Dogo GSM
Member
- Jul 31, 2021
- 65
- 91
Wakuu nchi imekuwa ngumu hii nahisi kila mtu amevurugwa, imetokea jana asubuhi kuna jamaa anasemekana ni mjeda amepewa kichapo na vijana hao wenye hasira kali.
Chanzo ni baada ya bodaboda kumpeleka mjeda huyo kazini..inasemwa mjeda huyo alifika kijiweni juzi asubuhi na kumchukua boda mmoja ampeleke kambini ila walipokaribia mjeda huyo alihamaki na kumtaka boda amshushe kwa kuwa anaendesha hivyo hivyo hatoi hela na akiendelea kumfwata atamuitia wenzie.
Basi jana mjeda huyo alionekana maeneo ya kijiweni ndipo boda wakamuamuru alipe hela ya kusafirishwa na riba juu ndipo akagoma basi vijana wakaanza kumshambulia lakini kwa bahati nzuri polisi walikuwa doria ndipo wakawahi kumuokoa na kumtoa katika tukio haraka sana.