Asiyoyajua Yericko Nyerere katika utafiti wa historia ya Mapinduzi ya Zanzibar

Mimi siku zote nasema Yeriko sio mtafiti anachokifanya ni kuunga maandishi ya watu na kijifanya kaandika yeye huwezi kumlinganisha Yeriko na gwiji kama Dr Mohamed Said tatizo vijana wengi ni wavivu wa kusoma wakiona porojo za kina Yerico wanajua wao ndio watunzi
Nakuuliza na wewe...!

Je ulianza kumsoma Mohammed Said lini?

Umeshasoma na kuelewa vitabu vyake vipi japo viwili?
 
Nenda kasome ewe ndugu Muislam wacha ngebe mfu.
Azarel,
Ukija na lugha kama hizi za matusi utaharibu mjadala kwa kuwa
tutawakaribisha watu hodari kwa matusi kukushinda.

Huu ni mjadala tu hatugombani.
Tuwe waungwana na tuheshimiane.

Kuhusu kusoma nimemsoma vizuri Yericko na ushahidi ni huo
hapo chini.

Nimeweka bold katika hayo aliyoandika ili uone ujuzi wake katika
uandishi.

Hayo ni makosa na sikusahihisha yote aliyoandika hizo ''paragraph,''
nyingine nimeona nikuachie wewe uzionyeshe.

Halikadhalika sikuona haja ya kusahihisha makosa ya ''facts,'' na
makosa mengine kama ''spellings,'' etc. katika hayo aliyoandika
kwani hakika inachekesha na pia inachosha.

Mathalan anasema Mtaa wa Stanley ni Mtaa wa Lumumba...

Nina mengi naweza nikakueleza katika hayo aliyoandika ikiwa
utapenda.

Kwa sasa nasimama hapa.

Tafadhali hebu na wewe soma hayo yaliyomo katika kitabu cha
Yericko hapo chini (''Nenda kasome ewe ndugu Muislam wacha
ngebe mfu).''

Nimesoma ewe ndugu yangu kwani wewe hivi vichekesho hukuviona?:

KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU KAMA ILIVYOANDIKWA NA YERICKO NYERERE
Mohamed Said January 18, 2017 0

.............Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maalumakwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanzaKlest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu CesilMatola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.

Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.

Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.

Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
 
Mhhh....

Mzee, naomba niweke wazi tu kuwa binafsi sijawahi kukisoma kitabu cha Ndugu yangu Yericko Nyerere zaidi ya Makala zake na nafikiri alikuwa bado hajakamilisha kitabu hasaa.

Naomba niishie hapa kwa kusema kuwa nitamsoma zaidi kadri nitakapopata muda.
 
Ridhwani...
Una jina zuri sana na naamini unajua maana yake.

Huba sababu ya kunitishia kutukana.

Ikiwa hiyo ndiyo hulka yako usijuzuie fanya lile linalokupendeza
usijali uzee wangu.

Ikiwa umelelewa katika nyumba isiyo na adabu nani wa kukubadili
katika umri huo uliofika?

Mimi sijaandika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar lakini nilikuwa
Mtafiti msaidizi wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti kitabu
chake maarufu, ''Kwaheri Uhuru Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

Inaelekea hukijui kitabu hiki kutokana na jinsi ulivyotoa fikra zako
hapa Majlis na kusema unaiamini historia iliyoandikwa na Mihangwa.

Kwa taarifa yako Mihangwa anaandika makala kuhusu Zanzibar hana
kitabu alichoandika kuhusu Zanzibar.

Kuandika kitabu hili ni jambo lingine kabisa.

Hiyo mosi.

Pili nimeandika na kuzungumza kuhusu historia ya Mapinduzi na
naweza kukuwekea link hapa zikusaidie.

Tatu sina khiyana dhidi ya Yericko ila naandika kusahihisha yake
ambayo mimi naona yamekosewa na hii ni kawaida katika duru
za uandishi na duru za kisomi.

Nne nakushauri tufanya mjadala wenye adabu na ustaarabu hizi
lugha za ''povu,'' zitumie kwa watu wengine kwangu si mahali pake.

Kwa kuhitimisha nakuomba urejee tena katika post yangu na angalia
zile picha za Mzee Mkwawa na Victor Mkello.

Katika vitabu ulivyosoma vya historia ya Zanzibar umepatapo kuona
mahali popote wametajwa?

