Askofu Bagonza: JWTZ ni Jeshi la Wananchi, si Jeshi la Watawala wala Viongozi!

Nchini kwetu sauti kama hii zimefifia na kupotea. Tunamshukuru baba askofu na wote wanaothubitu kusema katika mazingira haya.
 
Jaman kwani mnamjua anayetishia utulivu wa nchi??!! Maana mkuu katupa jiwe gizani.
 
Huyo askofu kwa kweli kaamua..
Hivi maaskofu wengine wana elimu kama yake au huyu kawazidi
 
Umenena vyema. Inahitaji kutambua kama ulivyo mfano wako wananchi wa uganda walishirikiana na wanajeshi wa Tanzania kumg'oa Idd Amin. Adui akirikiana na wananchi anaweza kulishinda jeshi imara lenye silaha za kisasa. Kulifanya jeshi la chama tawala na viongozi kwa njia yeyote ile ni ujinga na kulidhoofisha
 
Aisee, kwahiyo yeye kama mkuu wa jeshi mlitarajia angeongela vita wakati hatuna vita, au majukumu ya jeshi wakati wa amani yamebadilika!!!
Kwani ilikuwa lazima yeye aongee. Hata kama ni wakati wa amani ndio aongee vile kwa kuchimba mkwala. Wapi uliona hiyo! Umeongea kitoto, sorry kama nimekukwaza upo form gani?
 
Maneno murua toka kwa baba Askofu Bagonza.Baba Askofu,you have stricken the iron while hot.Sasa mtu akaze shingo atokwe damu masikioni.
 
Kwani ilikuwa lazima yeye aongee. Hata kama ni wakati wa amani ndio aongee vile kwa kuchimba mkwala. Wapi uliona hiyo! Umeongea kitoto, sorry kama nimekukwaza upo form gani?
Kwani baada ya kumaliza vidato vyote ulijuaje kwamba sasa umekua??? , unafikiri kitoto zaidi.

Huna sababu ya kuogopa kama si mvurugaji wa amani aliyetajwa, vinginevyo kaza shingo na mpango wako.
 
kuna watu mpaka leo hawaamini kuwa mtu wao alishindwa.
 
Suala la Kibiti lilikua na viashiria vya Ugaidi.
Hata hivyo Wanajeshi kuungana na polisi hailikua suala la kulenga Chama au wanasiasa bali adui .
Suala la Kibiti lilikua linahusisha adui mwenye silaha za kivita hivyo ni lazima vyombo vyote na wananchi washirikiane kumtoa adui kwanza.
Yanayofanywa na watawala na makada wa Chama tawala ni kutengeneza adui wa kufikirika wa madaraka yao na maslahi yao na kulihusisha jeshi.
Sio jambo jema hata kidogo.

Jiulize Mkurugenzi anayemtangaza Mgombea aliyeshindwa kuwa ameshinda ,halafu Jeshi lipo linamuangalia mtu anayetengeneza mazingira ya kuvunja amani kwa kutegemea Jeshi hilo hilo lije lipige au liue raia mamia kwa ubinafsi wa mtu mmoja kutetea cheo chake ; kwa nini wasianze kukata virungu kwanza huyo mkurugenzi na kumkamata mtu anayepora sanduku la kura kama kule kinondoni walivoachwa wakafanya?
Watu wanaporwa form za uchaguzi kwenye ofisi za mkurugenzi lakini hatusikii waporaji hao wakitolewa maneno ya vitisho kuwa wanahatarisha amani ya nchi kwa kuvuruga chaguzi zinazoandaliwa kwa mamilioni ya kodi za wananchi.

Tofautisha masuala ya uhalifu au mauaji ya Kibiti ambayo hayapo kikatiba wala kisheria bali ni viashiria vya ugaidi na Shughuli halali za kisiasa. Kwa sasa Tanzania mivutano iliyopo mingi inagusa maslahi na sio usalama wa watu.
Bunge na CAG, CCM na Wapinzani ,Serikali na vyombo vya habari, Serikali na uwazi, Spika na Wabunge wasema kweli n.k. haya ndiyo yanayowanyima walaji usingizi na sio vinginevyo.

Yule bwana Mkubwa wa wajeda anapaswa awe na tahadhari sana wakati wa kufanya mikutano ya hadhara ili asishiriki kuwagawa wananchi ambao ndio zao la wapiganaji wetu bila kujali vyama ,dini na makabila.

Ukitaka ujue nani mpiganaji ni wakati wa vita dhidi ya adui wa nje sio haya mambo ya kupiga watu waliobeba vichinjio vya kura.

Askofu Bagonza ni Mtu Mwona mbali sana. CCM na wapambe wake hawawezi kumwelewa kwa sasa wanadhani Vyama vya upinzani hawana ndugu wala marafiki ndani ya idara nyingine zaidi ya siasa.

Tusiruhusu watu kutafuta madaraka na maslahi yao kwa kutugawa au kutuchonganisha.
Jeshi lolote imara duniani ni lazima lilinde Katiba ,sheria ,na amani ya wananchi wake wote sio kusimama upande wa watawala na Makada wa Chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku umri wa mtu unapimwa kwa hoja zake. Ukija na hoja za kitoto hata kama una karne 4 unaonekana mpuuzi tu.
Sasa unaona ulivyojibakiza uchi!!!! Uliuliza kidato ukiwa na maana gani!!! Maana wewe labda umevuka kidato cha sita, lakini upeo wako ni mashaka makubwa.
 

Acha upotoshaji dogo, huyo CDF anacheza siasa hilo halina mjadala. Kama aliruhusu kamisheni ya jeshi kupokea wanaccm, hata aongee vipi msimamo wake uko wazi kwamba yuko kwa maslahi ya ccm na sio amani ya nchi fullstop.
 
Na yeye ndie alietufikisha hapa na li chama lake
 
No
Huo ndiyo ukweli mchungu

Inashangaza kumwona Kamanda wetu Jenerali Mabeyo ameamua kumlinda Jiwe badala ya kuwalinda wananchi wa Tanzania, kama anavyotakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977
Kwa kweli hata Mimi imenishtua maana hatukuzoea kumsikia kamanda nae anaingia mambo ya siasa na kutumia maneno tata kama uchochezi. Hayo awaachie akina Siro!
 
PhD za ukweli utazijua tu,Mungu mbariki Askofu Bagonza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…