DOKEZO Responded Askari wamewajeruhi vijana watatu kwa risasi – Uvinza wakati wa msafara wa DC, Mei 5, 2026, hatua zichukuliwe

DOKEZO Responded Askari wamewajeruhi vijana watatu kwa risasi – Uvinza wakati wa msafara wa DC, Mei 5, 2026, hatua zichukuliwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna watu watatu wamepigwa risasi za moto na askari waliokuwepo kwenye msafara wa Mkuu wa Wilaya ya Uvinza walipokuwa wakielekea Kijiji cha Kalilani kilichopo mkoani Kigoma Wilaya ya Uvinza, Tarafa ya Buhingu, Kata ya Buhingu.

Vijana hao wao walishambuliwa na Askari Polisi waliokuwa na silaha za mojo, vijana walitaka kuzui msafara wa Mkuu wa Wilaya hiyo ulipokuwa ukielekea kijijini hapo ili kuzindua tathimini kwa leongo la kuhamisha vitongoji viwili vya mahasa na Kabukuyungu kwa lengo la kuipanua na kuiongezea eneo Hifadhi ya Taifa ya Milima Mahale.

UFAFANUZI WA MKUU WA WILAYA ~ UVINZA: Vijana watatu kujeruhiwa kwa risasi, DC asema waliwavamia Askari wakitaka kuwanyang’anya bunduki

Ili hifadhi hiyo iweze kupata maeneo mazuri na yenye mvuto iweze kujenga nyumba za watalii na mahoteli.

Wananchi wa kijiji hicho wao hawataki kuondoka katika vitongoji hivyo kwa madai ya huko waendapo hakuna shughuli za uvuvi kwani wananchi hao shughuli yao kubwa ya kuwaingizia kipato ni uvuvi.

Hivyo, Mei 7, 2026 majira ya saa 6 mchana kuweza kutendeka tukio hilo vijana watatu waliopigwa risasi na kukimbizwa haraka katika Kituo cha Afya cha Buhingu kwa matibabu.

Vijana hao wameruhiwa vibaya mno huku maeneo yaliyiathirika kwa kupigwa risasi ni mguuni pajani na eneo la goti kwa kila mmoja akipigwa risasi sehemu yake.

Wananchi hao wanaomba kupaziwa sauti ili dunia ijue madhila na hadha wanayo ipitia wanakijiji hao wa kalilani.

Pia soma ~ KIGOMA: Tukio la Watu watatu kujeruhiwa kwa risasi Uvinza, Polisi yasema inafanya uchunguzi
 
Wameshaonja damu za watu ni ngumu wao kuacha kunywa damu! Na mama yao ameshawaambia wapige mikwaju tu...sasa hivi ukiigusa serikali yao dhalimu kidogo tu wanapiga risasi! Daah
 
Polisi + Wananchi
tokea uchaguzi mkuu, kila mtu amekuwa mwehu na Hakuna anaye muamini mwenzake
 
Wayaue tu Maamae si waliambiwa wawakatae wakajifanya kushupaza shingo, kwahiyo huko hadi wadiisii wana misafara ya asikari na mabunduki, wanywa damu sikuZote huendelea tu
 
Back
Top Bottom