Wale na wengine sikuwaeleza ndiyo waliokuwana funguo za mapinduzi
ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.

Hata Mihangwa hakuwa anawajua hawa.
Kwa mara ya kwanza kawasikia kwa Dr. Harith Ghassany.
Ahsanta[emoji120]
 
Nakuuliza na wewe...!

Je ulianza kumsoma Mohammed Said lini?

Umeshasoma na kuelewa vitabu vyake vipi japo viwili?
Nimemsoma sana kiuandishi huwezi mlinganisha na Yerico mambo anayoaandika yeriko ata ww unaweza maana ni kuchukua tu machapisho ya watu na kuyasimulia ubunifu ni zero
 
Huyo ndie Mohamed Said, ni kiumbe cha ajabu sana sana, ana gubu lisilosimulika kabisa....

Ameletewa kila aina ya ushahidi wa kinyaraka, anahamisha magoli.... Hahaaaha daaah ni wakumsamehe tu huyu mzee... Ni mnafiki haijapatapo kutokea duniani....
Yericko nilikuwa sijui ww nawe km ni mpuuzi kiasi hicho uwezi hata siku moja mtu mwenyewe umri zaidi ya baba yko ukamwita mnafiki na ana gubu naweza kusema watu wa bara wote fikra zenu na wazo yenu ni sawa sioni tofauti ya kauli zako na jmp pamoja bashite kumbe wote baba moja mama moja sijawai kkufikiria kuwa mkosefu wa adabu kiasi hicho mzee kaleta hoja jibu hoja ebu niambie kuna tofauti hapo na walio jaribu kujibu hoja za lisu kwa risasi badilika bila hivyo utofika mbali ww bado kijana mdogo sna...
 
Mimi siku zote nasema Yeriko sio mtafiti anachokifanya ni kuunga maandishi ya watu na kijifanya kaandika yeye huwezi kumlinganisha Yeriko na gwiji kama Dr Mohamed Said tatizo vijana wengi ni wavivu wa kusoma wakiona porojo za kina Yerico wanajua wao ndio watunzi
Shamba,
Yericko
anaandika historia za Abdul Sykes na baba yake Kleist katika historia
ya African Association na TANU.

Anamtaja Dr. Vedasto Kyaruzi na mapinduzi ya TAA ya 1950.

Historia hii ni mimi ndiyo niliyoitafiti na kuiandika katika kitabu cha Abdul Sykes
(1998).

Historia hii haikuwa inajulikana.

Judith Listowel (1965) kamtaja Dr. Kyaruzi lakini hakuwa anajua aliingia vipi
katika uongozi wa TAA.

Yericko anaeleza historia ya Dr. Kyaruzi baada ya kumsikia kwangu na anaacha
taarifa muhimu kuwa Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi waliingia katika uongozi kwa
juhudi kubwa ya Abdillah Schneider Plantan ambae Abdul ni baba yake katika
ukoo na jamii ya Wazulu waliokuwa Dar es Salaam na hawa akina Plantan walikuwa
ndiyo walioshika uongozi wa TAA miaka ile.

Hii historia ya African Association isingekuja kujulikana kama si kwa Kleist Sykes
mwenyewe kuandika historia ya maisha yake kabla hajafariki mwaka wa 1947.

Mswada huu ulihifadhiwa bila kuchapwa hadi kumfikia mjukuu wake Daisy na yeye
akauwakilisha kwa John Iliffe na Iliffe akauchapa katika kitabu (1973).

Nilichokuja kufanya mimi ni kuwa nilikwenda mbele zaidi na kutafiti maisha ya
viongozi wengine wa TAA waliokuwa na Kleist na waliokuja baada yake na hapa
ndipo nilipovumbua Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambayo Kleist na wenzake
kama Ali Jumbe Kiro waliasisi 1933.

Katika huu uongozi ndani ya TAA baada ya kifo cha Kleist ndipo sasa unawapata
vijana kama Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na Dr. Kyaruzi, Dr. Luciano
Tsere, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Michael Lugazia
na Dr. Wilbard
Mwanjisi
na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya walioingia katika uongozi wa TAA
1950 kama Mufti Sheikh Hassan bin Amir na Sheikh Said Chaurembo.

Kubwa katika utafiti huu ni kuwa ukimtoa John Iliffe mimi ndiye mtafiti pekee ambae
amefunguliwa nyaraka za akina Sykes na nimesoma kila jalada kuanzia ukurasa wa
kwanza hadi wa mwisho na matokeo yake kikawa kitabu cha Maisha ya Abdul Sykes
na historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ilikuja kushtua wengi ndani na
nje ya Tanzania.
 
