Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

Asante sana Bishop.

Hili ni somo zuri sana kwetu sote na hususani NEC na ZEC.

Umenikumbusha jambo moja kuhusu mitume 12 wa Yesu Kristo.

Baada ya Yuda Iskariote kujitenga na wenzake kwa usaliti wake kwa Bwana, walibaki 11.

Kufanya replacement ya Yuda Isakariote, demokrasia ilitumika na Mathias akachaguliwa na kujaza nafasi hiyo.

Mungu ndiye muumba na mwenye uwezo wote. Angeweza kutumia mamlaka na nguvu zake kumteua yoyote aliyemtaka.

Lakini aliacha watu wanaoongozwa wachague wenyewe wamtakaye lakini chini ya "guidance" ya Mungu Roho Mtakatifu.

Sijui NEC na ZEC wanakwama wapi ku - play role yao ya kutoa "guidance" njema na fair ili watu wajipatie viongozi watakaoshirikiana nao ktk shughuli zao za kila siku.

Asante sana Bishop. Wewe u mkweli na huu ndiyo Utumishi wa kweli wa Kristo Yesu anaoutaka, kuongea UKWELI bila woga.
 

Umeshindwa kuelewa jambo moja...

Askofu Bagonza, mimi na pengine hata wewe wote tunatambua kuwa ziko sheria za uchaguzi na kanuni zake zinazongoza (guide) mchakato mzima wa uchaguzi wote....

Na kimsingi, malalamiko na matatizo haya msingi wake ni SHERIA na KANUNI hizo....

Jiulize swali moja hili la msingi;

Kwamba, unaweza vipi kutunga sheria na kanuni zenye lengo la kupora HAKI ZA WATU?

Defenetely, SHERIA na KANUNI hizi ni batili kwa namna yeyote na ziko kinyume na KATIBA YA NCHI kama ambavyo Bishop ameeleza kwa ufasaha kuwa, sifa za msingi za mtu kuchaguliwa ili awe kiongozi ni hizi;

å Awe Raia wa Tanzania
å Awe na umri wa miaka 18+
å Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la jinai
å Awe hajawahi kuhukumiwa kwa kosa la kukwepa kulipa kodi
å Adhaminiwe na chama cha siasa.

Hayo mengine yote unayoyaeleza wewe siyo vigezo wala sifa za msingi...

Mfano kukosea uandishi wa jina, tarehe ya kuzaliwa nk hayo yanaweza kurekebishwa mbele ya msimamizi wa uchaguzi ili mradi mtu halisi anayetaka uongozi yuko pale na akiwa tayari anazo sifa zote za msingi...

Mbona kwenye mabenki ama ktk taasisi zingine huwa tunapata guidance ktk ujazaji wa fomu mbalimbali?

Kuna kosa gani msimamizi kumwelekeza mgombea kujaza fomu zake kwa usahihi so long as anazo sifa za msingi?

Bishop yuko very right. Nakubaliana naye 100%....
 
Mimi sijasema Bagonza yuko right au la! Nilichoshauri ni way forward Katika mazingira haya ya sasa.

Kipi bora Kuingia katika uchaguzi hivyo hivyo huku ukiwa na uwezekano wa kushinda au kufanya vurugu ukose hata hicho ambacho ungepata?

Kuna msemo " one bird at the hand is better than ten birds at the bush.
 
Ni kweli tupu baba Askofu, ni kuwadharau na kuwachokoza wananchi!
 
"Ni mzigo na adhabu kubwa kwa wananchi kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua. Ni kuwatesa wananchi, ni kuwadharau, na kuwadhalilisha. Tuliwakataa wakoloni kwa sababu walitutawala bila sisi kuwachagua"-; Dkt. Benson Bagonza, Askofu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
 
Sasa unamfananisha January na mwalimu Nyerere bwashee?!!
 
Subirini bas tupige kura na matokeo yatangazwe mbna mnaweweseka sana wakuu...
 
