Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

Uchaguzi 2020 Askofu Bagonza aitaka NEC isitumike kudhulumu Watanzania

*Lwakalinda Kalikawe Bagonza kaandika hivi:*

NEC WAHURUMIENI WANANCHI
NEC WAHURUMIENI VIONGOZI.

Kuna jambo haliko sawa. Kama liko sawa, basi kuna jambo haliko sawa ndani yangu.

1. Ni mzigo na adhabu kubwa kwa Wananchi kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua. Ni kuwatesa wananchi, ni kuwadharau, na kuwadhalilisha. Tuliwakataa wakoloni kwa sababu walitutawala bila sisi kuwachagua. Desemba 9 kila mwaka ni muhimu kwetu kwa sababu tunakumbuka siku tulipoamua kuchagua Viongozi na watawala wetu.

2. Ni mzigo mzito kwa kiongozi kuwaongoza watu ambao hawakukuchagua. Ni dharau na mateso kwake kulazimika kuwaongoza watu ambao hujui kama wanakupenda au hawakupendi kwa sababu hawakupiga kura kukuchagua.

Yote mawili hapo juu ni uchokozi. Tume inawachokoza wananchi kwa kuwalazimisha kuongozwa bila kuchagua. Ni kuwachokoza Viongozi kwa kuwalazimisha kuongoza bila ridhaa ya wananchi. Uchokozi haujawahi kuwa na matokeo mazuri.

Vigezo vya mtu kugombea vinafahamika kikatiba: Raia, umri, dhamana ya chama, kutohukumiwa kifungo, kutohukumiwa kukwepa kodi, muda wa kurejesha fomu nk. Haya hayahitaji wiki kuyaamua

Viongozi wetu uteuliwa/upendekezwa na vyama na kuchaguliwa na wananchi. Tume imeanzisha kundi jipya la Viongozi wanaoteuliwa na tume. Jimbo liitwalo TUME liko mkoa gani? Kata iitwayo TUME iko wilaya gani?

Tulifanya hivyo serikali za mitaa na sasa tunataka kufanya hivyo kwenye bunge. TUNAKOSEA. Hatutakuwa na uhalali wa kudai utii na Maendeleo kwa watu waliolazimishwa kuongozwa na watu wasiochaguliwa. Hatutakuwa na uhalali wa kudai matokeo chanya kwa Viongozi tuliowalazimisha kuongoza bila kuchaguliwa.

Hata baadhi ya mifumo ya kidini isiyochagua Viongozi kidemokrasia hailazimishi muumini kuikubali. Ni kwa mujibu wa Imani, si Sheria.
Hawa Viongozi Wa Dini Serikali iKiamuaa kuwachunguza wanamadahifu mengi sana Wanakula waumini Wanafuja sadaka ila kwa sababu Magu sio Mbeya kakubali kila MTU aubebe mzigo wake mwenyewe
 
Maaskofu hawahawa wanaokuja hapa na kukemea dhambi lakini majumbani kwao wanashindwa kuzikemea familia zao?

Unakuta baadi ya maasikofu vijana wao wameshindikana na wameshindwa kuwakemea.

Utakuta huyo askofu anakemea lakini yeye mwenyewe ni roho mbaya hata msaada hana kwa jamii anayoiongoza.

Kuliko jiwe?
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
We ng'ombe yani Kutetea HAKI ndio siasa???? Kweli misukule ya lumumba mnashida kubwa sana
 
Tume wanasimamia sheria.

Hili jambo litoe funzo kubwa kwa vyama kuhusu umakini wa kujaza fomu. Ujazaji fomu usiwe jukumu binafsi la mgombea bali chama chake. Chama kiwakusanye wagombea wake wa jimbo au mkoa pamoja kisha wasimamiwe kujaza na zikaguliwe ndipo waruhusiwe kuzirudisha tena kwa kusindikizwa.
Kumbuka kuna wagombea wanajaza vibaya makusudi na kuna wanaojaza vibaya sababu ya uelewa mdogo.
Hivi kama yule mgombea wa Moshi vijijini hata majina yake yaliyoko katika kitambulisho cha taifa hayajui?

Iweje fomu ajaze jina la Lucy na kitambulisho kina jina Lusesia tena na ubini majina tofauti je hawa ni mtu mmoja au wawili tofauti ? Ni rahisi kulaumu lakini kama wewe ndiyo unatakiwa uamue hizo rufaa na kanuni na sheria ziko wazi utapinda sheria tu ili kufurahisha watu?

Lingine, kwa kuwa hivi vyama viwili vya CDM na ACT ndivyo vinalalamikia zaidi jambo hili, busara hapa ni kumuunga mkono mgombea aidha wa ACT au CHADEMA ambaye amebaki kuliko kujidanganya wanaweza kulazimisha warudishwe kwa kufanya vurugu. Kule Pemba nimeona walau majina yasiyopungua mawili wamerejeshwa hivyo ACT wanaweza wasiwe na wagombea majimbo kama saba au sita hivi, lakini katika majimbo wasio na wagombea, CHADEMA wameweka wagombea kama majimbo manne hivi, kama kweli wanashirikiana kama wanavyodai ina maana mwisho wa siku wana wagombea kwa pamoja Pemba majimbo yasiyopungua 15 kati ya majimbo 18. Hivyo badala ya kuthubutu kufanya vurugu ambazo mwisho wa siku wanaweza hata wasishiriki uchaguzi na wakakosa uwakilishi kwa miaka mingine 5 ni bora waingie katika uchaguzi katika mazingira haya ya sasa kwani wana uhakika wa kambi yao kunyakua viti 15 .

