vipi?" jibu linakuwa simple and because of this, stupid. Weka hela zote benki kuu.Za wabadhirifu na wasio wabadhirifu, zote weka benki kuu zikae tu bila kutumika katika mzunguko wa baishara.

Ukiangalia mambo mengi hayo ya reduced government spending concept hiyo hiyo inajirudia.Watu wanapata jibu fulani, hawafanyi quantitative analysis - especially troubling since we have a Chemist PhD who should know a thing or two about quantitative analysis, this is secondary school chemistry after all)
 
Hhhaahahaha what do you mean first lady mkuu
 

Ni kweli dhana zinajirudia kwa mifano tofauti. Kimsingi kama ulivyosema, nia ni nzuri na nia ni Ku-solve issue ya corruption lakini mtu anakua so obsessed with that anashindwa kuona "the bigger picure" - throwing the baby with the bath water.
 
Ni kweli dhana zinajirudia kwa mifano tofauti. Kimsingi kama ulivyosema, nia ni nzuri na nia ni Ku-solve issue ya corruption lakini mtu anakua so obsessed with that anashindwa kuona "the bigger picure" - throwing the baby with the bath water.
Throwing the baby with the bathwater.

Ni kama mtu anayetafuta dawa ya UKIMWI halafu anatafuta dawa yenye nguvu kabisa itakayokiuilia mbali kirusi cha UKIMWI, lakini pia, kwa sababu ni kali sana, itakayomuua na mgonjwa pia.

Hiyo itakuwa si dawa.

Itakuwa sumu mbaya sana.
 
1. Unpredictability kwenye nini? kwenye kushughulikia wezi? yaani wezi wanataka RAIS awe predictable? huo ni uzuzu.
Nani katoa ushauri wa maana akatumbuliwa au unahisi mkuu?
2. Kwenye viroba ulitaka aamue taratibu wakati kwanza tulishachelewa sana! hadi vijana wakawa mazezeta barabarani?
Makinikia pia ulitaka tuendelee kuibiwa kwanza ndo aamue? ndo uchumi wetu ungekua?
3. Katika hali tulipokuwa tumefikia hakukuwa na jinsi mkuu. katika madeni yote ya suppliers ilikuwa ni lazima kuhakiki madeni genuine yalikuwa ni yepi. Hakuna kiongozi yeyote anayeweza kurekebisha uhovyo tuliokuwa nao bila kwanza wananchi kuumia hapa na pale. Hata Mh RAIS alishatuambia kuwa kutakuwa na kuumia kwa kipindi fulani ili kuirejesha nchi kutoka kwenye uhovyo tuliokuwa tumeufikia. Ni kweli kuna suppliers genuine kabisa wamekumbwa na maumivu haya hata wafanyakazi tuna madai mengi hatujalipwa lakini kwa tunaoelewa anachokifanya RAIS na malengo yake tupo happy kwa sababu tunajua wenye madai halali tutalipwa tu baada ya kuhakiki madeni na kuondoa madeni hewa.
4. Hili silijui vizuri.
5.Mkuu ushauri hapa ni serikali ijitoe kwenye biashara ya simu ili akina Voda, Tigo waendelee kuneemeka. Maana haiwezekani watoto wako ndani ya nyumba wakale pilau kwa jirani kisa kwako umewapikia ugali. Sioni shida kwa serikali kusisitiza kutumia TTCL ili nayo ikue itoe huduma bora. Kwanza unajua ni kwa nini TTCL imekuwa ikifanya vibaya? Imehujumiwa sana na hayo makampuni unayoyasifia mkuu. The story is very long ukitaka kujua kwa nini TTCL haikui.
6 Sijajua kama kuna kodi zozote zimeongezwa hadi uite aggressive taxation. Ninachojua usimamizi umeimarishwa zaidi which is a good thing.
 


1. Kutofuata utaratibu na maamuzi bila analysis. Kwa mfano kutishia kufuta leseni za telecoms kwa sababu kila siku wanalipa fines. Unajua jinsi gani hizo fines zilivo ridiculous? Telecom inapewa call centre phone response minimum target ya 98% wakati international industry standard ni 96%. Wanapigwa fine kila kukicha kwa sababu ya impossible target. TCRA wanajua lakini uoga umetanda. Kulazimisha uuzaji wa 25% soko la hisa kwa ALL telecoms and ISPs. Ziko ambazo hata hazina sifa za kuuza hisa. Vodacom wameshindwa mpaka imebidi wauuze kwa foreigners. What about Airtel and Tigo? Itakuaje? Nani atanunua? Uniformity iko wapi? Kwanini wamezuia uuzaji wa makinikia bila proof kwamba kuna wizi. Why not investigate, get proof then decide? Kama hakuna wizi je? vipi kuhusu damage ya reputation kwa foreign investors na kwa kampuni ya Acacia? Wizi wa ACACIA uko kwenye mkataba tulio sign, which is all legal. Si watetei nasema tutaumia mara mbili na kutisha wawekezaji wengine. Leo unaweza ukaanzisha biashara ikafungiwa kesho kutwa na huna pa kulalamika. Watu wameshikilia hela kwa sababu hii

