Askari wa JWTZ kizimbani kwa kukaidi amri halali ya askari wa Usalama Barabarani

Askari wa JWTZ kizimbani kwa kukaidi amri halali ya askari wa Usalama Barabarani

Kweli wanaodanyanyana ni wale ambao hawana hata member mmoja kwenye familia ambaye mwanajeshi au hajui kabisa maisha yao ,sasa mtu amekaa kotaz ,amezaliwa kotaz jeshini ,anaonana nao kila siku halafu kuna poyoyo anakuja hapa na kudanyanya watu kwamba wana mishahara mikubwa na wanaishi maisha mazuri.

JWTZ ni kazi kama kazi nyingine tu ,no any special coz hao wanajeshi wametoka uraiani na ni ndugu na marafiki zetu ,tunawaona na tunakunywa nao kitaani.
nenda pale mwenge kalibu na tra kuna kota zao ukacheke walivio lundikana kama nyaya kwenye tenga
 
Sikia maskari wote ni iron boy according to plato..iron boy ni watu wenye akili ndogo wanaotumia nguvu sana badala ya akili..ndio kilichotokea juzi
Sio kweli kwa zama za Sasa
Wapo watu wameingia kwa Shule wengi tu.

Halafu vyeo vina mambo mengi ila nakubali huyo mwamba kaharibu na kutokuwa na shule au exposure vimechangia.
 
Nafikiri ni MAGEREZA TANZANIA
😂🤣😅
ASKARI wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ) amepandishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka ya kukataa amri halali ya askari wa usalama barabarani.

Imedaiwa Mahakamani leo, kuwa MT 89487 CPL Hamis Ramadhan alishindwa kusimamisha gari yake katika kivuko cha watembea kwa miguu eneo la Mlimani City, barabara ya Survey.
Subiri nikachekee nje Mkuu
 
Hayo majengo yenyewe wameanza kuboreshewa sasa hivi,hapo lugalo kuanzia 2014 kushuka chini walikuwa wanakaa kwenye vibanda chakavu vya mabati ukienda maliwatoni unakuta bonge la hall wote mnaingia mnaoga uku mnaonana tupu zenu.
Nyumba zenye uafadhali ambazo walikuwa wanakaa wakubwa zipo mkabala na makongo na kule kambi ya chui tena nyumba zenyewe ni choka mbaya.
Siwezi kulidharau jeshi letu naliheshimu sana ila uyo jamaa amesababisha tuandike yote mpaka tunaonekana tunalidharau jeshi

Kabisa jamaa amefanya watu wafungue turbo ,hatuwadharau ila tunaongea uhalisia wenyewe ,yes wakubwa wanakaa upande wa juu wa makongo ,mimi nilikuwa naenda kumtembelea rafiki yangu afande chinga yaani zile kotaz acha tu hadi aibu.

Kuna Dogo ni soja yaani hadi kumlipia mwanae school fees alishindwa ikabidi ampeleke kayumba,yaani hao jamaa wanapata hela kama unavyosema kukiwa na vijisafari hivi ndipo wanapopata boom kidogo otherwise kwa salary yenye makato kibao ya mikopo wanabaki hawana kitu.
 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ ), MT 89487 CPL Hamis Ramadhan (36) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kukataa amri halali.

Mshitakiwa huyo amesomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Vailet Kyendesya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rahim Mushi, Vailet amedai Februari 07,2023 Mshtakiwa akiwa eneo la Mlimani City Barabara ya Survey, Kinondoni, Dar es Salaam akiendesha gari namba T. 433 ALB Nissan Patrol alisimamishwa eneo la kivuko cha watembea kwa miguu na Askari Polisi ambapo alikaidi na kuanza kumsukuma Askari kwa gari yake.

Kyendesya alidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, hivyo anaiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa, baada ya kusomewa shtaka hilo Mshtakiwa alikana makosa yake na kuachiwa kwa dhamana, ambapo kesi imehairishwa hadi March 6, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Itakumbukwa Feb 10,2023 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua Dereva wa gari aina ya Nissan Patrol aliyeonekana kwenye video iliyosambaa mitandaoni akikaidi amri ya kusimama iliyotolewa na Askari wa usalama barabarani.
Zamani wanajeshi walikua wanakwambia nitakupiga mpaka unitajie namba yangu ya Jeshi.
Siku hizi wanamenyeka vizuri hadi namba zao za Jeshi wanazitaja wenyewe. Chezea Askari Polisi nini?
 
Kabisa jamaa amefanya watu wafungue turbo ,hatuwadharau ila tunaongea uhalisia wenyewe ,yes wakubwa wanakaa upande wa juu wa makongo ,mimi nilikuwa naenda kumtembelea rafiki yangu afande chinga yaani zile kotaz acha tu hadi aibu.

Kuna Dogo ni soja yaani hadi kumlipia mwanae school fees alishindwa ikabidi ampeleke kayumba,yaani hao jamaa wanapata hela kama unavyosema kukiwa na vijisafari hivi ndipo wanapopata boom kidogo otherwise kwa salary yenye makato kibao ya mikopo wanabaki hawana kitu.
Sasa Kayumba si mdiyo shule zetu mkuu? Hivi itawezekana kweli kila mtanzania anayepokea mshahara apeleke mtoto wake Private??
 
