Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaoa Kifua?mbona kifuani yuko 'flati'
Haiwezi kuwa ya msingi kwa sababu zifuatazo majeshi yote yanahitaji askari wenye nidhamu. Kuna waliotoka JKT wakajiunga na makampuni mengine ya ulinzi wanafanya vizuri na hawana shina. Shida iko kwa hawa waliobaki na Tag ya JKT, wanajiona SEAL, KGB au Mosad. Wakubwa wao wawafundishe namna gani cooperate security ina operate. Tofauti na hapo watabaki kungángánia malindo machache kwenye taasisi za serikali. Suma JKT SIYO JESHI ni kampuni kama ilivyo kamopuni yeyote ya ulinzi, ndio maana kuanzia uniform wanafanana na kampuni zingine zooteHii ni point ya msingi sana ila wasioelewa hawawezi kukuelewa,
nitakujibu kesho, asubuhi na mapemaUkuje hapa nikubamize ngumi ya jicho ili ujue ilivyokuwa.
Na Pale NIT Hadi wakabadilishwaSuma jkt uwa wanachukua sheria mikononi nakumbuka ukatili waliokuwa wakifanya IFM.
Suma jkt uwa wanachukua sheria mikononi nakumbuka ukatili waliokuwa wakifanya IFM.
Ni hatari sana kuwatumia hawa askari kwenye ulinzi wa mageti kwenye sehemu ambazo wanakutana na watu wa kawaida.
Wanapaswa kuajiriwa na Polisi kulinda mabank na si kukaa mapokezi.
Wanapaswa kulinda sensitive areas usiku na si kuwa sehemu ya mapokezi.
Chuo cha Uhasibu Arusha kimethibitisha tukio la Askari wa SUMA JKT kumshambulia mwanafunzi wa chuo hicho baada ya kujibizana kwa madai ya kutokuwa na Kitambulisho.
Askari huyo amesimamishwa kazi huku Uongozi wa Chuo ukiagiza achukuliwe hatua zaidi za kiutendaji na kijinai, pia, Mwajiri wake (SUMA JKT) agharamie matibabu ya mwathirika pamoja na kuomba radhi kwa kitendo hicho.
Askari wa SUMA JKT wamekuwa wakilalamikiwa kwa kujichukulia Sheria mkononi na kuwashambulia watu mbalimbali katika maeneo wanayotoa huduma za ulinzi.
=========================
Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) kinapenda kutoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mmoja wa wanafunzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kupigwa na Askari wa SUMA JKT katika eneo la Chuo siku ya Jumanne tarehe 22/11/2022.
Uongozi wa Chuo kwa masikitiko makubwa unakiri kutokea kwa tukio hilo katika Kampasi yetu kuu ya Arusha na umelaani kitendo hicho kilichotokea baada ya majibizano kati ya Askari wa SUMA JKT na mwanafunzi ambayo yalipelekea kitendo hicho.
Baada ya kutokea kwa tukio hilo Uongozi wa Chuo umekutana na Uongozi wa SUMA JKT na kukubaliana kuchukua hatua zifuatazo:-
i) Askari husika amesimamishwa kazi mara moja mara baada ya tukio hilo
ii) Askari husika achukuliwe hatua za kisheria (kiutendaji na kijinai) juu yake
iii) SUMA JKT kufidia gharama za matibabu pamoja na kutoa fidia ya fedha kwa mwanafunzi husika
iv) SUMA JKT wameahidi kutoa tamko la kuomba radhi kwa kitendo kilichotokea cha Askari wake kukiuka taratibu za kiutendaji
Tunasikitika sana kwa kitendo hiki na tunaahidi kuhakikisha haya hayajitokezi tena ikiwa ni pamoja na kuendelea kutoa elimu ya mahusiano mazuri katika jamii yetu.
Bro wewe ndo upo vizuri kwenye kureason sasa mimi nimemaliza hapo IAA 2021, Nipo hapo tangu 2016 na hao suma jkt wameletwa hapo chuo kuanzia 2019 navyokumbuka na hakuna tukio lolote limewahi kutokea na wanafunzi wanafuata sheria zote kama code za mavazi kama vile wasichana hawaruhusiwi kuvaa suruali za kubana sana na kuingia getini ni mpaka uonyeshe ID mageti yote kubwa na dogo sema uyo dogo atakuwa kuna maneno kamtupia mlinzi sio mazuri ndo maana kakandwa japo harusiwi kumkanda mtu, mbona watu kibao uwa wanapita hapo getini na sometimes wanakuwa wamesahau ID sema wakifika wanajishusha kwa mlinzi na kwa polite language wanabonga naye wanapita , uyo demu sio student wa kwanza kusahau ID tangu chuo kianzishe huo utaratibu , iweje yeye ndo apokee kipigo, reasoning capacity ya wabongo ndogo sana uwa tunapokea vitu kwa mihemko bila kutuliza akili na kuprove/ judge both side,Naona wote mmeegemea kwenye kumshambulia askari wa SUMA JKT.......kiuhalisia nidhamu na kuheshimiana ni jambo la msingi sana kwenye maisha yetu ya kila Siku hasa sehemu za kazi au jamii zetu..... nidhamu na heshima inatakiwa itoke pande zote mbili ili kuleta msawazo na huku kila mmoja akitimiza wajibu wake kulingana na nafasi yake.........
Mabinti au wanachuo wengi huwa wanatabia za ujeuri, kejeli na dharau dhidi ya watu wengine wanaowaona wa kawaida kwao......wao kuanza masomo ya chuo wanaona wapo kwenye ulimwengu mwingine kabisa......Kwa kweli unahitaji busara na kiwango kikubwa cha ustahimilivu na uvumilivu ku deal na hao watoto wanaosoma vyuo.......
Kimsingi hao maaskari ni waajiriwa au wapo kwenye hizo taasisi kutoa huduma za ulinzi na usalama.....wanafanya kazi Kwa kufuata sera na miongozo ya taasisi husika kuhusu usalama na amani kwenye sehemu husika au taasisi husika.......bila shaka hata hao wanachuo kabla ya kujiunga na chuo na wao pia hupewa miongozo hiyo..........
Inawezekana askari alimkumbusha Binti jambo la kawaida kuhusu protocol za taasisi hiyo na pengine kwenye kurushiana maneno yule Binti akatoa lugha mbaya na mlinzi naye ni binadamu uvumilivu ukamshinda.........