Wewe ni mfuasi wa Mohammed Said binafsi au kazi yake uliyoisoma?

Hebu nitajie kitabu kimoja ama viwili vya Mohammed Said ulivyovisoma na kuvielewa kisha namimi nikueleze nilivyoelewa.

Karibu.
Mimi mfuasi wa kazi za Mohamed Said mm ni mfuasi wa kazi za kijana mwezangu Yericko Nyerere naweza kusema mm binafsi ni mpenzi kusoma vitabu ndio maana nina imani mmoja kati watu mwanzo kununua kazi ndugu yngu Yericko lkn atuwezi kkubari umungu mtu kwenye maandishi lazima tukubari kukoselewa ss Yericko ilo alitaki naona kile kile tunachokipinga mm na yy khs serikali hii kumbe kwake pia kipo
290baf969eb1810aabeddf9f86300a7d.jpg
ndugu yngu akiniuzia kitabu chake
 
Mhhh....

Mzee, naomba niweke wazi tu kuwa binafsi sijawahi kukisoma kitabu cha Ndugu yangu Yericko Nyerere zaidi ya Makala zake na nafikiri alikuwa bado hajakamilisha kitabu hasaa.

Naomba niishie hapa kwa kusema kuwa nitamsoma zaidi kadri nitakapopata muda.
Azarel,
Baada ya kuona uandishi wake kama nilivyokuonyesha umekaa kimya
kuhusu makosa yake katika uandishi kama nilivyoonyesha.

Yericko anasema kwa uandishi ule Dr. Ponera anataka apewe shahada
ya uzamivu na Yericko kaweka na ''audio'' tusikilize ushauri wa Dr. Ponera.
 
Nakuuliza na wewe...!

Je ulianza kumsoma Mohammed Said lini?

Umeshasoma na kuelewa vitabu vyake vipi japo viwili?
a3d208b4b46c716fac9a0bbc6626749c.jpg
na cha uhamuzi wa busara kutoka tabora kwa hlk ni hivyo viwili bila kuacha machapisho yke kwenye blog yke kila siku unaweza kuingia pia www.mohamedsaid.com hakika utapata faida kubwa...
 
kuna makosa ya kisarufi au lugha kwa ujumla nashukuru umeyaanisha. hili linatokea na hata kwenye maandiko mengine makubwa kabisa ya watu wenye ilimu kubwa duniani kuna makosa ya kuchapa n.k hilo nakubaliana nawe. kwenye kukosoa tutakosoa. lakini je hili peke yake linaweza kuondoa kabisa ukweli wa yale aliyoyasema kwenye hiki kitabu?

hebu enenda katika hoja zake mdadavulie hapa kuwa kuna makosa katika hoja moja mbili tatu.. na hizi ukweli wake upo hivi. hii itasaidia zaidi. kama hili linawezekana ni jambo jema. mimi nina tatizo moja kubwa katika kusoma kwangu. husoma ninayo yapenda na nisiyoyapenda. husoma yanayonihusu na yasiyo nihusu. ndo maana naifaham kiasi flani Quran na Biblia pia. Huwa sikubaliani na kila kitu mtu aandikacho au asemacho lakini hujiuliza wapi hayupo sawa ili kuanzia hapo sasa nielimishe wengine.

yericko ameandika facts nyingi kwa vielelezo na si yale maneno ya kwenye vikao vyetu sisi wengine vya kulalamika na kujishtukia. mimi nachukia sana udhaifu... udhaifu wa moyo ni mbaya sana kuliko wa mwili. maana ushupavu wa mwili hutoka moyoni. weka hoja moja moja hapa na Yericko Nyerere kwa kuwa yupo atakujibu kwa kina amenambia kupitia andiko lake kuwa yeye yupo tayari kuelimishana nawe na mwingine yeyote kwa hoja na si vioja. wanaotumia lugha za kuudhi mimi siafikiani nao na nilidhani hata wewe huhitaji kuwaita waje wamshambulie azarel maana si ustaarabu hata kidogo hasa kati umri huu na zama hizi za malumbano ya hoja. hakuna aliye bora zaidi ya mwenzie... watu wapate kuonyana kwa lugha ya upole.
Azarel,
Ukija na lugha kama hizi za matusi utaharibu mjadala kwa kuwa
tutawakaribisha watu hodari kwa matusi kukushinda.