Kati ya sehemu wanafundisha nidhamu ni jeshini,nashangaa askari uliyefunzwa unashindwa kutii sheria ndogo kama hizo za barabarani,hii inahitaji akili gani?kama unanidhamu utashindwa vipi kuheshimu kazi ya mtu.
Jeshi halihusiki na utovu wa nidhamu unaofanywa na watumishi wake,mtumishi akideviate uraiani atashughulikiwa na mahakama za kiraia.
Sure na hiyo ndiyo sera yao ,jeshi ni nidhamu ,hawa unawaoona wanaotishia watu mitaani ni wale ambao "SHULELESS".
 
Kaka unafikiri natania? Unazijua ajira ambazo ukimaliza kidato cha nne kuna uwezekano wa kuzipata? Unazijua ajira ambazo ukimaliza kidato cha sita unaweza kuzipata? Unazijua ajira ambazo ukimaliza degree, masters, n.k unaweza kuzipata? Basi hao wote ni takataka kwa wanajeshi ukiwa tu unafikiria sawasawa
Aisee, wewe haulijui Geshi
 
Unaita watu takataka ? Mimi nimezaliwa jeshini na ninaandika hapa nikiwa kambini, hawana pesa

Angekuwa na pesa asingeendesha hilo li Nissan la miaka ya 90
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila wee mtu khaaaah
 
Huyo ni mjinga anahitaji aelimishwe ,mwambie aende kambi ya Lugalo aone mabweni wanayokaa wanajeshi wapya yaani ni aibu ,mikojo hadi kwenye floor ,masinki hadi yamekuwa ya njano yaani tabu tupu ,hawa jamaa kinachowatoa ni mikopo na kweli wana access ya mikopo sana na pia ukiwa na elimu ukaingia TISS ndiyo unapata safari nyingi na kwenda kwenye taasisi hizi kubwa kubwa eg TRA ,TCRA ,Bandarini ,TPDC etc
Hata huko TISS utawakuta wenye njaa kibao tu.
Unadhani ni wangapi wanaopata hizo nafasi kwenda kwenye hivyo vitengo vingine.

Kifupi ukiingia Fanya kazai kama mzalendo na jishushe mbele ya jamii.
 
Maisha gani mazuri!!ya kawaida sana,
Hivyo vimikopo ndio vinawavimbisha vichwa?
Huwezi kuwalinganisha na wahandisi vijana waliopo UN,USAID,migodini,hata pale Helios tower,Kuna watu wanavuta mpunga mrefu kuliko hata wabunge,
Niambie mjeda gani anavuta 50Milioni kwa mwezi?mgodini wapo kibao Tena vijana tu.
Nitafutie connection huko mgodini jamani. Uwiiiiih
 
Bado ushamba haujawatoka ,hasahasa hawa ambao hawana vyeo ,utakuta kwenye "Vibakuli" vyao kwenye dashboard ameweka kofia ya jeshi au kwenye kiti amevalisha kombati lake la jeshi yaani ujinga ujinga.

JWTZ ambaye ameenda shule huwa na nidhamu sana ,hawana mambo ya kijinga na mara nyingi hata hawataki watu wajue kama ni JWTZ ila hawa ambao "makuruti" wana mwembwe sana ,fujo nyingi ili mradi ujue kama yeye ni Mwanajeshi.

Kuna Mjeshi mmoja alikuwa ndani ya kibakuli akawa analeta mwembwe kwa dereva wa bodaboda ambaye alikuwa amempakiza mother mmoja hivi ,alivyoenda mbele akataka kumzingua yule bodaboda kisa ni JWTZ ,yule mother aliyebebwa alishuka akampiga bonge la biti ,akamwambia aache ujinga atamfukuzisha kazi mara moja na akamchana aache ushamba wa kuweka makoti kwenye viti vya gari ili kutisha raia(inaonekana yule mother ni kama mtu wa system ,msoja kumsoma yule mother ikabidi atulie mwenyewe) ,akamwambia ushwahi kumuona mwamnyange ameweka shati kwenye kiti cha gari? JWTZ alinywea mwenyewe!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Elimu yake na huyo trafiki haiwezi kutofautiana; pia wote malimbukeni.

Alisimamishwa kwa kuwa hakuwa kavaa sare za jeshi.
hivi jamaa angesimama tu,wakaongea vizuri kitumishi tu na akaomba radhi angepungukiwa nini,huenda hata asingelipishwa faini,tena wangekuwa marafiki na huuo trafiki,nimeamini kujishusha kunainua.

Kama ameshtakiwa mahakama ya kiraia,maana yake kuna mengine yatampata lazima.
 
Kuna mmoja asubuhi tunawahi uwanjan mida ya sasa kumi na mbili alivalishakoti kwenye kiti bahati mbaya Basi imebeba wa kubwa hili hapa linapita Kushoto kwetu. Niliona akiwa Ana haha kulitoa koti.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom