Askofu Bagonza: Tujifanye kuuliza - Kanisa ni mali ya mtu? Kama kakosea yeye, kwanini kanisa lifungwe?

Askofu Bagonza: Tujifanye kuuliza - Kanisa ni mali ya mtu? Kama kakosea yeye, kwanini kanisa lifungwe?

Weeee, mimi siyo rahisi kutafuna matango pori yako.
hapa tunajadili masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi,
masuala ya kutafuna matango yenu kishirikina mafanye huko huko gentleman bila kusumbua wadau wasio husika :NoGodNo:
 
hapa tunajadili masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi,
masuala ya kutafuna matango yenu kishirikina mafanye huko huko gentleman bila kusumbua wadau wasio husika :NoGodNo:
Ondoa bango lako la kizushi juu ya askofu ni mzinzi ili usumbufu isiendelee. Asante.
 
Bangoza kakuachq mbali sana kwa kila kitu humuwezi wewe kima , hata KKKT na RC yote ni makanisa ya watu labda kama hujui historia za kuanzishwa kwake
Najua hiyo ndiyo hulka yenu..ebu niambie leo KKKT na RC hapa Tanzania yanamilikiwa na nani?
 
Yaani unazungumzua asili leo wakati issue umeulizwa nani anayamiliki daah
Hizo zote ni taasisi kongwe na zenye wamiliki ila zimekua na kuenea ndio maana hujui kama zina wamiliki sasa jua tuu, roman katoliki ni taasisi ya mtume petro ndiye muasisi na baadae limekua na kukomaa hadi lika sambaa dunia nzima likawa kubwa ,

Na KKKT mmililiki nq muasisi ni martin luther nayo ni taasisi kongwe imekuwa na kukomaa na ikasambaa dunia nzima

Hivyo hataka ufufuo na uzima ni tasisi nayo itakuwa na kukomaa na itakapo vuka mipaka ya nchi na kuwa kubwa sana kwa miongo kadhaa ndipo wao wa zama hizo watakapo dhani ni kanisa lisilo na mmiliki kama unavyo amini wewe kwa KkKT na Roman katholic
 
na kwasababu ya ufuska ya hao wazinzi madhabauni ndio mmezaliwa waropokaji kama wewe :NoGodNo:
Tanganyika pekee nchi ambayo kwanza inatawaliwa na Raia wa kigeni anaye wakandamiza wazawa na kuwanyanganya ardhi na kuwapa wageni halafu wazawa hao hao wenye ardhi yao wanamshangilia na kumpigia makofi , nchi ina vialaza wakutosha hii!
 
Tanganyika pekee nchi ambayo kwanza inatawaliwa na Raia wa kigeni anaye wakandamiza wazawa na kuwanyanganya ardhi na kuwapa wageni halafu wazawa hao hao wenye ardhi yao wanamshangilia na kumpigia makofi , nchi ina vialaza wakutosha hii!
Gentleman,
hiyo nonsese imebaki historia tu but hakuna kitu kama hicho, sijui ati tanganyika n.k.
mihemko ya mdau yeyote wa JF daima itapuuzwa na Tanzania itaongozwa bila fikra potofu za kibaguzi na kusonga mbele :pulpTRAVOLTA:
 