Zaidi hivi ni viti vy bunge la muungano na Maalim Sefu shida yake kubwa ni urais wa Zanzibar ambao kama akishinda ana nafasi ya kuteua wawakilishi 10 katika Baraza la Wawakilishi.

Msijidanganye eti mtafanya vurugu, kwanza hamuwezi na pili hamtafanikiwa kuwarejesha walioenguliwa na mtapoteza hata ambacho ilikuwa mpate.

Jifunzeni sana kutii na kufuata sheria.
Hapo unaposema watanzania hawawezi kufanya vurugu ndio mnapokosea mnawachukulia POA Sana.
 
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
Bogus. Angemuunga mkono Magufuli pia ungeongea hivyo.
 
Ingekuwa waislamu sasa wako police kuhojiwa
 
Kenge hasikii mpaka damu imtoke masikioni.

Ngoma wataicheza wote. Mda ni mwalimu mzuri. Ameeeeen.
 
Tulia dawa ikuingie japo chungu
Na hawa wa makanisani wangekaa kimya kuhusu siasa au Serikali ingewasweka kama mashehe wa Uamsho, maana nao siasa ziliwaponza baada ya kuhangaika na dini zao.
 
Nimemvulia kofia huyu Baba Askofu. Maneno yake yanachoma mpaka kwenye roho.
 
Mimi sijasema Bagonza yuko right au la! Nilichoshauri ni way forward Katika mazingira haya ya sasa.

Kipi bora Kuingia katika uchaguzi hivyo hivyo huku ukiwa na uwezekano wa kushinda au kufanya vurugu ukose hata hicho ambacho ungepata?

Kuna msemo " one bird at the hand is better than ten birds at the bush.

You are very right and I have no problem with your suggestion...

Hata hivyo, kwani kuna mtu kakuambia atafanya vurugu? Umeyapata wapi haya?...
 
Baba askofu yupo sahihi kwa asilimia mia , tume inapata wapi mamlaka ya kupitisha watu eti wamepita bila kupingwa ? Katiba inasema viongozi wote watapata mamlaka kutoka kwa wananchi sio kutoka tume ya uchaguzi muwe mnaelewa kijani kibichi .
IMG_20200910_181034_6.jpg
 
You are very right and I have no problem with your suggestion...

Hata hivyo, kwani kuna mtu kakuambia atafanya vurugu? Umeyapata wapi haya?...
Kwani wewe hujawasikia? Mbona mara nyingi tu wamesema , pitia clip zao you tube.
 
*Lwakalinda Kalikawe Bagonza kaandika hivi:*

NEC WAHURUMIENI WANANCHI
NEC WAHURUMIENI VIONGOZI.

Kuna jambo haliko sawa. Kama liko sawa, basi kuna jambo haliko sawa ndani yangu.

1. Ni mzigo na adhabu kubwa kwa Wananchi kuongozwa na kiongozi ambaye hawakumchagua. Ni kuwatesa wananchi, ni kuwadharau, na kuwadhalilisha. Tuliwakataa wakoloni kwa sababu walitutawala bila sisi kuwachagua. Desemba 9 kila mwaka ni muhimu kwetu kwa sababu tunakumbuka siku tulipoamua kuchagua Viongozi na watawala wetu.

2. Ni mzigo mzito kwa kiongozi kuwaongoza watu ambao hawakukuchagua. Ni dharau na mateso kwake kulazimika kuwaongoza watu ambao hujui kama wanakupenda au hawakupendi kwa sababu hawakupiga kura kukuchagua.

Yote mawili hapo juu ni uchokozi. Tume inawachokoza wananchi kwa kuwalazimisha kuongozwa bila kuchagua. Ni kuwachokoza Viongozi kwa kuwalazimisha kuongoza bila ridhaa ya wananchi. Uchokozi haujawahi kuwa na matokeo mazuri.

Vigezo vya mtu kugombea vinafahamika kikatiba: Raia, umri, dhamana ya chama, kutohukumiwa kifungo, kutohukumiwa kukwepa kodi, muda wa kurejesha fomu nk. Haya hayahitaji wiki kuyaamua

Viongozi wetu uteuliwa/upendekezwa na vyama na kuchaguliwa na wananchi. Tume imeanzisha kundi jipya la Viongozi wanaoteuliwa na tume. Jimbo liitwalo TUME liko mkoa gani? Kata iitwayo TUME iko wilaya gani?

Tulifanya hivyo serikali za mitaa na sasa tunataka kufanya hivyo kwenye bunge. TUNAKOSEA. Hatutakuwa na uhalali wa kudai utii na Maendeleo kwa watu waliolazimishwa kuongozwa na watu wasiochaguliwa. Hatutakuwa na uhalali wa kudai matokeo chanya kwa Viongozi tuliowalazimisha kuongoza bila kuchaguliwa.

Hata baadhi ya mifumo ya kidini isiyochagua Viongozi kidemokrasia hailazimishi muumini kuikubali. Ni kwa mujibu wa Imani, si Sheria.
Ni kweli ila hao ni wawakilishi tu wabunge, viongozi ni Rais na maRC na ma DC ambao ndiyo wenye mamlaka ya uongozi. Wakuu wa mikoa/wilaya tunachaguliwa hatuwachagui sisi. Kweli Tz bado hadi wabunge tunachaguliwa achilia mbali viongozi wakuu wa mikoa na wilaya
 
Back
Top Bottom