Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Askari wa JWTZ aliyemuita Polisi 'paka' wakati akitimiza majukumu yake afutwe kazi

Dunia imekwenda Kasi Sana lakini huyo Jw bado yupo kizamani. Yawezekana kule kwenye basi waliokuwepo mabosi zaidi yake lakini hawajui na wamenyamaza kimya. Hata hoo trafilki zamani walikuwa hawasalimii kwenye gari lakini siku hizi wanadalimia kwanza abiria ndio wanafanya kazi . Kamkosea sana
 
Ninavyowapenda wanajeshi na mateso ya mazoez wanayopiga,kuwasemasema ivi naweza kukudedisha😠
 
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482212
Yani mtu afutwe kazi kisa clip hiyo tu?? Hawajanasana hata vibao?? Hilo no suala la kimaadili litashughulikiwa huko huko ndani kwa ndani. Tena yule askari pia hana nidhamu, jeshini sio ulingo wa kisiasa wa cheo cha chini huwezi kufanyia mambo ya kimfedhehesha wa ngazi ya juu, hasa mbele za watu.
 
Inasemekana polisi ni wasomi kuliko JWTZ.

JWTZ wengi ni mbumbumbu
Mh sio kweli, sio jeshi la siku hizi, labda hao polisi ila jeshi siku hizi wanasoma sana

Yani wanajeshi watanzania wanatumia muda wao kazini kusoma kuliko kupigana vita
 
Lugha za kijeshi hizo hata samia ana jina la mnyama, wapo faru, tembo, poongo na huyo dogo mjeshi ni paka anampa mkwara panya!

Niutovu wa nidham constebo wa polisi kumzingua jwtz.
Naomba popote ukiona jwtz Afutwe
Mambo ya Kijeshi Huyu Trafic alitakiwa Kuheshimu Mkuu wake ambae ni Mjenda Staff Sergeant....
 
Matendo ya mtu Ndiyo yanaweza kuonesha yeye ni nani?

Don’t judge easily
 
Ilikuwa zamani hiyo mkuu. Polis siku hizi wengi ni degree holders. Lkn jeshini Kuna mijtu imejiunga juzi tu hapa eti kisa ina nguvu za kunyanyua vyuma
Wote wanaanzia JKT..kwa sifa zinazohotajika.
 
Hivi kati ya JWTZ na Polisi kina nani wanafanya kazi kubwa hapa nchini?
Kila moja kazi yake Ni muhimu ktk kujenga nchi hii, hakuna mwenye kazi kubwa kuliko mwingine. JW wasijione wao ni watu muhimu kuliko watanzania wengine
 
Nenda kenya kajifunze jeshi lao wanaishi vip... Wakiingia hata super market tu raia woote wanatoka nnje wakimaliza ndio mnaingia....
Hapana. Haya hayafanyiki Kenya.

Nchi ikiwa chini ya jeshi (utawala wa kidemokrasia ukipinduliwa ndiyo haya maisha hutokea)
 
Kinidhamu askari wa barabarani kakosea!

Huyo askari wa barabarani ni PC mwanajeshi ni staff serjeant. Askari wa barabarani hawezi kumuonya mwanajeshi kwa sababu ki protokali (yaani ngazi za kicheo) staff serjeant ni kiongozi wake.

Angemuita pembeni azungumze naye si kumuonya.
Mmh! Hapana. Hizi ni kada 2 tofauti. Ukubwa wa JWTZ hauhusiki kwa kazi ya polisi traffic.

Askari wa JWTZ awajibishwe
 
Sasa umeridhika mwenzako kupoteza kazi.Huyo alilewa tu.Sasa subiri aanze kutumia taaluma ya kijeshi kutafuta Pesa atajuta kwanini hamkuvumilia Matusi
Acha kupotosha umma wewe, ajaribu aone kama atatoboa. Au unadhani yeye ndiyo atakuwa wa kwanza kuchomolewa kundini?

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Kuna clip inasambaa kwa kasi mitandaoni ikimuonesha askari wa usalama barabarani akifanya kazi yake lkn askari wa JWTZ anaingilia kazi ya polisi.

Hata polisi alipompa onyo yule askari wa JWTZ kuwa aache kufanya hivyo yule askari alijibu "huwezi kunionya mm paka wewe".

Kwa utovu huu wa nidhamu uliooneshwa na askari wa JWTZ hatua za kinidhamu na kiutumishi zichukuliwe haraka sana dhidi ya huyu askari wa JWTZ ili kuendelea kulinda hadhi na heshima ya jeshi la wananchi.

View attachment 2482212
Naunga mkono hoja,anaweza asifutwe kazi ila akapewa adhabu nyingine
 
Back
Top Bottom