Mambo haya yalianza Polepole ila haikuwa raisi kuyaona. Kwasasa tunaona kama CCM na Serikali yake inafanya makosa mengi sana lakini ni hakika chama chochote kingepewa hayo mamlaka pia kungekuwa na tatizo la aina yake.
Tukumbuke na kutambua kwamba CCM ina wafuasi wanaokipenda na kukikubali pia Wapinzani wa CCM wanao wafuasi wa kutosha hivyo basi kila siku kutakuwa na wanaovita kamba kuelekea kwao kwa kuzingatia nguvu watakazokuwa wamejikusanyia.
Tumefikaje hapa? Majibu ni mengi na moja wapo ni hapo zamani za kale tulipokuwa tumetawaliwa na Mkoloni tulianzisha mapambano dhidi ya mkoloni ili akiondoka tuishi kama mkoloni na tukafanikiwa tukaiga mbinu alizozitumia ili kulinda maslahi yake na mbinu mojawapo ilikuwa ni kutugawa ili atutawale. Kwa bahati mbaya jamii yetu imegawanyika katika matabaka lukuki jambo ambalo leo ukitaka kuwaunganisha ni lazima utumie akili ya kukubali kuto kukubaliana na ni wachache sana wenye kipaji cha kuunganisha watu wenye itikadi tofauti na kufikia malengo wanayoyataka.Tulivyo anza miaka ile baada ya uhuru katika kila sekta kuanzia elimu kulikuwa na ubaguzi wa kutisha watoto wetu walikuwa wanapunguzwa makali kuanzia uchaguzi wa kuendelea na masomo ya Sekondari wakati ule shule za serikali zilikuwa zinatoa mwanafunzi mmoja hadi saba kwenda secondary na kuwaacha Mamia ya watoto wasijue cha kufanya baadaye zikaanzishwa Private School ambazo ziliwahusu wale wenye mali. Pamoja na madhila hayo kukaingia mdudu mmoja anaitwa kuiba mitihani,kutafuta vyeti feki ili kupata ajira nk. Hicho kipindi janja janja ilitamalaki tukatengeneza kizazi cha dili,connection nk.
Sasa tunavuna tulichokipanda bado uongozi wa kisiasa umebakia kuwa ni ajira kwa manufaa ya familia zao badala kuwa kazi ya kujitoa ili kuwakomboa watu wote bila kujali tabaka. Kwasasa Chuki uhasama vinaongezeka ili kulinda kubakia madarakani. Nini kifanyike? Tunatakiwa kuainisha mahitaji ya nchi alafu tuweke mipango ya kufikia mahitaji yetu (Katiba) katika malengo tuweke sheria kali dhidi ya mtu atakaye kwenda kinyume na mipango tuliyojiwekea(Katiba) Polisi wasimamie utekelezaji wa sheria kama ambavyo kwasasa wanalaumiwa kusimamia mambo ambayo hatujakubaliana.
Polisi ni kama ilivyo kwa Silaha siku zote Silaha haina shida lakini itabadilika kulingana na mtu atakayeishika na kuitumia ikishikwa na kichaa tegemea hatari wakati wowote inaweza kutokea.
 
Maneno mazito ya askofu mpigania haki huyu anaandika:

KAMA NI KWELI: Inaweza kumaanisha hivi..

Eti Kanisa Limefungwa au kufutiwa usajili. Kisa? Kiongozi wake kakosana na waliomsajili au kadaiwa kuhubiri kinyume na alivyotegemewa.

Kama ni kweli; tujifanye kuuliza? Kanisa ni mali ya mtu? Kama kakosea yeye, kwa nini kanisa lifungwe? Yaani mdomo utoe matusi halafu makalio ndiyo yachapwe kiboko?

Hakuna kanisa linalotuma mtu kuchochea, kutukana, kubaka, kuiba nk. Kama lipo, zipatikane miniti za kikao kilichoruhusu hayo. Kinyume na hayo ni kuingilia uhuru wa watu kuabudu. Uhuru wa kuabudu ni wa msingi sana maana unaruhusu hata kuabudu watawala. Tusiwachagulie watu ibada.

Bado siamini kama ni kweli kwa sababu zimetoka barua mbili: moja ina sahihi na nyingine haina sahihi.

Kama ni kweli kanisa limefungwa, maana yake yaweza kuwa hii;
1. Tangu sasa viongozi wote wa dini zote, watatakiwa kutoa nakala ya mahubiri yao kwa wakuu wa serikali siku mbili kabla ya ibada ili yahakikiwe.

2. Maimamu, mashehe, mapadre na wachungaji walio kwenye maeneo ya kata, wawasilishe mahubiri yao kwa Maafisa Watendaji wa Kata siku mbili kabla ya ibada.