Uko sahihi sana mkuu! Hili jambo linafikirisha na kuumiza roho sana! Linatia uchungu na hasira ya haraka! Sababu zinazotumiwa na TUME kuengua wagombea wa upinzani zinazua maswali mengi kuliko majibu!

1. Tume kumuengua mgombea eti kisa amekosea kujaza form, Je kwanini tume na wasimamizi hawatoi nafasi kwa wagombea kufanya marekebisho kwenye form zao kama kuna makosa??

2. Je kwanini tu asiitwe kuja kuilipia na kujaza upya???

3. Uchaguzi katika mfumo wa vyama vingi ni ushindani baina ya vyama , Je kwanini TUME inabariki mshindani aingie pekeake uwanjani, huo ni ushindani gani!??

4. Kwanini form itumike kama kipimo cha uwezo na sifa za kiongozi kwani bungeni na mabaraza ya madiwani wanakwenda kufanya kazi ya kuzaja form au kuwakilisha wananchi???

5.Kwanini katika orodha ya walioenguliwa hakuna hata diwani wala mbunge hata mmoja toka ccm??

6.Je huu sio mpango wa CCM yenyewe?

7. Je kwanini TUME inakuwa mchaguaji wa wagombea badala ya kuwa mwidhinishaji???

Hata hivyo majuzi nimemsikia mteuaji wa tume akiwa huko Mwanza ambako alisikika akipongeza wananchi wa Misungwi kwa kupitisha wagombea bila kupingwa!

Alienda mbali zaidi na kulalamika kuwa amebakia yeye tu ndiye hajapitishwa bila kupingwa! Kiukweli ni jambo la kusikitisha na kushangaza sana kwa mtu ambaye ndiye mlezi mkuu wa demokrasia kufagilia uminywaji wa mbaya wa demokrasia kama huo!

Wamefanya kampeni miaka 5 huku wapinzani wakiwa bench halafu leo wanakimbia kupambana na wapinzani! Mwenyezi Mungu tunakuomba ukatende maajabu, wale wote wenye nia ovu dhidi ya haki walegee, washindwe na waanguke kwa anguko kuu!
 
Hakika tunahitaji katiba mpya itakayofanya TUME hii kuwa mwidhinishaji tu wa wagombea walioteuliwa na vyama vyao na isiwe na mamlaka yoyote katika kumzuia au kumuengua mgombe yeyote, mamlaka hayo yabakie mikononi mwa chama kilichomteua! Tume ibaki kuwa chombo cha kusimamia uchaguzi tu na si zaidi ya hapo! Pia matokeo ya mgombea yeyote yaidhinishwe na mahakama ya kikatiba! Nafkiri ni Lissu tu ndiye anayeweza kutufikisha huko!
 
Kama gwajima anavyofanya
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
 

Hiyo haituhusu.. Dhambi kila mtu anaijua.. Ukikemewa usisingizie mbona nae hafanyi hivi.. Wewe acha dhambi tuu nae atajibu kivyake mbinguni.
 
Hiyo haituhusu.. Dhambi kila mtu anaijua.. Ukikemewa usisingizie mbona nae hafanyi hivi.. Wewe acha dhambi tuu nae atajibu kivyake mbinguni.
Kama ankemewa na sisi tutamkemea,
Kama ameweza kukemea basi na yeye atakemewa tu.
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
Unaelewa msingi wa dini? Jamaa yako kila siku anasema aombewe. Kwa nini wanasiasa wasijiombee wenyewe?

Kama ambavyo unaona umuhimu wa kuwaambia waamin na viongozi wa dini wawaombee ndivyo wanapaswa kuwa tayar kuyapokea makaripio yao pia.
 
Huku kulia yupo Askofu Bagonza, hapa kati wapo Sheikh Ponda & Askofu Mwamakula na kushoto pale kasimama Askofu Niwemugizi.

mbarikiwe sana enyi watumishi wa Mungu!
Wengine wanasubiri sadaka jumapili hii wakanywee bia hayo madhuluma hawayaoni.
 
Hawa Ndio ma Fake Pastors Anaonekana kabisa mpinzaniii wanacholialia wapinzani na Yeye analialia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…