Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Pre GE2025 Askofu Bagonza: KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu, Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu Askofu wa CHADEMA kwa jina la Bagonza aache upuuzi. Wakipondwa CCM na Mwenyekiti wake hufurahia na kukaa kimya ila wakisifiwa huwa wa kwanza kujitokeza na kuropoka upumbavu.
 
Huyu Askofu wa CHADEMA kwa jina la Bagonza aache upuuzi. Wakipondwa CCM na Mwenyekiti wake hufurahia na kukaa kimya ila wakisifiwa huwa wa kwanza kujitokeza na kuropoka upumbavu.
Ameshasema yeye anatumia Ujinga kueneza Dini na Siasa, kama wewe mjuaji kaa pembeni aendelee na safari yake

Sasa wewe unawashwa wapi?
 
Sababu 95 za Padri Martin Luther kuondoka Katoliki na kuanzisha kanisa zote ni za msingi sana, unataka nikutajie 5 za msingi?
Yaani umepita mulemule. Kwa hiyo nondo, jamaa akiinuka tena kukufuata, nigutue mkuu.
 
Ameshasema yeye anatumia Ujinga kueneza Dini na Siasa
Halafu usikute hapa alijivika uhusika wa wapelekewa-ujumbe huo ili kuzidi kuwachanganya na kuwachanganua. Bila shaka itachukua miezi kadhaa kuuelewa ukweli wote kuhusu alichosema askofu.
 
Hili Kanisa tatizo lilianza pale walipoamua kujitenga na Kanisa mama la Roman Catholic, wakijitambua , kuacha ujeuri, kiburi na tamaa za pesa wanaweza kujirudi ndani ya Kanisa Mama la RC


Tumsifu Yesu Kristu.
Wewe nawe.....kwani walijitenga lini ?....na hayo matatizo Yao yalianza lini baada ya kujitenga na hao RC ?
 
KKKT Ina MKUU MMOJA TU

Naona KKKT imepamba moto kutokana na matamshi ya mmoja wa Maaskofu wake. Kwa kimbelembele nilicho nacho naomba umma wa watanzania uelewe yafuatayo:

1. KKKT ina Mkuu mmoja tu. Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja.

2. KKKT hakuna cheo kinaitwa “Mkuu wa Kanisa Mstaafu”. Tunaweza kuwa na cheo cha “Aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa”. Hivi sasa tuna “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” ambaye amechaguliwa tena Mkuu wa Kanisa. Kama angekuwa Mstaafu asingechaguliwa. Inawezekana “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” akachaguliwa kuwa Mkuu tena. Sitashangaa aliyepita hivi karibuni, kuchaguliwa tena.

3. Kama kuna mstaafu, ASTAAFU. Si lazima kuhudhuria; si lazima kusema. Ukipenda, usipende kwa niaba. Ukichukia, usichukie kwa niaba. Kila ulimi una uwezo wa kuonja wenyewe,

4. KKKT ni shirikisho, siyo kanisa moja. Ukitaka kusema kwa niaba ya shirikisho, unashawishi siyo kuburuza, Hatujashawishika na hatujakaa.

5. Nampenda rais Samia, lakini sijatumwa na kanisa. Naweza kumpenda na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Hayo nitayasemea Karagwe siyo penginepo. Na nikiyasema, ni yangu na tumbo langu; siyo ya Wanyambo wala Walutheri walio wenye vyama vyao. Wanyambo haturuhusu mgeni kupiga mluzi katika nyumba ya mwenyeji.

6. Kanisa lina wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama. Chadema msitutolee macho na CCM msishangilie. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa.

7. Rais Samia ana uwezo wa kujiharibia. Tusimharibie. CCM ina uwezo kujiharibia; haijaomba msaada wa kuisaidia kuharibu. Lipo kundi linalodhani linamsaidia rais Samia, wakati linamharibia. Lipo linalodhani linamharibia lakini linamjenga. Anayesimama na HAKI anamsaidia rais Samia.

8. Tuna tatizo kitaifa: Kuna watu wanatumia dini kueneza siasa. Na kuna watu wanatumia siasa kueneza dini. Mimi si mmoja wa hao wawili. Mimi natumia ujinga kueneza dini na siasa. Wajinga tu, ndio wananisikiliza na kunifuata. Wewe mjuaji kaa pembeni tuendelee na safari.

9. Nikisema jambo mkanishangilia, mnanipa kiburi cha kusema bila kufikiri.
Nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari; si kuhemuka. Mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana.

10. Mungu analipenda Taifa hili kuliko mtu au chama chochote kinavyoweza kudai kulipenda. Usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili taifa. Ina gharama nzito kushuhudia Mungu anavyolipenda hili taifa.

Hata anayerudi nyuma ana mbele anakoelekea. Ukisifiwa kuwa na mbio, jihadhari usipitilize nyumbani kwenu.

Source: FB page yake

Pia soma
Kifo cha Dr Erasto Kweka, kimemfanya Dr Shoo kutotawalika Tena.
Hata katiba ya dayosisi ameisingina.
 
Wewe hutaki bahasha?!
Hivi huamini kuwa kuna watu wanaoweza kukataa kujitoa akili namna hiyo kwa sababu ya fedha? I mean mtu anaweza kuwa na shida kweli na akapokea fedha lakini angalau akapiga debe kwa kutumia akili na busara. BTW huyu askofu hizo alizokwisha chuma hazimtoshi mpaka afikie stage hii?
 
Askofu anatakiwe anyooki na sio mafumbo mengi ni kama mwoga, yeye ni kiongozi, na asiwe vuvugu . Pa kukemea akemee, pa kuonya na aonye kwa ajili ya masilai ya taifa
ELIMU ELIMU ELIMU
 
Nje ya mada kidogo kuna mapadri waliuawa na kutupwa kwenye matenk ya maji tena kanisani, mbona sisikii kanisa likishinikiza polisi wafanye uchunguzi haraka? Au tuamini ni INSIDE JOB?
Anzishia mada yake..
 
Shoo kama yuko CCM na Bagonza CDM kuna shida gani?
* Mbn Bagonza husema mengi lkn wenzake hawafuatilii wala kukosoa sapoti yk kwa CDM!

* Kuna mtanzania asojua msimamo wa Bagonza kuhusu CDM?
Wenzako wanaoandika pumba kama uliyoandika hutumia id fake.. sasa wewe unaandika jambo bila kushirikisha uongo kwa id halisi tena na picha lako umeweka.,!?!😭
 
Back
Top Bottom