3. Endapo Maafisa wa serikali watakosa muda wa kupitia na kuhariri mahubiri hayo, ibada ziahirishwe kusubiri uhariri huo.

4. Atakayehubiri bila kuhaririwa na akaenda kinyume, faini pekee haitoshi, kifungo kina unafuu bali kanisa/hekalu/msikiti utafungwa.

5. Maafisa wa serikali ngazi zote watatakiwa kwenda kozi ya kujifunza elimu ya dini na Teologia ili kufanya udhibiti huu kwa umakini.

6. Maafisa wote wa serikali itabidi wazikane dini zao ili wasije kuonea au kupendelea dini yoyote.

7. Upelekwe muswada bungeni haraka sana, tena kwa hati ya dharula, ili kubadili katiba na kutamka kuwa serikali yetu sasa ina dini rasmi isiyotamkika jina lake na dini nyingine zimefutwa na kubakiza hiyo dini ya serikali.

8. Viongozi hawataruhusiwa tena kuapa kwa misahafu ya dini zilizofutwa. Misahafu hiyo itakuwa imefikia ukomo wa matumizi maana inasababisha viongozi wa dini kufanya uchochezi.

9. Sikukuu za kidini zinafutwa rasmi na hakuna mapumziko siku hizo.

10. Mahusiano ya kibalozi na nchi zote zenye kutambua uwepo wa dini zilizofutwa au kufungiwa yanafungwa mara moja. Mabalozi wa nchi hizo walio nchini waondoke na mabalozi wa kwetu walio nchi hizo warejee nyumbani.

11. Tangu sasa ni marufuku kuomba sala ili kula chakula na ndoa zote zenye uhalali wa kidini hazitambuliki tena.
12. Wimbo wa Taifa uondoe neno Mungu kwa sababu Mungu huyo anaweza kuleta uchochezi wakati wowote.

Tulianza na uhuru wa kukusanyika, tukaja uhuru wa kuishi, tukaingia uhuru wa maoni, hatimaye tutakuwa tumeingia uhuru wa kuabudu. Imebaki nini? Uhuru wa kujinyonga?

I hope ninaota siyo kweli. Ni mitandao tu inazusha na kufanya uchochezi.


Sauti yake imesikika.

Bila shaka na nyingi nyingine zitasikika.

Kanisa si mtu!
Ni mpaka pale wamiliki wa makanisa watakapokataa majina yao kutumika kwenye makanisa yao na sadaka na mali za kanisa kunufaisha wanakanisa wote kwa usawa ndipo swali lako litapata majibu sahihi.

Kuna makanisa ambayo ni mali ya mtu kama vile kwa Kakobe, Kwa mwamposa, Lusekelo, Rwakatale, kanisa la gwajima, mwingira, mtume G, nk. Haya ya hivi ni makanisa ya watu, mwenye kanisa akikosea na kanisa litaathirika. Kuna makanisa ambayo kama mwenye kanisa hayupo na mahubiri hakuna, labda waweke CD/video zake waumini wasikilize. Sadaka na malimbuko yote yanakwenda kwenye mkoba wake. Yeye ndio anaeamua mapato yatumikije.

Au nakosea?
 
MAKANISA YAKO MENGI TUH WHY HAYAGUSWA LIGUSWE LA GWAJIMA??

NA MLIKUWA WAPI KUMKEMEA WAKATI ANATENGENEZA CHUKI KWA WANANCHI DHID YA SERIKALI??

KANISA LILE NI LA GWAJIMA,NA LIMEFUNGIWA KWA KUWA MTOA HUDUMA NI HUYO GWAJIMA MCHOCHEZI,KAMA UNAONA KUNA HAKI IMEVUNJWA AKAKATE RUFAA,ACHENI CHUKI ZENU
Wao wameanza kukemea matukio kabla hata gwajima hajaanza.
Kwann aliposnza gwajima tu vipingamizi vikainuka?

Au kuna double standards
 
Back
Top Bottom