Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Dunia imekwenda Kasi Sana lakini huyo Jw bado yupo kizamani. Yawezekana kule kwenye basi waliokuwepo mabosi zaidi yake lakini hawajui na wamenyamaza kimya. Hata hoo trafilki zamani walikuwa hawasalimii kwenye gari lakini siku hizi wanadalimia kwanza abiria ndio wanafanya kazi . Kamkosea sana
 
Ninavyowapenda wanajeshi na mateso ya mazoez wanayopiga,kuwasemasema ivi naweza kukudedisha😠
 
Yani mtu afutwe kazi kisa clip hiyo tu?? Hawajanasana hata vibao?? Hilo no suala la kimaadili litashughulikiwa huko huko ndani kwa ndani. Tena yule askari pia hana nidhamu, jeshini sio ulingo wa kisiasa wa cheo cha chini huwezi kufanyia mambo ya kimfedhehesha wa ngazi ya juu, hasa mbele za watu.
 
Inasemekana polisi ni wasomi kuliko JWTZ.

JWTZ wengi ni mbumbumbu
Mh sio kweli, sio jeshi la siku hizi, labda hao polisi ila jeshi siku hizi wanasoma sana

Yani wanajeshi watanzania wanatumia muda wao kazini kusoma kuliko kupigana vita
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz Afutwe
Mambo ya Kijeshi Huyu Trafic alitakiwa Kuheshimu Mkuu wake ambae ni Mjenda Staff Sergeant....
 
Matendo ya mtu Ndiyo yanaweza kuonesha yeye ni nani?

Don’t judge easily
 
Ilikuwa zamani hiyo mkuu. Polis siku hizi wengi ni degree holders. Lkn jeshini Kuna mijtu imejiunga juzi tu hapa eti kisa ina nguvu za kunyanyua vyuma
Wote wanaanzia JKT..kwa sifa zinazohotajika.
 
Hivi kati ya JWTZ na Polisi kina nani wanafanya kazi kubwa hapa nchini?
Kila moja kazi yake Ni muhimu ktk kujenga nchi hii, hakuna mwenye kazi kubwa kuliko mwingine. JW wasijione wao ni watu muhimu kuliko watanzania wengine
 
Nenda kenya kajifunze jeshi lao wanaishi vip... Wakiingia hata super market tu raia woote wanatoka nnje wakimaliza ndio mnaingia....
Hapana. Haya hayafanyiki Kenya.

Nchi ikiwa chini ya jeshi (utawala wa kidemokrasia ukipinduliwa ndiyo haya maisha hutokea)
 
Mmh! Hapana. Hizi ni kada 2 tofauti. Ukubwa wa JWTZ hauhusiki kwa kazi ya polisi traffic.

Askari wa JWTZ awajibishwe
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Acha kupotosha umma wewe, ajaribu aone kama atatoboa. Au unadhani yeye ndiyo atakuwa wa kwanza kuchomolewa kundini?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja,anaweza asifutwe kazi ila akapewa adhabu nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…