Askofu Bagonza: Lissu amekosea kueleza in details alichoongea na Rais, akiendeshwa na mashabiki

Askofu Bagonza: Lissu amekosea kueleza in details alichoongea na Rais, akiendeshwa na mashabiki

Lissu hajaongea ile summary bila idhini ya wasaidizi wa Rais.
Angekuwa kaamua yeye kuongea angeropoka sana Lissu
 
Summary ya pande zote mbili haiwezekani kiprotocal.
Samia ni Rais.
TL siyo Rais
hata mimi nililiona hili, nadhani hakupaswa kusema hayo yote..ingekuwepo na summary ya pande zote.

Rais ni rais tu..lazima apewe heshima yake
 
Mama huwa anajali sana kwa hilo nampa Hongera zake na Mnyaazi Mungu azidi kumpa maisha marefu kwa faida ya Watanzania sifa kuu ya Watanzania ni wakalimu mno mno..
 
Nakubaliana na wewe mia kwa mia ,wewe ndio mtu mwenye akili zaidi kuchangia mjadala huu.
Bila lisu kufanya hivyo kungetokea upotoshaji mkubwa na propaganda za hali ya juu kuhusu kikao hicho.
Lisu kichwa au waliomshauri afanye hivyo ni vichwa kwelikweli.
Asante kwa komenti hii.

CCM ni CCM tu mkuu, kuwaamini ni sawa na kujitia kitanzi.

Lissu amecheza vizuri sana.
 
Mama Samia,tunakuombea kwa Mwenyezimungu akujaalie umri mrefu uliojaa busara na hekima,akujaalie roho ya kusamehe na akufanyie wepesi ktk juhudi zako za kutu unganisha sisi watanzania.
TUSEME
Aaamiin

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Inawezekana hujamuelewa askofu. Ni kweli Lissu hakutakiwa kutoa taarifa ya walichozungumza unless otherwise kama wamekubaliana.

Naona kama inajenga taswira kwamba hata yale aliyoyasema japo ni ya msingi lakini Rais hawezi kutekeleza au kufanya jambo kwasababu eti Lissu kasema.
Siri ya nini?? Naomba jibu
 
Nakubaliana na wewe mia kwa mia ,wewe ndio mtu mwenye akili zaidi kuchangia mjadala huu.
Bila lisu kufanya hivyo kungetokea upotoshaji mkubwa na propaganda za hali ya juu kuhusu kikao hicho.
Lisu kichwa au waliomshauri afanye hivyo ni vichwa kwelikweli.
Asante kwa komenti hii.
Lissu hajawahi kuniangusha hata siku moja.
 
Katika mazingira ya Lissu kuwa ughaibuni na hana passport iwe imeibwa au ilipotea...ni lazima ujenge urafiki na serikali kwa udi na uvumba. Hizi vurugu zinatakaga uwe kwanza na passport
Kwani ndio Kusema Lissu sio Raia tena?
 
Ni kweli na hii inaonyesha hafai kuwa kiongozi mkubwa.

Rais kamheshimu amemfuata unless wangaitisha press ya pamoja.

Mh.Rais next time achana na Hawa wajinga wasio na adabu wala wasiojoelewa.
Maskini wa Roho maungulika sana moyoni.

Wachawi wote mmejulikana.
 
Uzuri ni kuwa SSH utu wake na busara zake zimepitiliza. Kuna wengine humu wangetamani TL wammalizie either kipindi akiwa hospitali au kule Ubelgiji.

Taifa linakuwa imara zaidi kama tunatofautiana mitizamo.
Let's embrace diversity!
Mama Samia amewaumbua wachawi wengi huko lumumba. Walikuwa hawapendi kabisa kitu kama cha Jana
 
Mkuu hapo tuta differ kidogo. Ukiangalia kwa makini, wasaidizi wa Ikulu na vuvuzela wa ccm walitaka kuanza kupotosha kwa kufanya neno "LISSU AMEOMBA KUKUTANA NA RAIS" kama agenda kuu. Kwani Rais atakutana na mpinzani wake kama tunavyokutana club au harusini? Lazima kuwe na maombi na nafasi ya ratiba iruhusu.
Lissu aliliona hilo la "ameomba" linaelekea kutumika vibaya hivyo amewa preempty kabla ya kufika mbali kwa kutoa contents za kikao chao kwani hakikuwa cha siri na amesifia maelewano ya walichozungumza na hata lugha ya picha inaonyesha.
Na kwa vile tamko la Ikulu limejieleza na hakuna pahala kauli ya Lissu ilupopingwa basi ni dhahiri lengo la Lissu limetimia.
Wanaobeza ni wale wenye tabia za kishenzi tu. Binadamu mwenye akili na busara anaelewa umuhimu wa Jambo lile.
 
Hapa duniani tunajukumu la kuwa na amani na watu wote!! Waebrania 12:14
Screenshot_20220218-000720.png
 
kwa mtazamo wangu Lissu sio mwanasiasa ni mwanaharakati, mwanasiasa anapozungumzia mazungumzo ya faragha huwa anabakisha na maneno
 
View attachment 2121877

Tuseme yote. Tulaumu kivyovyote. Lakini SSH kathibitisha yeye ni binadamu.
Tukimdharau huyu mama hasa wapinzani hakika Mungu atatuletea mtu kama Iddi Amini mana hajui wakati wa kujiliwa kwetu.

Mungu aliwaletea Waisrael Masihi Yesu Mwana wa Mungu akiwa mpole anayepigwa shavu na kugeuza upande wa pili lakini matokeo yake wakamuua na kumkejeli. Kilichofuata Palitoke uvamizi wa majeshi ya Rumi na kuisambaratisha Israel Kwa Karne 20 bila kuwa na Taifa.

Tumshukuru sana Mungu Kwa kutuletea Samia. Itachukua miaka mingi sana kumpata Mtu kama Mama Samia hasa Afrika.
Ana makosa madogo madogo kwenye namna ya kupanga safu yake yenye wazalendo wa kweli.
Chanzo ni Chama chake kilichojaa walafi na wahuni. Chama ambacho ndicho tatizo kuu kwenye nchi hii. Chama kinachoweza kufanya uovu wowote alimradi kishinde Kwa asilimia 90.

Tumuunge mkono mama Samia ili aiunganishe nchi kimaendeleo na kijamii na kisiasa pia
 
Ulitaka nani aseme?.Mwenye agenda zakumwambia rais alikua Lissu sasa ulitaka rais ndiye aje aseme kua niliongea na lissu na kaniambia kesi ya mbowe ni kesi ya mchongo..Rais hana sababu yoyote yakuelezea umma mazungumzo ya lisu yalivyokua maana yaye yuko kwenye upande wa kutekeleza hoja alizoletewa ila lissu ana sababu kwasababu mazungumzo yale yanafaida kwake,chama chake na hali ya kisiasa kwa ujumla.na amefanya vyema kueleza ili wananchi tujue na tumsubiri rais aamue atakalo amua.sasa sijui vichwa vyenu vinatakaje.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu agenda walioamusha Mh Rais na Mh Lissu kwanza ni pigo kwa sukuma gang na the Unknown. Pili inaibua nyoka woote wanafiki.
 
Back
Top Bottom