TUME HURU na MGOMBEA HURU
2020 ni mwaka wa Uchaguzi. Kama huchaguliwi basi unachagua. Kama hupigiwi kura na hupigi kura lazima kuna sababu inayokuzuia. Kuna watu wengi wanaruhusiwa kupiga kura lakini hawaruhusiwi kupigiwa kura. Wana haki ya kuongozwa tu lakini hawaruhusiwi kuongoza. Katiba yetu haitaki kujishighulisha na tatizo hilo. Una haki ya kupiga kura lakini huruhusiwi kupigiwa kura.
Vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu, vimetanguliza tamaa ya kupata madaraka bila kujali kundi kubwa linalopiga kura lakini haliruhusiwi kupigiwa kura. Hii ni kasoro kubwa sana.
Baba wa Taifa katika hotuba yake ya kustaafu uenyekiti wa CCM mwezi Agosti 1990, alituonya hivi:
"Lakini ni vizuri nikasema pia kwamba kwa maoni yangu hatuwezi tukaamua kuacha mfumo wa Demokrasia ya Chama Kimoja na tukajaribu mfumo wa Demokrasia ya Vyama vingi, kwa matumaini ya kwamba tukikuta kuwa mfumo huo hautufai, basi tutarudia tena Demokrasia ya Chama Kimoja. Tutajidanganya, haiwezekani na ni vigumu kabisa. Ukimwacha mkeo ukaoa mke mwingine na ukagundua kuwa huyu wa pili ni balaa, ni vigumu kumrudia mkeo wa kwanza. Demokrasia ya Vyama vingi, ikitushinda, mfumo ambao ni rahisi kufuatia utakuwa ni udikteta wa mtu mmoja au utawala wa kijeshi.”
Unabii wa Baba wa Taifa unaelekea kutimia. Ndani ya vyama vingi vya siasa kuna changamoto nyingi sana na demokrasia ndani ya vyama vyote ina hali mbaya sana. Viwango vya umakini vimeshuka sana katika vyama vyote. Katika miaka ya hivi karibuni kumejitokeza jambo la ajabu ambalo ni la kuwakatisha kabisa tamaa wananchi kushiriki katika mchakato wa uchaguzi. Kiwango cha wanasiasa kuhama vyama vyao na kusababisha ukiukwaji wa katiba na ustaarabu wa kitanzania kinatisha. Wanasiasa wengi wamekuwa wanahangaika miaka nenda rudi kutoka chama X kwenda Y na kutoka chama Y kwenda X. Idadi ya wapiga kura inaweza kushuka sana kwa sababu ya kukosekana kwa umakini katika kuhama na kupokea. Aidha, watu wengi sasa wanaamini upigaji kura si muhimu kama kuhesabu kura.
Changamoto hii inadhihirisha mambo mawili ambayo yamekuwa kilio cha Watanzania kwa muda mrefu bila mafanikio:
1. Hitaji la kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi
2. Mgombea Huru.
Bunge letu limeishavunjwa. Hakuna fursa ya kudai mabadiliko ya katiba ya kuruhusu hivi vitu muhimu kwa ajili ya afya demokrasia na amani ya nchi yetu. Na haya hayawezi tena kupatikana bila wananchi kuonyesha kwa vitendo kuyahitaji. Duniani kote njia moja ya kufikisha kilio cha watu ni kupitia maandamano ya Amani. Na Watanzania vile vile hawana historia ya kufanya vurugu kudai haki zao. Mfano mzuri ni Uhuru wetu wa 1961 ambao tuliupata bila kumwaga damu.
Pendekezo langu kwa Watanzania wote wanaoitakia mema nchi hii na kutaka kuona Demokrasia ya Vyama Vingi inastawi ni kuitikia wito wa kudai haki hizi mbili kwa njia ya amani.
Tarehe 7 ya mwezi wa 7 ni siku ya Saba Saba. Hii tarehe ina historia yake kuhusiana na kuanzishwa kwa chama cha ukombozi cha TANU. Chama hicho kilichoizaa CCM kinasifika kwa kuleta uhuru kwa amani. Siku hiyo kila mtanzania avae shati/gauni/koti/suruali/kofia/viatu/soksi/tai/ nyeupe kama ishara ya kuienzi amani ya taifa. Na amani ya kweli na endelevu katika Taifa letu ni kuunga mkono uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na mgombea huru katika chaguzi zetu.
Vyama vyote vya siasa vinaalikwa kuunga mkono kampeini hii. Mnufaika mkuu wa kampeini hii ni Mama Tanzania. Ushindi wa mezani, ushindi unaotokana na kasoro za kujaza fomu na utumwa wa kukitumikia chama kuliko nchi ni kasoro kubwa katika chaguzi zetu.
Mama Tanzania ni yetu sote!! Mungu Ibariki Tanzania!!
Mwana kulitafuta na kulipata
Kalikawe Lwakalinda Bagonza