Huu ni mjadala tu hatugombani.
Tuwe waungwana na tuheshimiane.

Kuhusu kusoma nimemsoma vizuri Yericko na ushahidi ni huo
hapo chini.

Nimeweka bold katika hayo aliyoandika ili uone ujuzi wake katika
uandishi.

Hayo ni makosa na sikusahihisha yote aliyoandika hizo ''paragraph,''
nyingine nimeona nikuachie wewe uzionyeshe.

Halikadhalika sikuona haja ya kusahihisha makosa ya ''facts,'' na
makosa mengine kama ''spellings,'' etc. katika hayo aliyoandika
kwani hakika inachekesha na pia inachosha.

Mathalan anasema Mtaa wa Stanley ni Mtaa wa Lumumba...

Nina mengi naweza nikakueleza katika hayo aliyoandika ikiwa
utapenda.

Kwa sasa nasimama hapa.

Tafadhali hebu na wewe soma hayo yaliyomo katika kitabu cha
Yericko hapo chini (''Nenda kasome ewe ndugu Muislam wacha
ngebe mfu).''

Nimesoma ewe ndugu yangu kwani wewe hivi vichekesho hukuviona?:

KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU KAMA ILIVYOANDIKWA NA YERICKO NYERERE
Mohamed Said January 18, 2017 0

.............Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maalumakwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanzaKlest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu CesilMatola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.

Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.

Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.

Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
 
Shamba,
Yericko
anaandika historia za Abdul Sykes na baba yake Kleist katika historia
ya African Association na TANU.

Anamtaja Dr. Vedasto Kyaruzi na mapinduzi ya TAA ya 1950.

Historia hii ni mimi ndiyo niliyoitafiti na kuiandika katika kitabu cha Abdul Sykes
(1998).

Historia hii haikuwa inajulikana.

Judith Listowel (1965) kamtaja Dr. Kyaruzi lakini hakuwa anajua aliingia vipi
katika uongozi wa TAA.

Yericko anaeleza historia ya Dr. Kyaruzi baada ya kumsikia kwangu na anaacha
taarifa muhimu kuwa Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi waliingia katika uongozi kwa
juhudi kubwa ya Abdillah Schneider Plantan ambae Abdul ni baba yake katika
ukoo na jamii ya Wazulu waliokuwa Dar es Salaam na hawa akina Plantan walikuwa
ndiyo walioshika uongozi wa TAA miaka ile.

Hii historia ya African Association isingekuja kujulikana kama si kwa Kleist Sykes
mwenyewe kuandika historia ya maisha yake kabla hajafariki mwaka wa 1947.

Mswada huu ulihifadhiwa bila kuchapwa hadi kumfikia mjukuu wake Daisy na yeye
akauwakilisha kwa John Iliffe na Iliffe akauchapa katika kitabu (1973).

Nilichokuja kufanya mimi ni kuwa nilikwenda mbele zaidi na kutafiti maisha ya
viongozi wengine wa TAA waliokuwa na Kleist na waliokuja baada yake na hapa
ndipo nilipovumbua Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ambayo Kleist na wenzake
kama Ali Jumbe Kiro waliasisi 1933.

Katika huu uongozi ndani ya TAA baada ya kifo cha Kleist ndipo sasa unawapata
vijana kama Abdul Sykes, Hamza Mwapachu na Dr. Kyaruzi, Dr. Luciano
Tsere, Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Michael Lugazia
na Dr. Wilbard
Mwanjisi
na viongozi wa Al Jamiatul Islamiyya walioingia katika uongozi wa TAA
1950 kama Mufti Sheikh Hassan bin Amir na Sheikh Said Chaurembo.

Kubwa katika utafiti huu ni kuwa ukimtoa John Iliffe mimi ndiye mtafiti pekee ambae
amefunguliwa nyaraka za akina Sykes na nimesoma kila jalada kuanzia ukurasa wa
kwanza hadi wa mwisho na matokeo yake kikawa kitabu cha Maisha ya Abdul Sykes
na historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ambayo ilikuja kushtua wengi ndani na
nje ya Tanzania.
Hongera sana ulifanya kazi kubwa sana
 
Gu Dume,
Mimi sina tatizo na kitabu cha Yericko.
Nimemjibu Yericko baada ya kunitaja katika historia ya uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi ya Zanzibar na nimeeleza yale ninayoyajua na nyote mmeona.

