Dkt.Benson Bagonza Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe alikuwa akihojiwa na Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu ambaye alimuuliza " Baba Askofu ningependa nikuulize, wewe umekuwa ukitoa mawazo yako hadharani juu ya masuala ya kisiasa huwa hakuna 'contradiction' kwamba unaingiza labda Siasa ndani ya Dini?..."
Askofu Dkt. Bagonza. “Mimi nadhani siasa ni uwanja wa watu wote lakini Dini ni uchaguzi wa mtu binafsi, Siasa ni yetu wote kwakuwa tunapiga kura, tunalipa kodi, ni yetu wote na sioni sababu ya mtu kumuwekea mtu mwenzake mipaka..." -
Aliongeza kusema, "Kwanini mnahoji kwamba nachanganya Dini na Siasa?, nikijenga Shule mbona hamsemi nachanganya Elimu na Dini?, nikijenga Hospitali mbona sihojiwi kwamba nachanganya Afya na Dini?, nikichimba kisima cha maji kwa wananchi mbona hawasemi kwamba unaingilia idara ya maji?..." -Askofu Dkt. Bagonza
"... nikimkuta mgonjwa pale nikampa dawa siulizwi kwanini unachanganya Dini na Siasa na hata sihojiwi kwanini unachanganya Afya na Dini lakini nikihoji kwanini mgonjwa huyu hana dawa?, kwanini serikali haileti dawa kwaajili ya mgonjwa wanasema aaah.., anachanganya Dini na Siasa, sasa huoni hapo kwamba kuna shida ya kimantiki?” -Askofu Dkt. Bagonza.