DOKEZO Askari Polisi atuhumiwa kumuua raia Arusha kwa kumpiga risasi 3, Wananchi wamtuhumu kwa mauaji ya mara kwa mara

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Wafugaji nao huwa wanajiamini sana, hapa kwenye taarifa wafugaji wameua mtu na wanawapiga wakulima, mleta taarifa haja balance taarifa yake nazani ni mihemko yake.
 
Ni wakorofi sana wafugaji
 
Kwenye tukio la kwanza aliingilia kuzuia asiuawe kwa sababu gani? Huyo diwani ana mashtaka ya kujibu.
 
Mtamlaumu askari bure .hamjui ujinga na ujeuri wa wafugaji kwa wakulima.....jamaa kama huna mguu kiunoni wanalisha wanasema asa ngombe ife njaa..?? Ni kuwapasua vichwa..uko lendebesi wanakula za kichwa tu na ujeuri wao...
 
Wewe mwenye master utakubali kukaa lindo ? Kuzunguka boda faster mtaani kama huko Goba alikosema mpoki kuna hadi fisi wanatembea kama mbuzi usiku?
why not kama mshahara upo vizuri?
 
Huo ni Mgogoro wa Wafugaji na Wakulima.Sasa wewe unalisha mifugo kwenye Shamba lake alafu unataka kumuua kwa kumchoma Mkuki anapokuambia toa mifugo unategemea yeye akuache wakati anacho Mguu wa kuku .Acheni kulisha mifugo kwenye mashamba ya Watu kibabe kuna jamii zingine zimevurugwa hasa mbayazaid anayo taaluma ya kijeshi.Hapo hata mahakamani anashinda kesi mapema sana maana sababu ya kumiliki silaha ni kujilinda mwenyewe na Mali zake na kweli kajiinda yeye na mali zake.Mimi nafikiri baldili Tittle ya post maana wala kazi yake hapo haihusiki .Poleni wafiwa maana kuondokewa na ndugu inauma ila hapo ni kosa la Marehemu hata mimi Raia ningetumia chuma tu siwezi kufa kizembe .
 
if it's impossible, ujinga na upumbavu kama huo hauwezi kuisha as you expect.
Suala la utashi sio lazima uende shule,kuna watu wamesoma lakini kichwa kimejaa matope.
Fikiria 2005 ditopile mzuzuri alivyompiga risasi dereva wa daladala !!ina maana ditopile ni form iv failure?
 
Kwanini wananchi wasijitetee wakamdedisha lau kwatumia ujumbe wauaji wenzake? Hili nalo linahitaji wafadhili kweli? Jicho kwa jicho, jino kwa jino na mtama kwa mtama, kifo kwa kifo.
 
Mshahara wawapi huo wangekuwa kila siku wanakaba mpaka elfu 2?
Hujanielewa na sizani kama utanielewa,, unaweza kuniambia kwanini Tanzania inaruhusu failures wa form 4 ndo wajiunge na upolisi?
 
Kwanini wananchi wasijitetee wakamdedisha lau kwatumia ujumbe wauaji wenzake? Hili nalo linahitaji wafadhili kweli? Jicho kwa jicho, jino kwa jino na mtama kwa mtama, kifo kwa kifo.
Wewewe Huwajui Mipolisi ya Arusha chalii yangu yaani haikawizagi kutumia cha moto Utafikiri Mapolisi ya South Africa. kwanza hayanaga time ya kujadili na Mhalifu mbabe
 
Hujanielewa na sizani kama utanielewa,, unaweza kuniambia kwanini Tanzania inaruhusu failures wa form 4 ndo wajiunge na upolisi?
Taarifa yako ya uongo mbona na imejaa ushabiki tu
Hawa hapa waliojiunga mwaka huu nani kafeli hapo

Hao waliokuwa awamu ya pili

Sasa angalia tovuti yao awamu ya kwanza walikwenda wakina nani
Hawa hapa na ujiulize ulitakamsomi yupi aende Polisi na hayupo huko.

Acha ushabiki maandazi kwakuwa unachuki nao

 
Sawa polisi.
 
Sawa polisi.
Mwenyewe umeona umefikiri kweli kweli hapo. Kwa ufupi sipendi kuona unapotosha jamii wakati ukweli unajulikana wazi ndugu na jamaa zetu wakiwa ni wasomi wanaomba kazi tunaona .Ila kwakuwa unazo hasira zako au bifu zako na hao Mapolisi basi unawapiga za uso tu huku jamii forum . Sasa rudi kwenye mjadala mkuu jadili kuhusu muaji wa Mfugaji huko Arusha na muulize mtoa mada kuwa aweke story yote asituletee Majungu hapa jamii forum akifikiri ndiyo Mahakama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…