Watakaokihukumu kitabu chake ni wasomaji.

Kama kuna watu wataamini kuwa Dar es Salaam alikuwapo Sheikh Issa Amiri mimi ninasema kuwa hajapatakuwapo sheikh mwenye jina hilo si Dar es Salaam wala katika historia ya AA na TANU.

Kama Yericko atasema kuwa Kanisa liliunda TANU mimi sina ugomvi na hilo kwani historia ya TANU ilipatapo kuandikwa na Chuo Cha Kivukoni 1981 na hao wenye TANU yao akina Tatu bint Mzee, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faiz Mafungo, Sharifa bint Mzee, Halima Selengia, Idd Tosiri hata makachero wa Special Branch akina Ali Mwinyi Tambwe hawakuwemo kwenye kitabu chao.

Hakuna la ajabu ikiwa itakuja historia ya TANU ya Kanisa iliyoandikwa na Yericko Nyerere.
 
Nyongeza
Tatizo katika historia hii ni kuwa kuna waliokuja kuona kuwa kuundwa kwa TANU was, ''the ultimate prize,'' na huyu ambae atalivaa taji lile jina lake halitosahaulika katika historia ya Tanganyika. Hii ndiyo sababu hata Chuo Cha Kivukoni kilipokuja kuandika historia ya TANU jina la Abdul Sykes likaondolewa. Vipi utaondoa jina la Abdul wakati hiyo mikutano ya siri ya kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwake? Mfano mwingine ni kuwa wanachama wote wa mwanzo kama Dossa, Said Chamwenyewe, Idd Faiz Mafungo, Idd Tosiri, Tatu bint Mzee, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Haidar Mwinyimvua kuwataja wachache na hawa wana mengi walifanya katika kujenga chama, hawamo katika kitabu kile.

Kushoto: Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya,
Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu,
Dodoma 1955.

Kushoto kwa Mwalimu Julius Nyerere ni Sheikh Suleiman Takadir
Clement Mohamed Mtamila, Titi Mohamed na nyuma kulia ni John
Rupia, Rajab Diwani na Mama Maria Nyerere.

Mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London) lilipochapa makala yangu, "In Praise of Ancestors," gazeti liliondolewa kwenye ''circulation,'' kwa kuwa nilieleza historia ya Abdul Sykes katika kuunda TANU na mchango wa Al Jamiatul Islamiyya katika kutoa viongozi wa mwanzo na wanachama wa TANU.

Ukimleta Abdul katika historia ya TANU lazima umlete na baba yake na wadogo zake wote kisha lazima umlete Hamza Mwapachu na watu wengine kama Earle Seaton na Chief Kidaha Makwaia na lile jopo la masheikh wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Amir na utake usitake lazima urudi nyuma 1929 kwenye historia ya African Association na historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hamza Kibwana Mwapachu

Katika historia hii utasema kuwa hata hilo jengo ilipoundwa TANU hiyo nyumba ilijengwa na baba yake Abdul kati ya 1929 na 1933 na Abdul akiwa mtoto wa miaka 5 baba yake alikuwa kila Jumapili akimchukua pale New Streets kuangalia ujenzi ule.
 
Yericko nilikuwa sijui ww nawe km ni mpuuzi kiasi hicho uwezi hata siku moja mtu mwenyewe umri zaidi ya baba yko ukamwita mnafiki na ana gubu naweza kusema watu wa bara wote fikra zenu na wazo yenu ni sawa sioni tofauti ya kauli zako na jmp pamoja bashite kumbe wote baba moja mama moja sijawai kkufikiria kuwa mkosefu wa adabu kiasi hicho mzee kaleta hoja jibu hoja ebu niambie kuna tofauti hapo na walio jaribu kujibu hoja za lisu kwa risasi badilika bila hivyo utofika mbali ww bado kijana mdogo sna...
Hapo sasa watukosea heshima ... kwamba watu wote wa bara akili zetu zafanana ... ina maana kama pana asiejitambua so wote hatujitambui pia ... That's NOT FAIR
 
Naomba radhi kwa ilo lkn mtakuwa na kitu kimoja ambacho wote mpo sawa naomba niseme wengi wenu ni wajuaji alichofanya Mdogo wngu Yericko sioni tofauti na anayopiga kila siku kwa jpm bashite nk...
 
