BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Chuo cha Uhasibu Arusha kimethibitisha tukio la Askari wa SUMA JKT kumshambulia mwanafunzi wa chuo hicho baada ya kujibizana kwa madai ya kutokuwa na Kitambulisho.
Askari huyo amesimamishwa kazi huku Uongozi wa Chuo ukiagiza achukuliwe hatua zaidi za kiutendaji na kijinai, pia, Mwajiri wake (SUMA JKT) agharamie matibabu ya mwathirika pamoja na kuomba radhi kwa kitendo hicho.
Askari wa SUMA JKT wamekuwa wakilalamikiwa kwa kujichukulia Sheria mkononi na kuwashambulia watu mbalimbali katika maeneo wanayotoa huduma za ulinzi.
=========================
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kinapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kupigwa na Askari wa SUMA JKT katika eneo la Chuo siku ya Jumanne tarehe 22/11/2022.
Uongozi wa Chuo kwa masikitiko makubwa unakiri kutokea kwa tukio hilo katika Kampasi yetu kuu ya Arusha na umelaani kitendo hicho kilichotokea baada ya majibizano kati ya Askari wa SUMA JKT na mwanafunzi ambayo yalipelekea kitendo hicho.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo Uongozi wa Chuo umekutana na Uongozi wa SUMA JKT na kukubaliana kuchukua hatua zifuatazo:-
i) Askari husika amesimamishwa kazi mara moja mara baada ya tukio hilo
ii) Askari husika achukuliwe hatua za kisheria (kiutendaji na kijinai) juu yake
iii) SUMA JKT kufidia gharama za matibabu pamoja na kutoa fidia ya fedha kwa mwanafunzi husika
iv) SUMA JKT wameahidi kutoa tamko la kuomba radhi kwa kitendo kilichotokea cha Askari wake kukiuka taratibu za kiutendaji
Tunasikitika sana kwa kitendo hiki na tunaahidi kuhakikisha haya hayajitokezi tena ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya mahusiano mazuri katika jamii yetu.