Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 28,916
- 40,479
Kanisa katoliki sio Takatifu, upo tayari tujadili kinagaubaga?Huyu Askofu kumbe nae ana kichwa kizuri...nitaanza kumfuatilia...
Huyu alifaa awe Kanisa Takatifu la Mitume...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kanisa katoliki sio Takatifu, upo tayari tujadili kinagaubaga?Huyu Askofu kumbe nae ana kichwa kizuri...nitaanza kumfuatilia...
Huyu alifaa awe Kanisa Takatifu la Mitume...
Ameshasema yeye anatumia Ujinga kueneza Dini na Siasa, kama wewe mjuaji kaa pembeni aendelee na safari yakeHuyu Askofu wa CHADEMA kwa jina la Bagonza aache upuuzi. Wakipondwa CCM na Mwenyekiti wake hufurahia na kukaa kimya ila wakisifiwa huwa wa kwanza kujitokeza na kuropoka upumbavu.
Yaani umepita mulemule. Kwa hiyo nondo, jamaa akiinuka tena kukufuata, nigutue mkuu.Sababu 95 za Padri Martin Luther kuondoka Katoliki na kuanzisha kanisa zote ni za msingi sana, unataka nikutajie 5 za msingi?
Halafu usikute hapa alijivika uhusika wa wapelekewa-ujumbe huo ili kuzidi kuwachanganya na kuwachanganua. Bila shaka itachukua miezi kadhaa kuuelewa ukweli wote kuhusu alichosema askofu.Ameshasema yeye anatumia Ujinga kueneza Dini na Siasa
Wote walikuwa wanampinga Magufuli kwa kuwa alikuwa hawapi ulajiAskofu Shoo amekua wa hovyo sana!
Wewe nawe.....kwani walijitenga lini ?....na hayo matatizo Yao yalianza lini baada ya kujitenga na hao RC ?Hili Kanisa tatizo lilianza pale walipoamua kujitenga na Kanisa mama la Roman Catholic, wakijitambua , kuacha ujeuri, kiburi na tamaa za pesa wanaweza kujirudi ndani ya Kanisa Mama la RC
Tumsifu Yesu Kristu.
Umesikika Mrs Bagonza.Ameshasema yeye anatumia Ujinga kueneza Dini na Siasa, kama wewe mjuaji kaa pembeni aendelee na safari yake
Sasa wewe unawashwa wapi?
Jibu swali mama, unawashwa washwa wapi?Umesikika Mrs Bagonza.
Kifo cha Dr Erasto Kweka, kimemfanya Dr Shoo kutotawalika Tena.KKKT Ina MKUU MMOJA TU
Naona KKKT imepamba moto kutokana na matamshi ya mmoja wa Maaskofu wake. Kwa kimbelembele nilicho nacho naomba umma wa watanzania uelewe yafuatayo:
1. KKKT ina Mkuu mmoja tu. Dereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja.
2. KKKT hakuna cheo kinaitwa “Mkuu wa Kanisa Mstaafu”. Tunaweza kuwa na cheo cha “Aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa”. Hivi sasa tuna “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” ambaye amechaguliwa tena Mkuu wa Kanisa. Kama angekuwa Mstaafu asingechaguliwa. Inawezekana “aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa” akachaguliwa kuwa Mkuu tena. Sitashangaa aliyepita hivi karibuni, kuchaguliwa tena.
3. Kama kuna mstaafu, ASTAAFU. Si lazima kuhudhuria; si lazima kusema. Ukipenda, usipende kwa niaba. Ukichukia, usichukie kwa niaba. Kila ulimi una uwezo wa kuonja wenyewe,
4. KKKT ni shirikisho, siyo kanisa moja. Ukitaka kusema kwa niaba ya shirikisho, unashawishi siyo kuburuza, Hatujashawishika na hatujakaa.
5. Nampenda rais Samia, lakini sijatumwa na kanisa. Naweza kumpenda na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Hayo nitayasemea Karagwe siyo penginepo. Na nikiyasema, ni yangu na tumbo langu; siyo ya Wanyambo wala Walutheri walio wenye vyama vyao. Wanyambo haturuhusu mgeni kupiga mluzi katika nyumba ya mwenyeji.
6. Kanisa lina wanachama wa vyama vyote na waumini wasio na vyama. Chadema msitutolee macho na CCM msishangilie. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda unakatwa.
7. Rais Samia ana uwezo wa kujiharibia. Tusimharibie. CCM ina uwezo kujiharibia; haijaomba msaada wa kuisaidia kuharibu. Lipo kundi linalodhani linamsaidia rais Samia, wakati linamharibia. Lipo linalodhani linamharibia lakini linamjenga. Anayesimama na HAKI anamsaidia rais Samia.
8. Tuna tatizo kitaifa: Kuna watu wanatumia dini kueneza siasa. Na kuna watu wanatumia siasa kueneza dini. Mimi si mmoja wa hao wawili. Mimi natumia ujinga kueneza dini na siasa. Wajinga tu, ndio wananisikiliza na kunifuata. Wewe mjuaji kaa pembeni tuendelee na safari.
9. Nikisema jambo mkanishangilia, mnanipa kiburi cha kusema bila kufikiri.
Nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari; si kuhemuka. Mkishangilia, mnamnyima msemaji nidhamu ya kufikiri kabla ya kusema. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana.
10. Mungu analipenda Taifa hili kuliko mtu au chama chochote kinavyoweza kudai kulipenda. Usiombe Mungu akuonyeshe anavyolipenda hili taifa. Ina gharama nzito kushuhudia Mungu anavyolipenda hili taifa.
Hata anayerudi nyuma ana mbele anakoelekea. Ukisifiwa kuwa na mbio, jihadhari usipitilize nyumbani kwenu.
Source: FB page yake
Pia soma
Hivi huamini kuwa kuna watu wanaoweza kukataa kujitoa akili namna hiyo kwa sababu ya fedha? I mean mtu anaweza kuwa na shida kweli na akapokea fedha lakini angalau akapiga debe kwa kutumia akili na busara. BTW huyu askofu hizo alizokwisha chuma hazimtoshi mpaka afikie stage hii?Wewe hutaki bahasha?!
KKKT ni sawa na CCM. Kanisa lenye mfumo mzuri ni RC. RC ni mfumo na siyo one man show.Kifo cha Dr Erasto Kweka, kimemfanya Dr Shoo kutotawalika Tena.
Hata katiba ya dayosisi ameisingina.
Makochi hayatakalika...atalazimika kubeba vilago vyake , kama nilikuwepo!Siri ni nini? Akipiga mluzi anaharibu kitu gani?
Aisee.....! Ebu imagine, Elon Musk, boss wa Mtandao wa X na Tesla, amzulumu boda boda nauli ya Buku(tzs 1000/-); inaingia akilini kweli?Wewe hutaki bahasha?!
Wenzako wanaoandika pumba kama uliyoandika hutumia id fake.. sasa wewe unaandika jambo bila kushirikisha uongo kwa id halisi tena na picha lako umeweka.,!?!😭Shoo kama yuko CCM na Bagonza CDM kuna shida gani?
* Mbn Bagonza husema mengi lkn wenzake hawafuatilii wala kukosoa sapoti yk kwa CDM!
* Kuna mtanzania asojua msimamo wa Bagonza kuhusu CDM?