2. Nilipata harabi ambazo azijathitishwa kwamba wanataka kuruhusu tena

3. Lazima tuangalie bigger picture. Hakiki bila kuumiza biashara za watu. Hiyo hela ni haki yao. Watu wanafamilia. Unasema hivyo kwasabu mshahara wako unaupata. Niliwahi kwenda kampuni moja imewarudisha wafanyakazi wake wote nyumbani mpaka madeni yake yalipwe. Dont throw the baby with the bath water. Kuua mtu mmoja unalipua basi la watu mia?

4. No comment

5. Nchi haitaendelea kwa kulea "watoto wa ndani". Uchumi utaendelea kwa kuweka mazingira ya "free market". Hapo ndio innovation na growth inapatikana. Hizo fikra za "kulinda" ni za wakati wa ujamaa. Kuna ubaya gani Voda na Tigo kuneemeka? Unakumbuka wakati hawapo? Kulikuwa na nani? Wameajiri wangapi? Wamesaidia kiasi gani maisha yetu na biashara zetu? Wamelipa kodi kiasi gani? Kinachorudisha TTCL nyuma ni siasa kuingilia na "no sense of ownership" amabyo inakumba makapuni yote ya kiserikali. Angalia Managing Director wa TTCL aliyewekwa sasa hivi. I'm sure he is smart guy lakini ana zero experience in the industry na zero experience in senior management. Alikuwa Branch manager wa benki. Unafikiri anaweza kuwa kupata kazi senior managment Voda au Tigo? No way! Why? Vyeti havitasaidia kwa hili. Najua ana masters from UK. CEO wa safaricom hana hata degree moja na ni the highest paid CEO in Kenya ila ana uzoefu wa industry, anaelewa industry dynamics na Safaricom inafanya vizuri sana. Hivi vitu havifundishwi vyuoni. TTCL haikupaswa kushindana na kin aVoda. It should be supplying to them. TTCL Inasimamia NICTBB (national ICT Back Bone) kwa uzembe mpaka telecoms zimeamua kujiunga na kutegeneza ya kwao for back up.Inayo infrastructure to supply to all major telecoms. Kwanini wasisimamie na kuboresha hilo/perfect that?? Naona jamaa anahangaika kujaribu kushindana nao kwenye retail market ambako yuko very very weak kwa sababu haelewi position yao kwenye industry. Maamuzi based on emoitions. Sasa utambeba kwa kulazimisha watu wanunue huduma mbovu kwao. Hapo unamsaidia nani?

6. Kaka kama ujui kuhusu kodi kuongezeka,unabisha nini tena. Fanya research. Zimeongezeka. Just to add kodi is not always a good thing. Dubai imeshamiri kwa sababu ya kuondoa kodi. Just an example
 
Magufuli hapo nyuma kila sehemu alipokuwa akihutubia alisimama kwa mbwembwe na kutamba kuwa uchumi umekuwa huku akitumia izo data za IMF. Leo umnaziita et ni data za mabebari.

Siku ukiona unabeba ndoo ya pesa ya tz kwenda kununua toilet paper ndipo akili itakukaa sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leta reference Baba wa Taifa akituonya juuu ya IMF. Alfu hizi data hazijatolewa na IMF. Wao walituonya tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona magufuli mpaka hivi sasa anamazungumzo yasiyokuwa na mwisho na wale aliowaita wezi wenye campuni ambayo haikusajiliwa lakini mpaka hivi sasa wanaendelea kusomba madini yetu wakati hawajasajiliwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwanza hizi habari za kupika, hazinw ukweli wowote. Hiyo first quarter ya budget hii imekwisha lini? Au financial year quarters siku hizi zina mwezi mmoja na nusu tu?

Kama hiyo halitoshi, tazama upupu huu:

6.8% - 5.7% kikwenu jawabu ni 2%?

Kikwetu umeongeza idadi kwa 100%. Hiyo ni only 1.1% simply 1% rounded.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…