Azarel,
Ukija na lugha kama hizi za matusi utaharibu mjadala kwa kuwa
tutawakaribisha watu hodari kwa matusi kukushinda.

Huu ni mjadala tu hatugombani.
Tuwe waungwana na tuheshimiane.

Kuhusu kusoma nimemsoma vizuri Yericko na ushahidi ni huo
hapo chini.

Nimeweka bold katika hayo aliyoandika ili uone ujuzi wake katika
uandishi.

Hayo ni makosa na sikusahihisha yote aliyoandika hizo ''paragraph,''
nyingine nimeona nikuachie wewe uzionyeshe.

Halikadhalika sikuona haja ya kusahihisha makosa ya ''facts,'' na
makosa mengine kama ''spellings,'' etc. katika hayo aliyoandika
kwani hakika inachekesha na pia inachosha.

Mathalan anasema Mtaa wa Stanley ni Mtaa wa Lumumba...

Nina mengi naweza nikakueleza katika hayo aliyoandika ikiwa
utapenda.

Kwa sasa nasimama hapa.

Tafadhali hebu na wewe soma hayo yaliyomo katika kitabu cha
Yericko hapo chini (''Nenda kasome ewe ndugu Muislam wacha
ngebe mfu).''

Nimesoma ewe ndugu yangu kwani wewe hivi vichekesho hukuviona?:

KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU KAMA ILIVYOANDIKWA NA YERICKO NYERERE
Mohamed Said January 18, 2017 0

.............Jukumu la kuandaa nchi hizo kupata uhuru liliratibiwa na shirika hilo la kijasusi kwa ustadi mkubwa bila baadhi ya makoloni kujua, lakini lilikumbana na kikinza hasa kufuatia mnyumbuliko wa kiimani ndani ya ukristu kufuatia nguvu ya Cambrige (Anglikana), mgogoro huo ulikuzwa kwakuwa Anglikana nao tayari walikuwa wameaandaa taasisi yao waliyoiita Fabian Sociaty maalumu kwaajili ya kuwaandaa vijana wa kiafrika kukabidhiwa nchi zao, Barani Afrika Jeisuiti ilibadili mbinu kwakuwa dola la Kiingereza lilikuwa kikwazo kwa sehemu fulani, haikujikita kwenye dola isipokuwa ilisimama katika muundo wa shirika lifanya shughuli zake ndani ya Kanisa. Dhamiri ilikuwa lazima itimie, kama ilivyosemwna huko mwanzo kuwa hawa ndio wabobevu wa elimu ya juu kwa kila nyanja na ndio wanaotawala ulimwengu, hivyo vikwazo havikukwamisha wao kufikia malengo.

Katika Tanganyika chini ya Udhamini wa Jumuiko la Kimataifa, kulikuwa na harakati za hapa na pale za kudai haki za kiraia kwa wenyeji. Ifahamike kuwa vyama vya harakati hizo Tanganyika vilikuwa vingi sana, na vipo vilivyokuwa vikipingana vyenyewe kwa vyenyewe.

Mwaka 1927 hadi 1929 kanisa Katoliki nchini chini Joseph Gabriel Zelger, lilibainika kuingiza siasa katika utendaji kazi zake, kitendo hiki kiliwakwaza wakuu wa mamlaka ya kikoloni na kupelekea majasusi wakikoloni wapendekeze aachishwe uongozi wa kanisa nchini. Ni kweli tarehe 12 februari 1929 Zelger alistaafu wadhifawake kwa lazima. Ni mwaka huohuo wa 1927 ndio Chama cha African Assosiotion (AA) kilianzishwa na Gavana Sir David Cameron maalumakwaajili ya kuratibu sherehe za watu weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanzaKlest Sykes (Mzulu Baba yake alikuwa mateka wa kikoloni toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).

Hao ndio mwaka 1927 waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu. (Chama cha walevi kwa lugha nyingine). Mwaka 1933 Mwalimu CesilMatola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948 yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwahid Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia huko Burma, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani, mapinduzi yaliyoitwa “ondoa wazee”. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA, Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi (Mhaya), huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwahid Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina la chama na kuwa TANU jina ambalo lilibuniwa na Abdulwahid Sykes, TANU ilikwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM baada ya Muungano wa ASP na TANU.

