Askofu Bagonza: Lissu amekosea kueleza in details alichoongea na Rais, akiendeshwa na mashabiki

Askofu Bagonza: Lissu amekosea kueleza in details alichoongea na Rais, akiendeshwa na mashabiki

Tukimdharau huyu mama hasa wapinzani hakika Mungu atatuletea mtu kama Iddi Amini mana hajui wakati wa kujiliwa kwetu.

Mungu aliwaletea Waisrael Masihi Yesu Mwana wa Mungu akiwa mpole anayepigwa shavu na kugeuza upande wa pili lakini matokeo yake wakamuua na kumkejeli. Kilichofuata Palitoke uvamizi wa majeshi ya Rumi na kuisambaratisha Israel Kwa Karne 20 bila kuwa na Taifa.

Tumshukuru sana Mungu Kwa kutuletea Samia. Itachukua miaka mingi sana kumpata Mtu kama Mama Samia hasa Afrika.
Ana makosa madogo madogo kwenye namna ya kupanga safu yake yenye wazalendo wa kweli.
Chanzo ni Chama chake kilichojaa walafi na wahuni. Chama ambacho ndicho tatizo kuu kwenye nchi hii. Chama kinachoweza kufanya uovu wowote alimradi kishinde Kwa asilimia 90.

Tumuunge mkono mama Samia ili aiunganishe nchi kimaendeleo na kijamii na kisiasa pia
Uko sahihi. Tuendelee kumwombea Mama Samia huko chamani kwake kuna machatu wengi
 
Naunga mkono!

Lissu hana kifua kipana kama Mbowe!
Mnakumbuka Maalif Seif na Mbatia walizungumza na Rais Samia Ikulu?

Walipotoka utadhani walikuwa wametekwa. Kimyaa. Then what happened? Tunajua waliongea nini??

Putin na Joe biden wanaongea mambo mazito ya kiusalama na wakimaliza wana publish walichoongea sembuse maongezi ya kawaida ya mapatano ya Mtu na Mdogo wake??
 
Hivi kuna siri gani katika kuelezea kuwa Serikali imejidhalilisha sana kwa kesi hii ya Mbowe.
Hata sisi wana CCM tunalijua hilo.
Mama amekuwa muungwana kupata maoni ya upande wa pili, hili litambeba.
Acha uongo. Wewe ni CHADEMA asilia.
 
Kwani kukutana Rais mlitaka iwe siri ? Naunga mkojo hoja...kila upande ulimuhitaji mwingine.

Lissu kafanya uwakilishi mpana kwa taifa, mama na yeye kwa niaba ya Serikali kaupiga mwingi tu.

Watu wanataka ligi eti nani alimwomba mwenzake kukutana? na ni nani mshindi na nani kapoteza etc..

Mshindi ni Tanzania.
Umeongea ukweli tena kwa jicho la tatu, tatizo baadhi wanataka kulifanya mmojawapo kati ya Lissu au Raisi aonekane Underdog
 
Mnakumbuka Maalif Seif na Mbatia walizungumza na Rais Samia Ikulu?

Walipotoka utadhani walikuwa wametekwa. Kimyaa. Then what happened? Tunajua waliongea nini??

Putin na Joe biden wanaongea mambo mazito ya kiusalama na wakimaliza wana publish walichoongea sembuse maongezi ya kawaida ya mapatano ya Mtu na Mdogo wake??
Maalim Seif na Mbatia wako derikalini.
 
Acha uongo. Wewe ni CHADEMA asilia.
Nyie ndio wale CCM wajinga wajinga mlio ingia mjini na mbio za mwenge na ushabiki mbuzi wa kusgabikia mtu na si misingi ya chama.
Sie CCM asilia tunawatazama tu.
 
Wewe ni chizi na Zezeta sana. Kuna mtu unaweza kuonana na rais kienyeji bila kukaguliwa? Kukaguliwa kwa Lisu Ni protoko ya kawaida ulizo kiazi unachukulia kuwa ni Jambo kubwa sana
 
Bahati mbaya katika hili kuna wanaojifanya wana umuhimu zaidi ya wengine....sio sahihi hii nchi ni yetu wote...
 
Akili kubwa hii mku
Siri ndio chanzo cha wizi,ufisadi na mikataba mibovu.

Lissu ni mtumishi wetu na anawajibika kwetu sisi wananchi na wanachama,siri ya nini wakati matatizo yetu yanajulikana!?

Hizo siri mfanye na hao wenza wenu sio ktk kazi hizi za wananchi.
Jicho la mwewe umeona mbali sana
 
Lissu amefanya vile ili kusiwepo na aina yoyote ya kukasalitiana. Ikumbukwe leo Rais alitakiwa kukutana na uongozi wa EU hivyo kikao na Lissu ni turufu kwa serikali ya SSH kuliko kwa Lissu.

Kwa vyovyote, Rais alitaka kujenga hoja ya kuwa na nia njema ya kuanzisha mjadala na upinzani hususani Lissu ambaye yupo ukimbizini alikokwenda kupitisha bakuli.

Kwa Lissu kutoka hadharani na kusema yale, Rais anafungwa na hawezi kumgeuka Lissu kwenye zile hoja, labda atashindwa kutekeleza makubaliano kwa shinikizo la chama chake lakini dunia itajua hakuwa mkweli katika mjadala. Lissu asingetumia ile fursa, hoja zingepitishwa kinyemela katika meza ya mazungumzo na viongozi wa EU alafu rais akirudi nchini anaamua kupotezea, hapo tayari Lissu anakuwa ametumika.
Kweli tupu
 
Nyie mnajuaje kasema yote? Mlikuwepo kwenye kikao au ni hisia zenu zinawatuma kuwa Lissu kaongea yote? Mnajuaje kazungumza kuwawin wazee wa kulisha maneno kaamua kuwawahi
najua kuwa walizungumza mengi.. mm nasemea hayo aliyoyasema
baadhi utaona ni kama anatoa maagizo au masharti kwa raisi.. kitu ambacho naona sio sawa
 
Yesu Kristo alisema maneno yetu yawe machache yaani Ndio au Siyo kwa maana maneno mengi yanatoka kwa yule mwovu.

Wakati mwingine hakunaga sababu ya kuweka hadharani mambo yaliyojadiliwa faraghani.

Maendeleo hayana vyama!
 
Nilimwambia bwana mmoja hakunielewa, ingawa Lissu anajua vitu vingi lakini bado hayuko stable katika kuonesha maturity yake.

Na ndiyo hii inatia mashaka uwezo wa oposition kushika nchi japo tunawasuport....

Kwa alichokileta Lissu hadharani, mahakama ingeamua vinginevyo ingeweka msingi mbaya sana kwa serikali na mifumo mizima ya kuendesha nchi.

Lissu akue.
 
Back
Top Bottom