Asiyetakiwa ni Waziri Mkuu Majaliwa, kila kitu kimepangwa, ajiandae kuachia ngazi


CCM ipi? Hii inayomtegemea Jecha kufuta uchaguzi inaposhindwa?. Punguza uongo na maneno mengi.
 
Saana
 
Huu ni ukweli Mchungu
 
Reforms na Rebuilding ya mama Samia si mchezo. Mliozowea kuishi kimazowea mtakuja na kila hoja ya kijinga.

Majaliwa niliwahi kuandika uzi kuhusu yeye siku nyingi sana.

Binafsi, bila kutafuna maneno namuona Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa ni mnafik na ameshindwa kabisa yake.

Haiwezekani Halmashauri zote na idara zote nyeti zilizo chini yake ziwe na madudu na yupo hapo kwa miaka.

Majaliwa anaufahamu wizi wote unaoendelea serikalini na anaufumbia macho au kwa makusudi, au usaliti? Au hayupo "competent".


Madudu yanayoongelewa bungeni ilikuwa inatakiwa Majaliwa awachie ngazi yeye mwenyewe kabla hajaambiwa na mtu.

Dudu moja tu lilimfanya Lowassa awachie ngazi.
 
Wabunge hudhani wananchi wao hawana akili na wao wana akili kiasi cha kufanya siasa za kinafiki na wananchi wao wasijue unafiki wanaoufanya bungeni. Kwenye huu mjadala wa ripoti GAG wanachangia kinafiki kwa kumlenga yule aonekane ni mzembe hakuchukua hatua kudhibiti ubadhirifu wa fedha za umma na hatimaye aachie ngazi kwa aibu. Hizi ni siasa mufilisi za kuangalia mkulu anasema nini na anataka nini, akisema stupid basi inakuwa ndiyo muelekeo wa siasa na wabunge wanazama huko kukomalia
 
Ila chama cha mapinduzi k8na wanachama wanao ishi kindezi kweli kweli.
Wao wanajifanya wanampenda Waziri wao mkuu kiutendaji, lakini akionewa kwa mifumo ya wajanja na majizi ndani ya CCM hakuna hata mmoja anaye simama kumtetea au kumsemea.
Hawa ni kondoo kweli kweli!
 
Ata akitoa taarifa sehemu husika,bila utayari wa mfumo kuchukua hatua basi ni kazi bure
 
Wizara Gan yenye madudu ipo Ofisi ya Waziri Mkuu?

Faiza bana
 
Akifanikiwa kumungoa tu, kitakachofuata ni zamu yake na yeye kungolewa ili na yeye ayapate machungu ya kuwangoa wenzake...
Msimamo wa uchaguzi 2025 kukiwa na Tume huru ya uchaguzi ndio kutamfanya Samia ajue Rungu ni nani na alipatwa na nini kwenye uchaguzi Zambia.
Atakutana na ubao ukisema;
*Mgombea ACT Wazalendo: 4.8%
*mgombea NCCR 2.08%
*Mgombea CCM 39.8%
*Mgombea Chadema 52.01%
*Wengineo wote 2.2%.
 
Hiyo ni siri ya wazi ... maandishi yako ukutani. "The writing is on the wall'
 
Hata mimi naona, kwa kuzingatia ripoti ya CAG ingekuwa heri kabla maazimio hayajafikiwa atumie kichaka hicho kuachia ngazi yeye mwenyewe.

Ajipange kwa wakati mwingine tukiwnza kuwa serious na fedha za umma. Alinde heshima yake kabla hajaangushiwa jumba bovu.
 
Kwa hivyo mama anatengenezs njia kutoa ccm madarakani. Pale mwanzo akihojiwa na chombo kimoja cha huko ubeberuni alijidai yeye analeta demokrasia hatajali hata ccm ikipoteza uchaguzi. Hii ni lugha wanapenda mabeberu kusikia. Asichojua mama ni kwamba demokrasia yetu kwa mabeberu ni kuwapa mwanya kuendelea kututawala kiuchumi. Watanzania wameshajua viongozi wanaowataka. Kama mama anajitengenezea njia kupitia ccm ajue ccm itatoshwa madarakani.
 
Wewe empty kabisa. Lowasa alitolewa kafara na JK Kwa ahadi za uongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…