Kisa hiki cha kufukuzwa kwa Kasisi huyu Bw. Zelger kinasema, Kanisa lilianzisha mafundisho yenye kuchochea fikra za kimaasi, nalilifanikiwa kuandaa wakufunzi maalumu kwenda katika majimbo yote ya kihuduma Tanganyika, hilo lilipelekea kuleta mtafaruku na dola ya mkoloni wa kiingereza ambapo ilimgharimu kiongozi huyu wa kiroho kuachia madaraka yake. Alipoingia askofu Edger Aristide Maranta mwaka 1930, ikiwa kama vile mwendelezo wa mtangulizi wake, Askofu Maranda alianzisha harakati za kuwashawishi viongozi wengine wa majimbo kuendeleza kutoa mafundisho yenye kumfanya mtanganyika ajitambue na adai uhuru wake, mfano, 23 mei 1938 wakati makanisa saba ya Kilutheri yakiwa kwenye hatua za mwanzo za mchakato wa kuungana, Askofu maranda aliomba kuhudhuria kikao cha tarehe 8 mwezi wa sita kilichofanyika Mjini Arusha, Askofu Maranda aliudokeza mpango ule wa siri wa katoliki katika kikao hicho, japokuwa kulikuwa na hofu ya kutoaminiana, lakini uthabiti wa malengo hayo ulijipembua baadae na kuwa wamafaa, ushahidi wa nyaraka za kumbukumbu za mkutano huo unaeleza.

Juhudi za kanisa kupigania mkataba wa Versailles ziliendelea kushika kasi huku zikiendeshwa kwa siri sana kwamfumo wa neno la kiroho, na ilipofikia miaka ya 1950+ kanisa sasa lilikuwa tayari linanguvu ya ushawishi kufuatia mafanikio ya harakati za kanisa katika nyanja za ukombozi barani afrika. Wakati hayo yakiendelea tayari kanisa kupitia shirika lake la kijasusi lilikuwa limewekeza kwa nguvu kubwa kumtafuta mtu imara mwenye weledi na vipawa atakayejengwa ili aje kuongoza nchi. Mtihani mkubwa kwa kanisa ilikuwa ni namna gani linaweza kuingia rasmi kudai uhuru wa Tanganyika. Katika kipindi hiki tangu harakati za kanisa zianze, Askofu Maranta pamoja na mapadre wa baadhi ya mikoa, walikuwa tayari ameshafanya juhudi kadhaa za kukutana na Mashehe waliokuwa na ushawishi mkubwa, mfano 05/02/1948, Askofu Maranda alikutana Shehe Issa bin Amir kiongozi wa kiroho katika msikiti wa Ilala - mchikichini.

Shehe Issa Bin Amir alizaliwa 1846 katika viunga vya Mzizima, mchikichini na kuhudumu katika wadhifa wa shekhe katika msikiti uliokuwa hapohapo viwanja vya nyumbani kwake na alifariki mwaka 1953 akiwa na umri 107, Shehe Issa Bin Amir kwa kabila alikuwa Mzaramo na akiishi hadi kifo chake Mchikichini pale nyuma ya kilipo kiwanda cha bia leo (TBL). Shehe Issa Bin Amir rafiki kipenzi wa Padre Maranta na mzee wa hekima za kilele cha zama hizo, mtu aliyekuwa kiungo muhimu kati ya uislamu na ukristu, Mtu ambae Mwalimu Cesil Matola rais wa kwanza wa AA na Klest Sykes katibu mkuu wakwanza wa AA, na wanachama wengine waliokuwa AA walimheshimu sana kwa hekima zake na mmoja wa wasisi wa Jumuiko la Uislamu Afrika Mashariki (EAMWS) Mazungumzo yao yalihusu harakati za ukombozi, Shehe Issa alimshauri Askofu kuwa ikiwa makanisa na misikiti yanapigwa marufuku na mkoloni kujihusisha na siasa za ukombozi basi watafute baadhi ya vyama vya harakati za ukombozi na waviunge mkono, wazo hilo lilimvutia Askofu lakini akajenga hofu kama je ndani ya vyama hivyo watapata vijana wasomi?.

Siku chache baada ya makutano yake na Shehe Issa, Askofu Maranta aliletewa mapendekezo kutoka kwa Attilio Beltramino kasisi wa katoliki aliyehudumu kule Iringa, mapendekezo ya kasisi huyu yalikuwa ni, Umishonari makao makuu uruhusu udurufu wa biblia zisomeke kwa makabila ya wahusika wa eneo, ndani ya biblia hizo yaongezwe mafundisho ya haki ya kujitambua na kujitawala wenyewe. Pendekezo hili lilimvutia sana Maranta hivyo akalipa baraka zake, kwa hakika lilifanikiwa na ndio lilizaa hisia kali za mwamko wa kudai uhuru, mfano biblia ya lugha ya kihehe ilikuwa inaeleza wazi athari za kutawaliwa.

