Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Alishaua sana watu pindi ni askari polisi mkoa wa morogoro..sasa damu alizozimwaga zinamlilia.mmsishangae hata akajiua ndio hali iwatokeao ma veterans wa jeshi...huwa wanapata ugonjwa wa kisaikolojia uitwao PTSD (post traumatic stress disorder)...ni ugonjwa wa akili ambapo mtu hushindwa kurejea katika hali ya kawaida mara baada ya kukumbana au kushuhudia matukio ya kutisha (kama umwagaji damu,mauaji n.k).Huyu askari mstaafu Kimaro a.k.a Saba Sita, anafukuzana na kivuli chake cha mauti.
Siyo rahisi kwa mila za kiafrika, kukikaribisha kifo kwa bashasha na kimipango kama huyu Saba Sita anavyofanya.
Msuti yake yamemkaa akilini kisawasawa na hafikirii kitu kingine cha maendeleo.
Huyu Saba Sita asingekuwa na muonekano wa afya, tungesema anaumwa, anatamani kufa.
Hisia zangu ni kwamba huyu Saba Sita kuna kitu kinamsumbua kiskili. Kuna mshali kacheza rafu wakati wa utumishi polisi.
Kuna harufu ya damu inamfukuzia.
Hili swala huwa halipaziwi sana sauti hapa TZ ila lipo na huwaiumba sana maaskari na wanajeshi wastaafu...akili zao huwa hazikai sawa...muda wote huwa na wasiwasi.