Katika hali ya kuzimwa data na umeme Gaza kuna mengi tunayokosa kuyaona.Hata hivyo machache yanayovuja kwa shida inaonesha vita huko ni kali kuliko ule ukali uliotarajiwa na jeshi la IDF.
Mara kadhaa jeshi hilo limeshatangaza kuingia katikati ya Gaza lakini baadae ikaonesha kuwa bado wako pembeni kabisa wakitumia makombora ya kutoka kwenye ndege zao za kisasa.
Katika moja ya vidio zilizotolewa kwa shida na wapiganaji wa Hamas imeonesha kifaru cha Israel kikiripuka baada ya kupigwa na silaha hafifu.
Baada ya hapo mmoja wa waendeshaji kifaru hicho akachomoka kwa nyuma huku akivua magwanda yake na kukimbia akiwaacha waenzake waungue ndani ya kifaru hicho.
Pembeni ya kifaru hicho vipo vyengine kadhaa vilivyotelekezwa baada ya ama kuharibiwa au askari wake kuamua kuviacha tu na kukimbia.
Huamini macho yako kutokana na ukubwa wa jeshi la Israel.
Lakini hapo hamna dalili za vidio game.Kila kitu kinaonesha ni uhalisia kabisa.Angalia michoro ile ya vijana wa mtaani kwenye kuta za hapo anapokimbilia huyo askari.
Israel ,Taifa Teule la Mungu, liliwah kufutika katika Ramani ya Dunia Kisha likarudi.
Taifa hili ninkielelezo Cha Mungu, yaan ukitaka kujua kua Mungu yupo, unaitazama Israel Ile iloandikwa kwenye maandiko matakatifu ndo hiii hii Sasa
Tutawapiga tuu ,no way !!!
Huamini macho yako kutokana na ukubwa wa jeshi la Israel.
Lakini hapo hamna dalili za vidio game.Kila kitu kinaonesha ni uhalisia kabisa.Angalia michoro ile ya vijana wa mtaani kwenye kuta za hapo anapokimbilia huyo askari.
Mtu yupo zake Kasulu, anajiita mwana wa Israel. Mwingine yupo Katavi, ila anaiongelea Hammas utadhani yeye ndio kamanda wao. Akili zenu ziko sawasawa kweli?
Du! Huyo mwanajeshi ni kiboko. Hivi ule mlipuko wa kwanza haukuwa na joto kali kweli? Mana jamaa katoka mbio, kama vile hajapata chochote ndani ya kifaru.
Halafu hivi kitengo cha kifaru si ndio huwa hatari sana mana unakuwa umo ndani, watu wakikuotea wanapanda juu wanarusha bomu humo humo.