Harakati za Ukombozi za Mwalimu Nyerere akiwa na nguvu mpya ya kifikra toka Chuo kikuu, zililivutia kanisa na uungaji mkono ukachagizwa, mfano mwaka 1953 wakati TAA kikiwa chama chenye nguvu kufuatia mabadiliko ya 1948 toka AA kwenda TAA. Askofu Maranta alimwalika ofisini kwake Mwalimu Nyerere, walizungumza mengi lakini kubwa nikuwa alimsifu kwa juhudi za kujipambanua bila kuwaogopa wakoloni, akamweleza jinsi kanisa linavyounga mkono juhudi za ukombozi wa Tanganyika, kisha akamshauri kuwa ajaribu kuvishawishi baadhi ya vyama vya harakati za kiraia viungane ili kuvipa nguvu ya kudai uhuru na kanisa litasaidia.

Wazo la Askofu Maranta lilimkaa Mwalimu Nyerere na mwaka 1954, alianza juhudi za kuwaunganisha vijana wenzake wa kariakoo ambao walikuwa ndani ya TAA na wenye nguvu ya ushawishi lakini wakikabiliwa na matatizo makubwa mawili katika lengo lao ambayo ni Elimu na Woga. Ikumbukwe kuwa mwaka 1953 baada ya harakati za ukombozi kupamba moto na kamata kamata ya wanaukombozi, Askofu Edger Aristide Maranta alihamishiwa Zanzibar na nafasi yake ikachukuliwa na Vicar Apostolic, lakini bado aliendelea kuwa mshauri imara wa Mwalimu Nyerere. Jambo la kushangaza kama si kufurahisha, mwaka huohuo mwezi wa 8, Edger Aristide Maranta alirudishwa tena Dar es Saalam, na sasa mbinyo dhidi ya ukoloni ukashika mkondo wake.

Mnamo tarehe 07/07/1954, Vijana (wazee wa kariakoo) wakiongozwa na Julius Kambarage Nyerere, walikubaliana wazo la kuhuisha chama kutoka TAA kwenda TANU, chini ya uratibu wa karibu wa Wajeisut (Askofu Maranta) na Waislamu (Shehe Issa bin Amir) ijapokuwa alikuwa amefariki mwaka mmoja nyuma, lakini hekima za Shehe huyu zilisaidia. Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,

Si hivyo tu bali katika moja ya utani wa Mwalimu wenye ukweli ndani yake aliwahi kusema kuwa makasisi Walsh na Art Wille wa Shirika la Maryknoll ni maboss wake, akikumbuka malipo ya shilingi 600 angali ameacha kazi ya ualimu akiwa kijijini Butiama.Kuna ushahidi wa kihistoria pia unaochagiza habari hizi kwamba majasusi wa Kanisa walimuandaa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuja kuwa kiongoza Tanganyika mpya................

Kutoka kwenye kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.
Mzee Said, unachukua post za mitandaoni tena za hapahapa jf ambazo ni miswada tu kisha unasema ndio umesima kitabu?

Acha utoto ndugu.....unajiita msomi, basi enenda kisomi....

Unachokileta humu sio kitabu ni makala tu ambazo hazikuhaririwa kuwa kitabu....
 
Naomba radhi kwa ilo lkn mtakuwa na kitu kimoja ambacho wote mpo sawa naomba niseme wengi wenu ni wajuaji alichofanya Mdogo wngu Yericko sioni tofauti na anayopiga kila siku kwa jpm bashite nk...
Dhana iloenea sana kwamba wanawake wa Kimachame wanaua waume zao haiwezi kuchukuliwa kuwa ni KWELI kuwa jambo hilo latendwa na wanawake WOTE wa Kimachame ... hiyo yaeza kuwa SILIKA ya BAADHI yao ... naamini nitakuwa nimeeleweka vyema ...

Kwa hao ulowataja ... naomba huko nisitoe contribution yoyote ... ubaki na uendelee kuwa mtazamo wako ...
 
Lkn walikuwa na Asili hiyo lazima pia tukubariane kwa ilo...
 
Back
Top Bottom